Wimbo 68
Huruma za Kimungu
1. Sisi Wakristo halisi,
Tuonyeshe huruma
Wapenzi pia wageni,
Na tusiowajua.
Na Mwalimu Yesu
Alifundisha hivyo
Wazi kwa mufano.
Shangwe wasikiao.
2. ‘Samaria safarini
Akienda Yeriko.
Kaona ’Yahudi chali;
Aliyeshambuliwa.’
Alisaidia,
Pasipo ubaguzi.
Ni upendo huo.
Amri za Mungu hizo.
3. Huo ndio ujirani,
Kusaidia watu.
Mungu hufadhili wote,
Atoa jua, mvua.
Anahurumia!
Yehova ni Rafiki.
Anazo fadhili.
Anatumainika.
4. Na tuwape majirani
Chakula na mavazi.
Lakini tuwape haja
Ya muhimu zaidi.
Wajue ukweli,
Ufalme na adili
Tweleze jirani
Mungu awabariki.