Wimbo 97
Sifa za Yehova
1. Yehova mwenye nguvu kubwa,
U chanzo cha uzima na
Wakuzwa na uumbaji;
Na Har-Magedoni pia.
2. Uliumba kwa hekima, lo!
Viumbe vyasifu hilo.
Neno lako twatazama,
Twaona nyingi hekima.
3. Haki ni musingi wa enzi.
Adili umejulisha.
Tupe masikio wewe,
Kwa hofu tuende nawe.
4. Fadhili zako twajivuna;
Tunadaiwa zaidi.
Sifa, jina lako kuu,
Tutatangaza kwa shangwe!