Wimbo Na. 133
Mtafute Mungu Upate Ukombozi
Makala Iliyochapishwa
1. Mataifa yote,
Yanamupinga Kristo.
Muda wao umekwisha.
Mungu ameagiza.
Siku zao kwisha;
Ufalme utadumu.
Kristo ataponda adui.
Hatakawia kamwe.
(KORASI)
Mutafuteni Yehova,
Mutegemeeni Yeye.
Utafuteni,
Uadilifu.
Tegemeza enzi yake.
Mungu atakukomboa,
Kwa nguvu zake.
2. Twapa wote fursa,
Ya kusikia Neno.
Waamue wapendavyo,
Uchaguzi ni wao.
Licha ya magumu,
Hatuogopi kamwe.
Mungu husikia maombi,
Ya watumishi wake.
(KORASI)
Mutafuteni Yehova,
Mutegemeeni Yeye.
Utafuteni,
Uadilifu.
Tegemeza enzi yake.
Mungu atakukomboa,
Kwa nguvu zake.
(Ona pia 1 Sam. 2:9; Zab. 2:2, 3, 9; Met. 2:8; Mt. 6:33.)