Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb14 uku. 169
  • Ninaipenda Sana Nchi ya Sierra Leone

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ninaipenda Sana Nchi ya Sierra Leone
  • 2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Habari Zinazolingana
  • Kazi ya Kufanya Wanafunzi Imefinyanga Maisha Yangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Nimeazimia Kumtumikia Yehova
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Kitu Bora Zaidi Kuliko Almasi
    2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
  • Nilipata Usalama wa Kweli kwa Kumtumaini Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
Pata Habari Zaidi
2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
yb14 uku. 169

SIERRA LEONE NA GUINEA

Ninaipenda Sana Nchi ya Sierra Leone

Cindy McIntire

  • ALIZALIWA 1960

  • ALIBATIZWA 1974

  • MAELEZO MAFUPI KUMHUSU  Mmishonari tangu 1992. Alitumikia nchini Guinea na Senegal, na sasa anatumikia Sierra Leone.

Picha katika ukurasa wa 169

NILIPOFIKA kwa mara ya kwanza katika nchi ya Sierra Leone, ilinichukua wiki mbili tu kuipenda. Nilishangazwa na jinsi watu walivyobeba mizigo mizito kichwani kwa njia rahisi sana. Majirani walikuwa na shughuli nyingi. Katika mitaa, watoto walifurahia michezo mbalimbali. Nilizungukwa na watu wachangamfu, waliopenda muziki, na mavazi yenye rangi mbalimbali.

Jambo linalonifurahisha zaidi ni kuhubiri. Wasierra Leone ni watu wakarimu kwelikweli. Wanaiheshimu Biblia na kusikiliza ujumbe wake. Mara nyingi, wao hunikaribisha katika nyumba zao. Ninapoondoka, wengine hunisindikiza hadi barabarani. Sifa hizo nzuri zinanisaidia kukabiliana na mambo mengine madogo-madogo, kama vile uhaba wa maji na kukatika-katika kwa umeme.

Kwa kuwa ningali mseja, wakati mwingine watu huniuliza ikiwa mimi huhisi upweke. Kwa kweli, nina mambo mengi ya kufanya hivi kwamba sihisi nikiwa mpweke. Maisha yangu yana kusudi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki