Wimbo Na. 113
Kulithamini Neno la Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Ee, Yehova Baba, Twakushukuru,
Kwa kutupa Neno lako la nuru!
Roho iliongoza, walioandika.
Twafundishwa nawe, twafaidika.
2. Nalo Neno lako, latuvutia.
Manabii walilizingatia.
Tujifunzapo Neno, tunaimarishwa;
Tunatiwa nguvu; twaburudishwa.
3. Neno lina nguvu, lapenya moyo,
Nalo hugawanya nafsi na roho.
Hutambua fikira na makusudio.
Huturekebisha tuhekimike.
(Ona pia Zab. 119:16, 162; 2 Tim. 3:16; Yak. 5:17; 2 Pet. 1:21.)