Wimbo Na. 112
Mungu Mkuu, Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Mungu mukuu, unastahili,
Kusifiwa zaidi,
U Mungu mwenye haki.
Ufalme wako, ni wa upendo;
U Mungu wa milele.
2. Unasamehe, Unarehemu,
Walio kama wewe.
Walio na rehema.
Fadhili zako, Unaonyesha,
Kwa yote ufanyayo.
3. Viumbe vyote, na vikusifu;
Jina na litakaswe,
Masuto lisipate.
Ufalme uje, ututawale,
Ulimwenguni pote.
(Ona pia Kum. 32:4; Met. 16:12; Mt. 6:10; Ufu. 4:11.)