Wimbo 186
Furaha Yetu ya Kimungu
1. Kusudi tuvumilie
Tuwe na furaha.
Kuwa na furaha hii
Tuwe na imani.
Si furaha ya muda tu;
Yatakwa daima.
“Furahini”! “Furahini”!
Ndivyo tunasoma.
2. Twafurahi kwa kujua:
Mungu na Mwanaye;
Sisi mashahidi wao;
Tu umoja nao.
Ni furaha siku moja
Wote ’tasifu Yah,
Waliomo kaburini
Kufuata Mungu.
3. Ili kukuza furaha
Tuhudumu Mungu,
Tulinde mioyo yetu
Tuepuke baya.
Tuwe macho siku kutwa
Kumusifu Mungu;
Tufikiri yajengayo,
Tuepe mabaya.
4. Tujaposongwa nuruni
Tunapotembea,
Furaha ndiyo thawabu
Kwa kumuhudumu.
Hututambulisha kuwa
Watumwa wa Mungu.
Lazima furaha hii
Tuwape wengine.