Wimbo Na. 110
Kazi za Mungu za Ajabu
Makala Iliyochapishwa
1. Mungu, wanijua vizuri,
Nilalapo na niamukapo.
Na fikira zangu umechunguza,
Maneno na matendo
yangu wajua.
Sirini nilipofanyizwa,
Uliiona mifupa yangu.
Yote yalikuwa yameandikwa.
Unastahili sifa
na utukufu.
Ee, Yehova, una hekima nyingi;
Nafsi yangu inajua vema.
Hata katika giza la usiku,
Roho yako ingeniongoza.
Yehova nijifiche wapi,
Kutoka mbele za uso wako?
Si milimani wala Kaburini,
Gizani wala baharini, siwezi.
(Ona pia Zab. 66:3; 94:19; Yer. 17:10.)