Wimbo Na. 38
Mtupie Yehova Mzigo Wako
Makala Iliyochapishwa
1. Ee Yehova nakuomba,
Usijifiche mbali.
Sikiliza, unijibu,
Ili nisisumbuke.
(KORASI)
Mutupie Yah muzigo;
Atakutegemeza wewe.
Hataacha utikiswe,
Atakuimarisha.
2. Kama ningekuwa njiwa,
Ningeruka nyikani,
Mbali na watu waovu,
Watendao jeuri.
(KORASI)
Mutupie Yah muzigo;
Atakutegemeza wewe.
Hataacha utikiswe,
Atakuimarisha.
3. Nitamulilia Mungu,
Nitamwomba ulinzi.
Tujapopingwa na watu,
Anatutia nguvu.
(KORASI)
Mutupie Yah muzigo;
Atakutegemeza wewe.
Hataacha utikiswe,
Atakuimarisha.
(Ona pia Zab. 22:5; 31:1-24.)