Wimbo 57
Watu wa Yehova Wenye Furaha
1. Wana furaha wenye vigelegele,
Wenye kweli ile, na baraka tele.
Wataenenda nuruni mwa uso wako;
Wafurahi wakijitumikisha.
(Korasi)
2. Shetani, majeshi yake watusonga;
Kazi zidisheni, Sifa vumisheni.
Kwao wapole Yehova ni kimbilio;
Atakinga watafutao haki.
(Korasi)
3. Ijapo wengi waukane ukweli.
La hatufi moyo, Tulinde, tusali.
Na tulishinde jaribu pia kushika
Ukamilifu; Mungu apendezwa.
(KORASI)
Mungu fadhili Wazionyesha
Kwa wote wahubiri jina lako.
Kwa neno, roho, kweli waijua,
Waonyesha imani kwa kazi.