Wimbo Na. 59
Tumejiweka Wakfu kwa Mungu!
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova ametuvuta kwake Kristo
Tupate kuwa wanafunzi.
Toka juu mbinguni,
Nuru Yake yang’aa.
Tumekuza imani;
Tunajikana wenyewe.
(KORASI)
Twajiweka wakfu kwake; kwa kupenda.
Mbele zake tunashangilia.
2. Twasimama mbele zake Mungu wetu.
Tumutumikie milele.
Ni shangwe kubwa sana,
Kumutangaza kote,
Jina lake kubeba,
Na Ufalme kutangaza.
(KORASI)
Twajiweka wakfu kwake; kwa kupenda.
Mbele zake tunashangilia.
(Ona pia Zab. 43:3; 107:22; Yoh. 6:44.)