Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matangazo
    Huduma ya Ufalme—2004 | Mei
    • Matangazo

      ◼ Toleo la vichapo la Mei: Toa magazeti ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Unapowarudia watu wanaopendezwa, kutia ndani wale ambao huhudhuria Ukumbusho au matukio mengine ya kitheokrasi lakini hawashirikiani na tengenezo, jitahidi kuwatolea kitabu Mwabudu Mungu. Jitahidi sana kuanzisha funzo la Biblia la nyumbani, hasa na watu ambao tayari wamejifunza kitabu Ujuzi na broshua Anataka. Juni: Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu. Watu fulani wakisema kwamba hawana watoto, watolee broshua Anataka. Jitahidi kuanzisha mafunzo ya Biblia ukitumia broshua hiyo. Julai na Agosti: Broshua yoyote kati ya broshua zifuatazo zenye kurasa 32 yaweza kutumiwa: Furahia Milele Maisha Duniani!, Je! Kweli Mungu Anatujali?, Je! Uamini Utatu?, Jina la Mungu Litakaloendelea Milele, Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa, Ni Nini Hutupata Tunapokufa?, Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai—Wewe Waweza Kulipataje?, Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je! Ziko Kweli?, Serikali Itakayoleta Paradiso, na “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya.”

      ◼ Mwangalizi-msimamizi au mtu fulani aliyeteuliwa naye apaswa kukagua hesabu ya kutaniko Juni 1 au upesi iwezekanavyo baada ya tarehe hiyo. Jambo hilo lifanywapo, tangazieni kutaniko baada ya ripoti ya hesabu kusomwa.

      ◼ Wanafunzi wa darasa la 15 la Shule ya Mazoezi ya Kihuduma nchini Kenya walihitimu Januari 25, 2004. Wanafunzi hao 24 walitoka Ethiopia, Kenya, Sudan, Tanzania, na Uganda. Programu hiyo iliwatia moyo sana wanafunzi na pia wale waliohudhuria. Ndugu waseja wenye umri wa kati ya miaka 23 hadi 50 ambao wangependa kuhudhuria shule hiyo wanaweza kupata habari zaidi katika mikutano inayofanywa na mwangalizi wa wilaya wakati wa kusanyiko la mzunguko. Lazima wawe wazee au wawe wametumikia wakiwa watumishi wa huduma kwa angalau miaka miwili mfululizo.

      ◼ Darasa la kwanza la Shule ya Waangalizi Wanaosafiri lilifanywa Februari 20 hadi Aprili 17, 2004. Madarasa mengine mawili yatafuata. Waangalizi wanaosafiri kutoka Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Tanzania, na Uganda watahudhuria.

      ◼ Kuanzia Juni, fomu za kila mwaka zitatiwa ndani ya upakizi wa vichapo wa kutaniko zikipatikana. Maagizo kuhusu jinsi ya kuzigawanya fomu hizo yatapatikana kwenye orodha ya upakizi. Ikiwa makutaniko kadhaa yanatumia Jumba moja la Ufalme, mratibu wa vichapo anapaswa kuhakikisha kwamba kila kutaniko linapokea fomu zake mara tu zifikapo.

  • Kutoa Kitabu Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
    Huduma ya Ufalme—2004 | Mei
    • Kutoa Kitabu Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu

      ◼ “Je, unafikiri ulimwengu ungekuwa mahali pazuri ikiwa watu wangefuata maneno haya? [Soma Mathayo 7:12a. Kisha ngoja jibu.] Kitabu hiki kina mafunzo mengi kutoka kwa mwalimu mkuu zaidi aliyewahi kuishi.” Kazia picha na maelezo yaliyo kando ya picha kwenye sura ya 17.

      ◼ “Wazazi wengi leo hujaribu kuwafundisha watoto wao maadili mazuri. Je, unafikiri ni muhimu kufanya hivyo? [Ngoja jibu. Kisha soma Methali 22:6.] Ona kwamba wazazi wanatiwa moyo kuanza kuwafundisha watoto wao wakiwa bado wachanga. Kitabu hiki kimekusudiwa kuwasaidia kufanya hivyo.” Kazia picha na maelezo yaliyo kando ya picha kwenye sura ya 15, 18, au 32.

      ◼ “Mara nyingi, wazazi hushangazwa na maswali ambayo watoto wao huuliza. Si rahisi kujibu baadhi ya maswali hayo, sivyo? [Ngoja jibu. Kisha soma 2 Timotheo 3:14, 15.] Mama na nyanya ya Timotheo walimfundisha Maandiko tangu utotoni. Kitabu hiki kinaweza kuwasaidia wazazi wawafundishe watoto wao vivyo hivyo leo.” Kazia picha chache na maelezo yake kwenye sura ya 11 na 12 au 34 mpaka 36.

  • Ripoti Ya Utumishi Ya Januari
    Huduma ya Ufalme—2004 | Mei
    • Ripoti Ya Utumishi Ya Januari

      Wast. Wast. Wast. Wast.

      Idadi ya: Saa Mag. Z.K. Maf. Bi.

      B

      Pai. Pekee 102 139.9 17.3 83.4 14.9

      Mapai. 517 66.5 5.0 31.4 6.1

      Pai. Msai. 223 56.5 4.6 23.8 4.4

      Wahu. 4,295 17.4 1.5 7.7 1.7

      JUMLA 5,137 Kilele Kipya: 5,137

      ER

      Pai. Msai. 17 56.1 1.4 14.1 0.9

      Wahu. — 14.4 0.5 4.6 0.4

      K

      Pai. Pekee 329 126.1 35.7 51.3 10.4

      Mapai. 2,157 65.1 19.2 22.5 4.5

      Pai. Msai. 677 52.4 15.0 15.5 3.2

      Wahu. 14,831 14.2 5.9 4.7 1.0

      JUMLA 17,994 Kilele Kipya: 17,946

      S

      Pai. Msai. 44 55.6 21.1 40.4 3.5

      Wahu. — 12.8 6.3 10.2 1.3

      T

      Pai. Pekee 202 126.0 40.4 61.0 9.7

      Mapai. 1,271 61.9 17.7 25.4 4.3

      Pai. Msai. 365 50.5 14.3 21.3 3.6

      Wahu. 9,597 13.1 5.8 5.6 1.1

      JUMLA 11,435

      U

      Pai. Pekee 90 127.3 42.3 72.2 11.4

      Mapai. 331 65.3 20.2 32.9 5.6

      Pai. Msai. 263 57.8 14.0 23.3 3.7

      Wahu. 2,757 13.9 6.0 6.4 1.4

      JUMLA 3,441

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki