Wimbo Na. 90
Kichwa Chenye Mvi—Taji la Uzuri
Makala Iliyochapishwa
1. Twawaona wazee,
Pamoja nasi.
Wanaovumilia;
Waaminifu.
Nguvu wamepoteza,
Ama kufiwa.
Baba, tunakuomba,
Uwakumbuke.
(KORASI)
Baba, ikumbuke,
Imani yao.
Uwategemeze;
Wasonge mbele.
2. Waadilifu wako
Wanapendeza,
Mbele zako Yehova.
Nasi twajua,
Zamani walikuwa,
Wenye bidii,
Walipotumikia,
Kwa nguvu zote.
(KORASI)
Baba, ikumbuke,
Imani yao.
Uwategemeze;
Wasonge mbele.
(Ona pia Mt. 25:21, 23; Zab. 71:9, 18; Met. 20:29; Luka 22:28; 1 Tim. 5:1.)