Wimbo Na. 88
Watoto—Amana Kutoka kwa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Baba apatapo mwana
Na mama anapopata mwana,
Amana kubwa wamepata,
Si yao tu, peke yao.
Zawadi toka kwa Yehova.
Yeye ndiye chanzo cha uhai.
Anawaagiza wazazi,
Wapate kuwa na hekima.
(KORASI)
Mumepata amana kubwa,
Ni urithi toka Kwake.
Basi ninyi, wafundisheni,
Maagizo ya Yehova.
2. Amuri zote za Mungu—
Ziwe katika mioyo yenu.
Wafunzeni wana na binti;
Hiyo ndiyo kazi yenu.
Wafundishe barabarani,
Mulalapo na muamukapo.
Wazikumbuke sikuzote,
Uaminifu wadumishe.
(KORASI)
Mumepata amana kubwa,
Ni urithi toka Kwake.
Basi ninyi, wafundisheni,
Maagizo ya Yehova.
(Ona pia Kum. 6:6, 7; Efe. 6:4; 1 Tim. 4:16.)