Wimbo 137
Wakati Uliowekwa Wakaribia
1. E Yehova, Ndiwe Mwamba
wa tangu kale,
Ungurume Sayuni;
Nawe uhukumu.
Hata ikikawia,
Haitachelewa.
Lo! Mwisho waja haraka;
Twasubiri basi.
2. Karibuni utauchomoa
upanga.
Duniani twaona
Ibada ya kweli.
Na ingawa waovu
Watake kudhuru,
Wakati wako
karibu uliouweka.
3. Bwana Mungu, Ewe jina
lako Yehova.
Na wote wanyamaze
Wakujue wewe.
Kupitia Mwanao
Watawala wewe.
Unatawala, E Mungu,
Juu ya dunia.
4. Twafurahi kuimba; Kwako
Ewe Mungu.
Waondoka na Yesu
Kuleta wokovu.
Uliye Juu huu
Ni wakati wako.
Tunakungojea sana
Ushinde kabisa.