Wimbo 61
“Mimi Ni Yehova”!
1. Ona wafalme wapagani
Wamupuuza Yehova.
Waikataa enzi kuu yake,
Uweza wake wakaidi.
Lakini nani alishinda majeshi yao,
yote yakafa fo fo?
Nani kakomesha kiburi chao
Akapa ushindi watu wake?
(Korasi)
2. Ona tawala zaungana
Dhidi ya Mwanaye Mungu!
Hofu yashika mashujaa wao,
Hali maskini waugua.
Ni nani ’tavunja kongwa la mwonezi
akomboe wanyenyekevu?
Na ni nani atawaadilisha
Afanye huzuni yao shangwe?
(KORASI)
Mimi Bwana; na ni mimi tu.
Jina langu naitwa Yehova.
Mufalme nimeweka mulimani
Utiini utawala wake.