Wimbo Na. 89
Mwaliko Wenye Upendo wa Yehova: “Uwe na Hekima, Mwanangu”
Makala Iliyochapishwa
1. Binti na mwanangu,
nipe moyo wako.
Apate kuona yule
mudhihaki.
Nawe unitumikie
kwa kupenda;
Na ulimwengu uone
wanipenda.
(KORASI)
Binti yangu, nawe mwanangu,
Furahisha moyo wangu.
Nitumikie kwa hiari,
Ulisifu jina langu.
2. Nitumikie kwa
shangwe na furaha.
Ujapoanguka,
Nitakuinua.
Hata ukivunjwa moyo
na yeyote,
Kumbuka ninakupenda
sikuzote.
(KORASI)
Binti yangu, nawe mwanangu,
Furahisha moyo wangu.
Nitumikie kwa hiari,
Ulisifu jina langu.
(Ona pia Kum. 6:5; Mhu. 11:9; Isa. 41:13.)