Tunza
Nina Maoni Gani Kuhusu Visehemu vya Damu na Matibabu Yanayohusisha Damu Yangu Mwenyewe?
Biblia inawaamuru Wakristo “wajiepushe na . . . damu.” (Mdo. 15:20) Hivyo Mashahidi wa Yehova hawakubali kutiwa damu nzima mishipani au sehemu zake nne kuu, yaani, chembe nyekundu za damu (red blood cells), chembe nyeupe za damu (white blood cells), chembelele (platelets), na utegili (plasma). Vilevile hawatoi damu yao ili itumiwe na watu wengine wala hawaihifadhi ili irudishwe mwilini mwao baadaye. —Law. 17:13, 14; Mdo. 15:28, 29.
Visehemu vya damu ni nini, na kwa nini kila Mkristo anapaswa kujiamulia ikiwa atavitumia?
Visehemu vya damu ni vitu vinavyotolewa kwenye damu inapogawanywa. Kwa mfano, utegili (plasma), ambayo ni mojawapo ya sehemu nne kuu za damu, inaweza kugawanywa katika visehemu vifuatavyo: maji, asilimia 91 hivi; protini, kama vile uteute (albumins), globulini, na fibrinojeni, asilimia 7 hivi; na vitu vingine, kama vile virutubishi, homoni, gesi, vitamini, takataka, na elektroliti, hufanyiza asilimia 1.5.
Je, visehemu vya damu vinatiwa ndani katika amri ya Mungu ya kujiepusha na damu? Hatuwezi kutoa jibu hususa. Biblia haitoi maagizo hususa kuhusu visehemu vya damu.a Bila shaka, visehemu vingi vimetolewa kwenye damu ambayo imetolewa kwa matumizi ya kitiba. Kila Mkristo anapaswa kujifanyia uamuzi wake mwenyewe unaotegemea dhamiri yake ikiwa atakubali au atakataa matibabu yanayohusisha visehemu hivyo.
Unapofanya maamuzi kama hayo, fikiria maswali yafuatayo: Je ninaelewa kwamba kukataa visehemu vyote vya damu kunamaanisha kuwa sitakubali dawa fulani kama zile zinazosaidia kupigana na virusi na magonjwa, ama zile zinazosaidia damu kuganda ili kuzuia damu isivuje? Je, ninaweza kumweleza daktari kwa nini ninakataa au kukubali kutumia visehemu fulani vya damu?
Kwa nini uamuzi wa kutumia mbinu fulani za kitiba zinazohusisha matumizi ya damu yangu ni wa kibinafsi?
Ingawa Wakristo hawatoi au kuhifadhi damu yao kwa ajili ya kutiwa mishipani, baadhi ya mbinu au majaribio yanayohusisha damu ya mtu mwenyewe hayapingani na kanuni za Biblia. Kwa hiyo, kila mmoja anapaswa kufanya uamuzi wake mwenyewe ikiwa atakubali au kukataa mbinu fulani za kitiba ambazo zinahusisha damu yake.
Unapofanya maamuzi kama hayo, jiulize maswali yafuatayo: Ikiwa kiasi fulani cha damu yangu kitaelekezwa nje ya mwili na huenda mzunguko wa damu ukatizwe kwa muda fulani, je, dhamiri yangu itaniruhusu kuona damu hiyo kuwa sehemu ya mwili wangu bado, bila kuwa na uhitaji wa ‘kuimwaga kwenye udongo’? (Kum. 12:23, 24) Je, dhamiri yangu iliyozoezwa na Biblia ingenisumbua ikiwa wakati wa matibabu kiasi fulani cha damu yangu kingetolewa, kuboreshwa, na kurudishwa tena mwilini? Je, ninatambua kwamba kukataa matibabu yote yanayohusisha damu yangu kunamaanisha kwamba ninakataa matibabu kama utenganishaji wa koloidi (dialysis), au mashine ya kusaidia moyo au mapafu kufanya kazi (heart-lung machine)? Kabla ya kufanya uamuzi, je, nimesali kuhusu jambo hilo?b
Nimefanya maamuzi gani?
Chunguza daftari mbili zilizo kwenye kurasa zifuatazo. Daftari ya 1 inaorodhesha visehemu fulani vinavyotolewa kwenye damu na jinsi vinavyotumiwa kwa ukawaida katika matibabu. Andika ikiwa utakubali au utakataa kutumia kila moja ya visehemu hivyo. Daftari ya 2 inaorodhesha mbinu za kawaida za matibabu zinazohusisha damu yako. Andika kama utakubali au kukataa mbinu hizo. Madaftari hayo si hati za kisheria, bali zitakusaidia kujaza kadi ya DPA (mamlaka ya kudumu ya uwakilishi).
Unapaswa kujifanyia uamuzi na hupaswi kutegemea dhamiri ya mtu mwingine. Hakuna yeyote anayepaswa kuchambua maamuzi ya Mkristo mwenzake. Kuhusiana na mambo haya, “kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe.”—Gal. 6:4, 5.
[Maelezo ya Chini]
a Habari zaidi kuhusu jambo hili zinapatikana katika Mnara wa Mlinzi la Juni 15, 2004, ukurasa wa 29-31.
b Habari zaidi kuhusu jambo hilo zinapatikana katika Mnara wa Mlinzi la Oktoba 15, 2000, ukurasa wa 30-31, au katika DVD yenye kichwa Transfusion Alternatives—Documentary Series.
[Chati katika ukurasa wa 5]
Daftari ya 1
HAIFAI KWA UAMUZI WAKO
WAKRISTO
DAMU Uamuzi Unaopaswa
NZIMA VISEHEMU Kufanya
UTEGILI (PLASMA) UTEUTE (ALBUMIN)—KUFIKIA
ASILIMIA 4 YA UTEGILI
Protini inayotolewa katika
utegili. Aina mbalimbali
za uteute hupatikana pia
kati kamimea, katika
chakula kama vile maziwa
na mayai, na katika
maziwa ya mama ․․ Nakubali uteute
anayenyonyesha. Nyakati au
nyingine, uteute ․․ Nakataa uteute
unaotolewa katika damu
hutumiwa katika umajimaji
unaoongeza kiasi cha damu
ili kutibu mshtuko na majeraha
mabaya yanayotokana na kuungua.
Umajimaji huo unaweza kuwa na
asilimia 25 hivi ya uteute.
Kiasi kidogo sana cha uteute
hutumiwa kutengeneza dawa nyingine,
kutia ndani aina fulani ya dawa
zinazotumiwa kuchochea kutokezwa
kwa chembe nyekundu zinazoitwa
erythropoietin (EPO).
GLOBULIKINGA AU FINGO (IMMUNOGLOBULINS)
—KUFIKIA ASILIMIA 3 YA UTEGILI
Visehemu vya protini vinavyoweza
kutumiwa kwenye dawa fulani
ambazo hupigana na virusi na ․․ Nakubali
magonjwa, kama vile, globulikinga
dondakoo, pepopunda, uvimbe au
wa ini, na kichaa cha mbwa. ․․ Nakataa
Vinaweza pia kutumiwa kulinda globulikinga
dhidi ya magonjwa fulani
yanayohatarisha uhai wa kitoto
tumboni na kupunguza
madhara ya sumu ya nyoka au buibui.
VIGANDISHA-DAMU—CHINI YA ASILIMIA
1 YA UTEUTE
Kuna aina mbalimbali
za protini zinazosaidia
kugandisha damu ili
kuzuia isivuje.
Hupewa wagonjwa
ambao huvuja damu
kwa urahisi. ․․ Nakubali
Pia hutumiwa katika vigandisha-damu
gundi ya kitiba vinavyotokana na damu
kitiba kuziba majeraha au
na kuzuia kuvuja ․․ Nakataa
kwa damu baada ya vigandisha-damu
upasuaji. Moja vinavyotokana na damu
kati ya dawa
zinazotumiwa
kugandisha damu inaitwa
cryoprecipitate. Taarifa:
Sasa kuna dawa fulani
zinazotumiwa kugandisha damu
zinazotengenezwa kutokana na vyanzo
visivyohusisha damu.
CHEMBE NYEKUNDU HIMOGLOBINI—ASILIMIA 33
YA CHEMBE NYEKUNDU
Protini inayosafirisha
oksijeni mwilini
na inayosafirisha ․․ Nakubali himoglobini
kaboni-dioksidi au
kwenye ․․ Nakataa himoglobini
mapafu. Dawa
ambazo zimetengenezwa
kutokana na himoglobini
ya binadamu au mnyama
zinaweza kutumiwa
kumtibu mtu mwenye
upungufu wa damu au
aliyepoteza damu nyingi.
HEMINI (HEMIN)—CHINI YA
ASILIMIA 2 YA CHEMBE NYEKUNDU
Kimeng’enya kinachotokana
na himoglobini ambacho
kinatumiwa kutibu
magonjwa ya damu ․․ Nakubali hemini
yanayorithiwa ambayo au
si ya kawaida ․․ Nakataa hemini
(yanajulikana kama
porphyria) yanayoathiri
mfumo wa kumeng’enya
chakula, wa neva,
na mifumo ya damu.
CHEMBE NYEUPE INTERFERON—SEHEMU NDOGO
YA CHEMBE NYEUPE
Protini inayotumiwa ․․ Nakubali Interferon
kutibu magonjwa zinazotokana na damu
yanayosababishwa na au
virusi na kansa. ․․ Nakataa Interferon
Interferon nyingi zinazotokana na damu
hazitokani na damu.
Nyingine zinatokana
na visehemu vya chembe
nyeupe za damu ya wanadamu.
CHEMBELELE Wakati huu hakuna visehemu
(PLATELETS) vya chembelele (platelets)
ambazo zimetolewa kwa ajili
ya matibabu.
[Chati katika ukurasa wa 6]
DAFTARI YA 2
UAMUZI WAKO
MATIBABU YANAYOHUSISHA DAMU YAKO MWENYEWE
*Taarifa: Kila daktari ana njia yake ya kutumia mbinu hizi za matibabu. Mwombe daktari akueleze mambo yanayohusika katika matibabu aliyopendekeza ili uhakikishe yanapatana na kanuni za Biblia na dhamiri yako.
AINA YA YANATIBU NINI Uamuzi Unaopaswa
MATIBABU Kufanya
(Huenda ukapenda
kuzungumza na
daktari kabla ya
kukubali au kukataa
yoyote kati ya
matibabu haya.)
UOKOAJI WA Hupunguza kupotea kwa
CHEMBE ZA DAMU damu. Wakati wa upasuaji,
damu inayotoka kwenye ․․ Nakubali
kidonda au tundu ․․ Huenda nikakubali*
hukusanywa. Inasafishwa ․․ Nakataa
au kuchujwa kisha, labda
bila kukatiza mtiririko,
inarudishwa kwa mgonjwa
UZIMUAJI WA Hupunguza kupotea kwa damu.
DAMU Wakati wa upasuaji, damu
(Hemodilution) inaelekezwa katika
mifuko na kubadilishwa
na umajimaji usiotokana
na damu unaopanua kiasi
cha damu. Damu inayosalia ․․ Nakubali
wakati wa upasuaji ․․ Huenda nikakubali*
huongezwa umajimaji ․․ Nakataa
mwingine na hivyo kuwa
na chembe chache nyekundu
za damu. Wakati au baada
ya upasuaji, damu iliyokuwa
imeelekezwa kando hurudishwa
kwa mgonjwa.
MASHINE YA Hudumisha mzunguko.
KUSAIDIA MOYO Damu huelekezwa kwenye
MAPAFU KUFANYA mashine ya kusaidia ․․ Nakubali
KAZI (Heart- moyo au mapafu kufanya ․․ Huenda nikakubali*
Lung Machine) kazi ambako inatiwa ․․ Nakataa
oksijeni na kurudishwa
tena kwa mgonjwa.
UTENGANISHAJI Hufanya kazi kama kiungo.
WA KOLOIDI Damu huzunguka katika
(Dialysis) mashine hii ambayo ․․ Nakubali
huichuja na kuisafisha ․․ Huenda nikakubali*
kabla ya kuirudisha ․․ Nakataa
ndani ya mwili wa mgonjwa.
KUDUNGWA Huzuia kuvuja kwa umajimaji
SINDANO YA ulio kwenye uti wa mgongo.
DAMU KWENYE Mgonjwa hudungwa sindano
UTI WA MGONGO iliyo na kiasi kidogo
(Epidural cha damu yake mwenyewe ․․ Nakubali
Blood Patch) katika utando ․․ Huenda nikakubali*
unaozunguka uti wa ․․ Nakataa
mgongo. Hutumiwa kuziba
tundu linalotoa umajimaji
ulio kwenye uti wa mgongo.
PLASMAPHERESIS Hutibu ugonjwa. Damu hutolewa
ndani ya mwili wa mgonjwa
na kuondolewa utegili
(plasma). Kibadala
cha utegili huongezwa, ․․ Nakubali
na damu hiyo hurudishwa ․․ Huenda nikakubali*
kwa mgonjwa. Huenda ․․ Nakataa
baadhi ya madaktari
wakataka kutumia utegili
kutoka katika damu ya
mtu mwingine badala
ya ule wa mgonjwa.
Ikiwa ndivyo, Mkristo
hapaswi kukubali
matibabu haya.
KUWEKA ALAMA Hutambua au kutibu ugonjwa.
(Labeling or Sehemu ya damu hutolewa,
Tagging) inachanganywa na dawa, ․․ Nakubali
kurudishwa kwa mgonjwa. ․․ Huenda nikakubali*
Muda ambao damu huwa ․․ Nakataa
nje ya mwili wa mgonjwa
unatofautiana.
JELI YA Inaziba majeraha,
CHEMBELELE inapunguza kuvuja kwa
(Platelet Gel) damu. Kiasi fulani cha
(HUTOLEWA damu hutolewa na
KATIKA DAMU kushinikizwa katika
YA MGONJWA mchanganyiko uliojaa
MWENYEWE) utegili na chembe ․․ Nakubali
nyeupe za damu. ․․ Huenda nikakubali*
Mchanganyiko huu ․․ Nakataa
hupakwa kwenye sehemu
zilizopasuliwa au
kwenye majeraha.
Taarifa: Katika
michanganyiko fulani,
kigandisha-damu kilichotolewa
kwenye damu ya ng’ombe hutumiwa.