Wimbo 86
Kulisitawisha Tunda la Upendo
1. Yehova kwa pendo awapa
Wahudumu wa chini hapa
Zawadi ili watende
Penzi lake takatifu.
Wathamini roho yake,
Wakuze matunda yake;
Tunda watunzalo sana
—Ndilo tunda la upendo.
2. Sifa zote za kuhudumu
Twajaribu kuzitumia;
Twajikaza kipekee
Muhimu kukamilisha.
Akili hazitatosha
Ili kulisha kondoo;
Bali tutoe kwa moyo
Tuwabariki wengine.
3. Tufanyapo kwa ongezeko
Na tulinde ile amani.
Mabaya tuvumilie;
Wanyonge tusaidie.
Tuhisi na kwa madogo
Furaha ya bila choyo;
Upendo ukamilishwe
Tuwe kama Mungu juu.