Wimbo Na. 93
“Acheni Nuru Yenu Iangaze”
Makala Iliyochapishwa
1. Yesu aamuru, Twangaze nuru.
Bila ubaguzi, Wote waone.
Neno lake Mungu, Liwape nuru.
Kwa neno na matendo, Twangaze nuru.
2. Twawatangazia Habari njema.
Waombolezao, Twawafariji.
Nayo Maandiko, Yatuongoza.
Tuseme kwa fadhili, Tuhubiripo.
3. Tufanyapo mema, Nuru yang’aa.
Fundisho la Bwana, Tunalipamba.
Tunamupendeza, Yehova Mungu.
Tuangaze daima, Nuru ya kweli.
(Ona pia Zab. 119:130; Mt. 5:14, 15, 45; Kol. 4:6.)