Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • td kur. 1-44
  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1. Biblia
  • 2. Damu
  • 3. Dhambi
  • 4. Dini
  • 5. Dunia
  • 6. Fidia
  • 7. Har-magedoni
  • 8. Ibada ya Maria
  • 9. Ibilisi, Roho Waovu
  • 10. Kaburi (Hell, Hadesi, Sheoli)
  • 11. Kanisa
  • 12. Kifo
  • 13. Kuabudu Mababu wa Kale
  • 14. Kuandikiwa Kimbele Yatakayompata Mtu
  • 15. Kuchanganya Imani Mbalimbali
  • 16. Kuponya, Lugha
  • 17. Kurudi kwa Kristo
  • 18. Kutoa Ushahidi
  • 19. Manabii wa Uwongo
  • 20. Mashahidi wa Yehova
  • 21. Mbingu
  • 22. Mhudumu
  • 23. Mifano, Sanamu
  • 24. Msalaba
  • 25. Nafsi
  • 26. Ndoa
  • 27. Roho, Kuwasiliana na Pepo
  • 28. Sabato
  • 29. Sala
  • 30. Siku za Mwisho
  • 31. Sikukuu, Sikukuu za Kuzaliwa
  • 32. Tarehe za Matukio (Kronolojia)
  • 33. Ubatizo
  • 34. Ufalme
  • 35. Ufufuo
  • 36. Ukumbusho, Misa
  • 37. Uovu, Taabu za Ulimwengu
  • 38. Upinzani, Mateso
  • 39. Utatu
  • 40. Uumbaji
  • 41. Uzima
  • 42. Wokovu
  • 43. Yehova, Mungu
  • 44. Yesu
  • Yesu Kristo
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Mwalimu, Ufundishaji
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Sala
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Uhai
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
Pata Habari Zaidi
Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
td kur. 1-44

Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

(Kutoka Tafsiri ya Ulimwengu Mpya)

1. Biblia

A. Neno la Mungu limeongozwa na roho

Wanadamu walichochewa na roho ya Mungu kuandika. 2Pe 1:20, 21

Ina unabii: Da 8:5, 6, 20-22; Lu 21:5, 6, 20-22; Isa 45:1-4

Biblia nzima imeongozwa na roho ya Mungu na ina faida. 2Ti 3:16, 17; Ro 15:4

B. Ni mwongozo wenye kutumika kwa siku zetu

Kupuuza kanuni za Biblia kunaleta kifo. Ro 1:28-32

Hekima ya binadamu haichukui nafasi ya Biblia. 1Ko 1:21, 25; 1Ti 6:20

Inatulinda na adui aliye na nguvu zaidi. Efe 6:11, 12, 17

Humwongoza mwanadamu katika njia inayofaa. Zb 119:105; 2Pe 1:19; Met 3:5, 6

C. Iliandikwa kwa ajili ya watu wa mataifa na jamii zote

Uandikaji wa Biblia ulianzia Mashariki. Kut 17:14; 24:12, 16; 34:27

Uandalizi wa Mungu si kwa Wazungu tu. Ro 10:11-13; Ga 3:28

Mungu hukubali watu wa namna zote. Mdo 10:34, 35; Ro 5:18; Ufu 7:9, 10

2. Damu

A. Kutia damu mishipani huvunja utakatifu wa damu

Noa aliambiwa damu ni takatifu, ndiyo uhai. Mwa 9:4, 16

Agano la Sheria lilikataza kula damu. Law 17:14; 7:26, 27

Katazo hilo lilirudiwa kwa Wakristo. Mdo 15:28, 29; 21:25

B. Suala la kuokoa uhai halifanyi iwe sawa kuvunja sheria ya Mungu

Utii ni bora kuliko dhabihu. 1Sa 15:22; Mk 12:33

Kutanguliza uhai wa mtu mwenyewe badala ya sheria ya Mungu kunaleta kifo. Mk 8:35, 36

3. Dhambi

A. Maana ya dhambi

Kuvunja sheria ya Mungu, kiwango chake kikamilifu. 1Yo 3:4; 5:17

Mwanadamu, akiwa uumbaji wa Mungu, atatoa hesabu kwake. Ro 14:12; 2:12-15

Sheria ilifafanua dhambi, ilifanya wanadamu waitambue. Ga 3:19; Ro 3:20

Wote wana dhambi, wamepungukiwa na kiwango kikamilifu cha Mungu. Ro 3:23; Zb 51:5

B. Sababu ya wote kupatwa na dhambi ya Adamu

Adamu alipitisha kutokamilika na kifo kwa wote. Ro 5:12, 18

Mungu alikuwa mwenye rehema katika kuwavumilia wanadamu. Zb 103:8, 10, 14, 17

Dhabihu ya Yesu hufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi. 1Yo 2:2

Dhambi na kazi nyingine zote za Ibilisi zitafutwa. 1Yo 3:8

C. Tunda lililokatazwa lilikuwa kutokutii, si tendo la ngono

Katazo la mti lilitolewa kabla ya kuumbwa kwa Hawa. Mwa 2:17, 18

Adamu na Hawa waliambiwa wazae watoto. Mwa 1:28

Watoto si tokeo la dhambi, bali ni baraka ya Mungu. Zb 127:3-5

Hawa alitenda dhambi wakati mume hakuwapo; alijitanguliza. Mwa 3:6; 1Ti 2:11-14

Adamu, akiwa kichwa, aliiasi sheria ya Mungu. Ro 5:12, 19

D. Maana ya kuitendea dhambi roho takatifu (Mt 12:32; Mk 3:28, 29)

Dhambi ya kurithi si ya aina hiyo. Ro 5:8, 12, 18; 1Yo 5:17

Huenda mtu akaihuzunisha roho, lakini apate nafuu. Efe 4:30; Yak 5:19, 20

Kuzoea kufanya dhambi kwa kukusudia huongoza kwenye kifo. 1Yo 3:6-9

Mungu huwahukumu wanaofanya hivyo, huondoa roho yake. Ebr 6:4-8

Hatupaswi kusali kwa ajili ya hao wasiotubu. 1Yo 5:16, 17

4. Dini

A. Kuna dini moja tu ya kweli

Tumaini moja, imani moja, ubatizo mmoja. Efe 4:5, 13

Imepewa utume wa kufanya wanafunzi. Mt 28:19; Mdo 8:12; 14:21

Inatambuliwa kwa matunda yake. Mt 7:19, 20; Lu 6:43, 44; Yoh 15:8

Upendo, mapatano kati ya washiriki. Yoh 13:35; 1Ko 1:10; 1Yo 4:20

B. Inafaa kushutumu mafundisho ya uwongo

Yesu alishutumu mafundisho ya uwongo. Mt 23:15, 23, 24; 15:4-9

Alifanya hivyo ili kuwalinda waliopofushwa. Mt 15:14

Kweli iliwaweka huru wawe wanafunzi wa Yesu. Yoh 8:31, 32

C. Ni muhimu mtu kubadili dini ikithibitishwa kuwa ni ya uwongo

Kweli huweka mtu huru; huthibitisha kuwa wengi wamekosea. Yoh 8:31, 32

Waisraeli, wengine, waliacha ibada ya kwanza. Yos 24:15; 2Fa 5:17

Wakristo wa kwanza walibadili maoni. Ga 1:13, 14; Mdo 3:17, 19

Paulo alibadili dini yake. Mdo 26:4-6

Ulimwengu mzima umedanganywa, lazima mtu afanye upya akili yake. Ufu 12:9; Ro 12:2

D. Unaoonekana kuwa “wema katika dini zote” hautoi uhakikisho wa kibali cha Mungu

Mungu huweka kiwango cha ibada. Yoh 4:23, 24; Yak 1:27

Huo si wema kama haulingani na mapenzi ya Mungu. Ro 10:2, 3

“Matendo mema” yaweza kukataliwa. Mt 7:21-23

Hutambuliwa kwa matunda. Mt 7:20

5. Dunia

A. Kusudi la Mungu kuelekea dunia

Paradiso ilifanywa duniani kwa ajili ya wanadamu wakamilifu. Mwa 1:28; 2:8-15

Kusudi la Mungu ni hakika. Isa 55:11; 46:10, 11

Dunia itajazwa wanadamu wenye amani, wakamilifu. Zb 72:7; Isa 45:18; 9:6,7

Ufalme utairudisha Paradiso. Mt 6:9, 10; Ufu 21:3-5

B. Haitaharibiwa kamwe wala kuondolewa wakaaji

Dunia halisi itadumu milele. Mhu 1:4; Zb 104:5

Wanadamu wa wakati wa Noa waliharibiwa, si dunia. 2Pe 3:5-7; Mwa 7:23

Mfano huo watoa tumaini la kuokoka wakati wetu. Mt 24:37-39

Waovu wataharibiwa; “umati mkubwa” utaokoka. 2Th 1:6-9; Ufu 7:9, 14

6. Fidia

A. Uhai wa kibinadamu wa Yesu ulilipwa kuwa “fidia kwa ajili ya wote”

Yesu alitoa uhai wake kuwa fidia. Mt 20:28

Thamani ya damu iliyomwagwa huandaa msamaha wa dhambi. Ebr 9:14, 22

Dhabihu moja ilitosha kwa wakati wote. Ro 6:10; Ebr 9:26

Faida hazijileti tu; lazima zitambuliwe. Yoh 3:16

B. Ilikuwa bei inayolingana

Adamu aliumbwa mkamilifu. Kum 32:4; Mhu 7:29; Mwa 1:31

Kwa kutenda dhambi alijipotezea ukamilifu yeye na watoto wake. Ro 5:12, 18

Watoto hawakuweza kujisaidia; mtu aliye sawa kabisa na Adamu alihitajiwa. Zb 49:7; Kum 19:21

Uhai mkamilifu wa kibinadamu wa Yesu ni fidia. 1Ti 2:5, 6; 1Pe 1:18, 19

7. Har-magedoni

A. Vita vya Mungu vya kukomesha uovu

Mataifa yakusanywa kwenye Har-magedoni. Ufu 16:14, 16

Mungu apigana, kwa kutumia Mwana na malaika. 2Th 1:6-9; Ufu 19:11-16

Jinsi tunavyoweza kuokoka. Sef 2:2, 3; Ufu 7:14

B. Inapatana na upendo wa Mungu

Ulimwengu umeharibika sana. 2Ti 3:1-5

Mungu ana subira, lakini haki inataka hatua ichukuliwe. 2Pe 3:9, 15; Lu 18:7, 8

Lazima waovu waondoke ili waadilifu wasitawi. Met 21:18; Ufu 11:18

8. Ibada ya Maria

A. Maria ni mama ya Yesu, si “mama ya Mungu”

Mungu hana mwanzo. Zb 90:2; 1Ti 1:17

Maria alikuwa mama ya Mwana wa Mungu, katika hali yake ya kidunia. Lu 1:35

B. Maria hakuwa “bikira sikuzote”

Aliolewa na Yosefu. Mt 1:19, 20, 24, 25

Alikuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu. Mt 13:55, 56; Lu 8:19-21

Hao wakati huo hawakuwa “ndugu zake wa kiroho.” Yoh 7:3, 5

9. Ibilisi, Roho Waovu

A. Ibilisi ni mtu wa roho

Si uovu ulio ndani ya mtu mwenyewe bali ni mtu wa roho. 2Ti 2:26

Ibilisi ni mtu jinsi malaika walivyo. Mt 4:1, 11; Ayu 1:6

Alijifanya Ibilisi kwa kuwa na tamaa mbaya. Yak 1:13-15

B. Ibilisi ndiye mtawala asiyeonekana wa ulimwengu

Ulimwengu uko chini ya utawala wake akiwa mungu wake. 2Ko 4:4; 1Yo 5:19; Ufu 12:9

Ameruhusiwa kubaki mpaka suala litatuliwe. Kut 9:16; Yoh 12:31

Atatiwa katika abiso, kisha aharibiwe. Ufu 20:2, 3, 10

C. Roho waovu ni malaika waasi

Walijiunga na Shetani kabla ya Gharika. Mwa 6:1, 2; 1Pe 3:19, 20

Walishushwa, wakatengwa na nuru yote. 2Pe 2:4; Yuda 6

Hupigana na Mungu, huwaonea wanadamu. Lu 8:27-29; Ufu 16:13, 14

Wataharibiwa pamoja na Shetani. Mt 25:41; Lu 8:31; Ufu 20:2, 3, 10

10. Kaburi (Hell, Hadesi, Sheoli)

A. Si mahali halisi penye moto wa mateso

Ayubu mwenye kutaabika alisali aende huko. Ayu 14:13

Ni mahali pasipo na utendaji. Zb 6:5; Mhu 9:10; Isa 38:18, 19

Yesu alifufuliwa kutoka kaburini, Hadesi. Mdo 2:27, 31, 32; Zb 16:10

Kaburi litawatoa wengine waliokufa, litaharibiwa. Ufu 20:13, 14

B. Moto ni mfano wa kuangamizwa

Moto hufananisha kukatiliwa mbali katika kifo. Mt 25:41, 46; 13:30

Waovu wasiotubu waharibiwa milele kana kwamba kwa moto. Ebr 10:26, 27

“Mateso” ya Shetani motoni ni kifo cha milele. Ufu 20:10, 14, 15

C. Masimulizi ya tajiri na Lazaro si uthibitisho wa mateso ya milele

Moto si halisi kama vile kifua cha Abrahamu kisivyo halisi. Lu 16:22-24

Kibali cha Abrahamu kinatofautishwa pia na giza. Mt 8:11, 12

Kuangamizwa kwa Babiloni kunaitwa mateso ya moto. Ufu 18:8-10, 21

11. Kanisa

A. Kanisa ni la kiroho, limejengwa juu ya Kristo

Mungu hakai katika mahekalu yaliyotengenezwa na mwanadamu. Mdo 17:24, 25; 7:48

Kanisa la kweli ni hekalu la kiroho la mawe yaliyo hai. 1Pe 2:5, 6

Kristo ndiye jiwe la pembeni; mitume ni msingi wa pili. Efe 2:20

Mungu anapasa kuabudiwa kwa roho na kweli. Yoh 4:24

B. Kanisa halikujengwa juu ya Petro

Yesu hakusema kanisa limejengwa juu ya Petro. Mt 16:18

Yesu atambulishwa kuwa ndiye “mwamba.” 1Ko 10:4

Petro alimtambulisha Yesu kuwa msingi. 1Pe 2:4, 6-8; Mdo 4:8-12

12. Kifo

A. Sababu ya kifo

Mwanadamu alikuwa na mwanzo mkamilifu, tazamio la uzima usio na mwisho. Mwa 1:28, 31

Kutokutii kulileta hukumu ya kifo. Mwa 2:16, 17; 3:17, 19

Dhambi na kifo vilipitishwa kwa watoto wote wa Adamu. Ro 5:12

B. Hali ya wafu

Adamu alifanywa kuwa nafsi, hakupewa nafsi. Mwa 2:7; 1Ko 15:45

Ni mwanadamu, nafsi, ambaye hufa. Eze 18:4; Isa 53:12; Ayu 11:20

Wafu hawana fahamu, hawajui lolote. Mhu 9:5, 10; Zb 146:3, 4

Wafu wamelala wakingojea ufufuo. Yoh 11:11-14, 23-26; Mdo 7:60

C. Haiwezekani kuongea na wafu

Wafu hawako hai pamoja na Mungu wakiwa roho. Zb 115:17; Isa 38:18

Tunaonywa juu ya kujaribu kusema na wafu. Isa 8:19; Law 19:31

Wanaowasiliana na pepo, wapiga-ramli, hushutumiwa. Kum 18:10-12; Ga 5:19-21

13. Kuabudu Mababu wa Kale

A. Kuabudu mababu wa kale ni ubatili

Mababu wa kale wamekufa, hawana fahamu. Mhu 9:5, 10

Mababu wa kwanza hawastahili kuabudiwa. Ro 5:12, 14; 1Ti 2:14

Mungu anakataza ibada hiyo. Kut 34:14; Mt 4:10

B. Wanadamu wanaweza kuheshimiwa, lakini wa kuabudiwa ni Mungu tu

Vijana wanapaswa kuwaheshimu watu wenye umri mkubwa. 1Ti 5:1, 2, 17; Efe 6:1-3

Lakini ni Mungu tu anayepasa kuabudiwa. Mdo 10:25, 26; Ufu 22:8, 9

14. Kuandikiwa Kimbele Yatakayompata Mtu

A. Binadamu hakuandikiwa kimbele yatakayompata

Kusudi la Mungu ni hakika. Isa 55:11; Mwa 1:28

Watu mmoja-mmoja wamepewa uchaguzi wa kumtumikia Mungu. Yoh 3:16; Flp 2:12

15. Kuchanganya Imani Mbalimbali

A. Kujiunga na dini nyingine si njia ya Mungu

Ni njia moja tu, ni nyembamba, ni wachache huipata. Efe 4:4-6; Mt 7:13, 14

Tunaonywa kwamba mafundisho ya uwongo huchafua. Mt 16:6, 12; Ga 5:9

Tunaamriwa kujitenga. 2Ti 3:5; 2Ko 6:14-17; Ufu 18:4

B. Si kweli kusema kuna “wema katika dini zote”

Nyingine zina bidii lakini si kupatana na Mungu. Ro 10:2, 3

Ubaya huharibu mengine yote ambayo huenda yakawa mema. 1Ko 5:6; Mt 7:15-17

Walimu wa uwongo huleta uharibifu. 2Pe 2:1; Mt 12:30; 15:14

Ibada safi inataka mtu kujitoa kikamili. Kum 6:5, 14, 15

16. Kuponya, Lugha

A. Kuponya kiroho kuna faida zenye kudumu

Ugonjwa wa kiroho unaharibu. Isa 1:4-6; 6:10; Ho 4:6

Kuponya kiroho ndio utume wa msingi. Yoh 6:63; Lu 4:18

Huondoa dhambi; huleta furaha, uzima. Yak 5:19, 20; Ufu 7:14-17

B. Ufalme wa Mungu utaleta maponyo ya kimwili yenye kudumu

Yesu aliponya udhaifu mbalimbali, alihubiri baraka za Ufalme. Mt 4:23

Ufalme umeahidiwa kuwa njia ya kuleta maponyo yenye kudumu. Mt 6:10; Isa 9:7

Hata kifo kitafutiliwa mbali. 1Ko 15:25, 26; Ufu 21:4; 20:14

C. Uponyaji wa imani wa sasa hauna uthibitisho wa kibali cha Mungu

Wanafunzi hawakujiponya wenyewe kimuujiza. 2Ko 12:7-9; 1Ti 5:23

Zawadi za kimuujiza ziliisha baada ya siku za mitume. 1Ko 13:8-11

Kuponya si uthibitisho hakika wa kibali cha Mungu. Mt 7:22, 23; 2Th 2:9-11

D. Kusema kwa lugha kulikuwa kuwe kwa muda mfupi tu

Kulikuwa ishara; zawadi kubwa zaidi zilipasa kutafutwa. 1Ko 14:22; 12:30, 31

Zawadi za kimuujiza za roho zilitabiriwa kupitilia mbali. 1Ko 13:8-10

Matendo ya ajabu si uthibitisho hakika wa kibali cha Mungu. Mt 7:22, 23; 24:24

17. Kurudi kwa Kristo

A. Kurudi hakuonekani kwa wanadamu

Aliwaambia wanafunzi ulimwengu hautamwona tena. Yoh 14:19

Ni wanafunzi tu walioona akipanda mbinguni; kurudi ni vivyo hivyo. Mdo 1:6, 10, 11

Yuko mbinguni, ni roho asiyeonekana. 1Ti 6:14-16; Ebr 1:3

Anarudi katika nguvu za Ufalme wa mbinguni. Da 7:13, 14

B. Hutambuliwa kwa mambo yanayoonekana

Wanafunzi waliuliza ishara ya kuwapo. Mt 24:3

Wakristo “huona” kuwapo kwa njia ya uelewaji. Efe 1:18

Matukio mengi ya pamoja ni uthibitisho wa kuwapo. Lu 21:10, 11

Adui ‘huona’ uharibifu unapowafikia. Ufu 1:7

18. Kutoa Ushahidi

A. Lazima Wakristo wote watoe ushahidi, watangaze habari njema

Lazima wamkiri Yesu mbele ya watu ili wakubaliwe. Mt 10:32

Lazima kuwa mtendaji wa Neno, na kuonyesha imani. Yak 1:22-24; 2:24

Wapya, pia, wapaswa kuwa walimu. Mt 28:19, 20

Tangazo la hadharani huleta wokovu. Ro 10:10

B. Uhitaji wa ziara za tena na tena, kuendelea kutoa ushahidi

Lazima onyo juu ya mwisho litolewe. Mt 24:14

Yeremia alitangaza mwisho wa Yerusalemu kwa miaka mingi. Yer 25:3

Kama vile Wakristo wa kwanza, hatuwezi kuacha. Mdo 4:18-20; 5:28, 29

C. Lazima kutoa ushahidi ili tusiwe na hatia ya damu

Lazima kuonya juu ya mwisho unaokaribia. Eze 33:7; Mt 24:14

Kutofanya hivyo huleta hatia ya damu. Eze 33:8, 9; 3:18, 19

Paulo aliepuka hatia ya damu; alisema kweli kamili. Mdo 20:26, 27; 1Ko 9:16

Humwokoa anayetoa ushahidi na pia yule anayesikiliza. 1Ti 4:16; 1Ko 9:22

19. Manabii wa Uwongo

A. Manabii wa uwongo walitabiriwa; walikuwako siku za mitume

Kanuni ya kutambua manabii wa uwongo. Kum 18:20-22; Lu 6:26

Walitabiriwa; watambuliwa kwa matunda. Mt 24:23-26; 7:15-23

20. Mashahidi wa Yehova

A. Mwanzo wa Mashahidi wa Yehova

Yehova hutambulisha mashahidi wake mwenyewe. Isa 43:10-12; Yer 15:16

Mfuatano wa mashahidi waaminifu ulianza na Abeli. Ebr 11:4, 39; 12:1

Yesu alikuwa shahidi mwaminifu na wa kweli. Yoh 18:37; Ufu 1:5; 3:14

21. Mbingu

A. Ni 144,000 tu wanaoenda mbinguni

Hesabu yenye kikomo; watakuwa wafalme pamoja na Kristo. Ufu 5:9, 10; 20:4

Yesu alikuwa mtangulizi; wengine wamechaguliwa tangu wakati huo. Kol 1:18; 1Pe 2:21

Wengine wengi wataishi duniani. Zb 72:8; Ufu 21:3, 4

144,000 katika cheo cha pekee ambacho wengine hawana. Ufu 14:1, 3; 7:4, 9

22. Mhudumu

A. Wakristo wote lazima wawe wahudumu

Yesu alikuwa mhudumu wa Mungu. Ro 15:8, 9; Mt 20:28

Wakristo hufuata kielelezo chake. 1Pe 2:21; 1Ko 11:1

Lazima wahubiri ili kutimiza huduma. 2Ti 4:2, 5; 1Ko 9:16

B. Sifa za kustahili kwa ajili ya huduma

Roho ya Mungu na ujuzi wa Neno lake. 2Ti 2:15; Isa 61:1-3

Fuata kielelezo cha Kristo katika kuhubiri. 1Pe 2:21; 2Ti 4:2, 5

Mungu huzoeza kwa kutumia roho, tengenezo. Yoh 14:26; 2Ko 3:1-3

23. Mifano, Sanamu

A. Kutumia mifano, sanamu, katika ibada hushusha hadhi kwa Mungu

Haiwezekani kufanya sanamu ya Mungu. 1Yo 4:12; Isa 40:18; 46:5; Mdo 17:29

Wakristo wanaonywa juu ya sanamu. 1Ko 10:14; 1Yo 5:21

Mungu ni lazima aabudiwe kwa roho, kweli. Yoh 4:24

B. Ibada ya sanamu ilileta kifo kwa taifa la Israeli

Wayahudi walikatazwa kuabudu sanamu. Kut 20:4, 5

Haziwezi kusikia, kusema; wanaozitengeneza watakuwa kama hizo. Zb 115:4-8

Zilileta mtego, uharibifu. Zb 106:36, 40-42; Yer 22:8, 9

C. Ibada ya “kadiri” hairuhusiwi

Mungu alikataa kuruhusu ibada yake iwe ya “kadiri.” Isa 42:8

Mungu peke yake ndiye “Msikiaji wa sala.” Zb 65:1, 2

24. Msalaba

A. Yesu alitundikwa juu ya mti wa kuulia iwe shutuma

Yesu alitundikwa juu ya mti au nguzo ya kuulia. Mdo 5:30; 10:39; Ga 3:13

Wakristo ni lazima wauchukue mti kuwa shutuma. Mt 10:38; Lu 9:23

B. Haupasi kuabudiwa

Kuonyesha mti wa Yesu ni shutuma. Ebr 6:6; Mt 27:41, 42

Kutumia msalaba katika ibada ni kuabudu sanamu. Kut 20:4, 5; Yer 10:3-5

Yesu ni roho, hayupo tena juu ya mti. 1Ti 3:16; 1Pe 3:18

25. Nafsi

A. Maana ya nafsi

Mwanadamu ni nafsi. Mwa 2:7; 1Ko 15:45; Yos 11:11; Mdo 27:37

Wanyama huitwa nafsi pia. Hes 31:28; Ufu 16:3; Law 24:18

Nafsi ina damu, hula, yaweza kufa. Yer 2:34; Law 7:18; Eze 18:4

Mwanadamu, mwenye uhai, husemekana ana nafsi. Mk 8:36; Yoh 10:15

B. Kuna tofauti kati ya nafsi na roho

Uhai ukiwa mtu au kiumbe ni nafsi. Yoh 10:15; Law 17:11

Nguvu za uhai zinazotendesha nafsi huitwa “roho.” Zb 146:4; 104:29

Mtu anapokufa, mamlaka juu ya nguvu za uhai hurudi kwa Mungu. Mhu 12:7

Mungu tu ndiye anayeweza kutendesha nguvu za uhai. Eze 37:12-14

26. Ndoa

A. Lazima muungano wa ndoa uheshimiwe

Yafananishwa na Kristo na bibi-arusi. Efe 5:22, 23

Kitanda cha ndoa kisitiwe unajisi. Ebr 13:4

Wenzi wa ndoa washauriwa wasitengane. 1Ko 7:10-16

Por·neiʹa ndio msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka. Mt 19:9

B. Kanuni ya ukichwa lazima iheshimiwe na Wakristo

Mume akiwa kichwa lazima aipende, aitunze familia. Efe 5:23-31

Mke, hujitiisha, humpenda, humtii mume. 1Pe 3:1-7; Efe 5:22

Lazima watoto wawe watiifu. Efe 6:1-3; Kol 3:20

C. Daraka la wazazi Wakristo kwa watoto

Lazima waonyeshe upendo, kutoa wakati, uangalifu. Tit 2:4

Msiwakasirishe. Kol 3:21

Toa mahitaji, kutia ndani mambo ya kiroho. 2Ko 12:14; 1Ti 5:8

Wape mazoezi ya maisha. Efe 6:4; Met 22:6, 15; 23:13, 14

D. Wakristo wanapaswa kufunga ndoa na Wakristo tu

Funga ndoa “katika Bwana” tu. 1Ko 7:39; Kum 7:3, 4; Ne 13:26

E. Ndoa ya wake wengi si ya Kimaandiko

Mwanzoni mtu alipaswa kuwa na mke mmoja tu. Mwa 2:18, 22-25

Yesu alirudisha kiwango kwa Wakristo. Mt 19:3-9

Wakristo wa kwanza hawakuoa wake wengi. 1Ko 7:2, 12-16; Efe 5:28-31

27. Roho, Kuwasiliana na Pepo

A. Maana ya roho takatifu

Ni nguvu za utendaji za Mungu, si mtu. Mdo 2:2, 3, 33; Yoh 14:17

Ilitumiwa katika uumbaji, kuongoza uandikaji wa Biblia, n.k. Mwa 1:2; Eze 11:5

Huzaa, hutia mafuta, washiriki wa mwili wa Kristo. Yoh 3:5-8; 2Ko 1:21, 22

Hutia nguvu, huongoza watu wa Mungu leo. Ga 5:16, 18

B. Nguvu za uhai zinaitwa roho

Msingi wa uhai, hutegemezwa na kupumua. Yak 2:26; Ayu 27:3

Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya nguvu za uhai. Zek 12:1; Mhu 8:8

Nguvu za uhai za wanadamu, wanyama, ni mali ya Mungu. Mhu 3:19-21

Roho hukabidhiwa Mungu kukiwa na tumaini la ufufuo. Lu 23:46

C. Lazima kuwasiliana na pepo kuepukwe kwa kuwa ni kazi ya roho waovu

Neno la Mungu linakataza. Isa 8:19, 20; Law 19:31; 20:6, 27

Upigaji-ramli ni ibada ya roho waovu; unashutumiwa. Mdo 16:16-18

Huongoza kwenye uharibifu. Ga 5:19-21; Ufu 21:8; 22:15

Unajimu unakatazwa. Kum 18:10-12; Yer 10:2

28. Sabato

A. Siku ya Sabato si takwa kwa Wakristo

Sheria ilifutwa kwa msingi wa kifo cha Yesu. Efe 2:15

Sabato si takwa kwa Wakristo. Kol 2:16, 17; Ro 14:5, 10

Walikaripiwa kwa kushika Sabato, n.k. Ga 4:9-11; Ro 10:2-4

Wanaingia pumziko la Mungu kwa imani na utiifu. Ebr 4:9-11

B. Kushika Sabato kulitakiwa kwa Israeli wa kale tu

Sabato ilishikwa kwa mara ya kwanza baada ya Kutoka. Kut 16:26, 27, 29, 30

Ilikuwa ishara ya pekee kwa Israeli wa asili. Kut 31:16, 17; Zb 147:19, 20

Miaka ya Sabato pia ilikuwa takwa chini ya Sheria. Kut 23:10, 11; Law 25:3, 4

Sabato si lazima kwa Wakristo. Ro 14:5, 10; Ga 4:9-11

C. Pumziko la Mungu la Sabato (siku ya 7 ya “juma” la uumbaji)

Lilianza mwishoni mwa uumbaji duniani. Mwa 2:2, 3; Ebr 4:3-5

Liliendelea hata baada ya siku za Yesu duniani. Ebr 4:6-8; Zb 95:7-9, 11

Wakristo hupumzika kutokana na kazi za faida za kibinafsi. Ebr 4:9, 10

Litamalizika Ufalme utakapokamilisha kazi kuelekea dunia. 1Ko 15:24, 28

29. Sala

A. Sala ambazo Mungu husikia

Mungu husikiliza sala za wanadamu. Zb 145:18; 1Pe 3:12

Wasio waadilifu hawasikilizwi ila wabadili mwendo. Isa 1:15-17

Lazima mtu asali katika jina la Yesu. Yoh 14:13, 14; 2Ko 1:20

Lazima mtu asali kupatana na mapenzi ya Mungu. 1Yo 5:14, 15

Imani ni muhimu. Yak 1:6-8

B. Sala zinazorudiwa-rudiwa bure kwa Maria au “watakatifu” hazifai

Lazima kusali kwa Mungu katika jina la Yesu. Yoh 14:6, 14; 16:23, 24

Maneno ya kurudiwa-rudiwa hayatasikiwa. Mt 6:7

30. Siku za Mwisho

A. Maana ya “mwisho wa ulimwengu”

Mwisho wa mfumo wa mambo. Mt 24:3; 2Pe 3:5-7; Mk 13:4

Si mwisho wa dunia, bali wa mfumo mwovu. 1Yo 2:17

Wakati wa mwisho watangulia uharibifu. Mt 24:14

Kuokoka kwa waadilifu; ulimwengu mpya utafuata. 2Pe 2:9; Ufu 7:14-17

B. Uhitaji wa kukaa macho kuelekea ishara za siku za mwisho

Ishara zinatolewa na Mungu ili kutuongoza. 2Ti 3:1-5; 1Th 5:1-4

Ulimwengu unashindwa kutambua uzito. 2Pe 3:3, 4, 7; Mt 24:39

Mungu hakawii, bali hutoa onyo. 2Pe 3:9

Thawabu ya kukaa macho, kujali. Lu 21:34-36

31. Sikukuu, Sikukuu za Kuzaliwa

A. Sikukuu za kuzaliwa, Krismasi, hazikusherehekewa na Wakristo wa kwanza

Wale wasio waabudu wa kweli walisherehekea. Mwa 40:20; Mt 14:6

Siku ya kifo cha Yesu kufanyiwa ukumbusho. Lu 22:19, 20; 1Ko 11:25, 26

Sherehe za kupindukia hazifai. Ro 13:13; Ga 5:21; 1Pe 4:3

32. Tarehe za Matukio (Kronolojia)

A. 1914 (W.K.) hukomesha Nyakati za Wasio Wayahudi

Mfuatano wa watawala wa ufalme wakatizwa, 607 K.W.K. Eze 21:25-27

“Nyakati saba” kumalizika ndipo utawala urudishwe. Da 4:32, 16, 17

Saba = 2 × nyakati 3 1⁄2, au 2 × siku 1,260. Ufu 12:6, 14; 11:2, 3

Siku moja kwa mwaka mmoja. [Hufanya iwe miaka 2,520] Eze 4:6; Hes 14:34

Kuendelea mpaka kusimamishwa kwa Ufalme. Lu 21:24; Da 7:13, 14

33. Ubatizo

A. Ni takwa la Kikristo

Yesu aliweka kielelezo. Mt 3:13-15; Ebr 10:7

Huonyesha kujikana au kujiweka wakfu. Mt 16:24; 1Pe 3:21

Kwa wale tu wenye umri wa kutosha kufundishwa. Mt 28:19, 20; Mdo 2:41

Uzamisho majini ndiyo njia inayofaa. Mdo 8:38, 39; Yoh 3:23

B. Hauoshi dhambi

Yesu hakubatizwa ili kuosha dhambi. 1Pe 2:22; 3:18

Damu ya Yesu ndiyo huosha dhambi. 1Yo 1:7

34. Ufalme

A. Mambo ambayo Ufalme wa Mungu utawafanyia wanadamu

Kutimiza mapenzi ya Mungu. Mt 6:9, 10; Zb 45:6; Ufu 4:11

Serikali yenye mfalme na sheria. Isa 9:6, 7; 2:3; Zb 72:1, 8

Utaharibu uovu, utatawala dunia nzima. Da 2:44; Zb 72:8

Utawala wa miaka 1,000 utaponya wanadamu, kurudisha Paradiso. Ufu 21:2-4; 20:6

B. Utendaji waanza wakati adui za Kristo wangali wanatenda

Baada ya Kristo kufufuliwa alingojea muda mrefu. Zb 110:1; Ebr 10:12, 13

Aanza kutawala, apigana na Shetani. Zb 110:2; Ufu 12:7-9; Lu 10:18

Ufalme ulisimamishwa wakati huo, ole za dunia zinafuata. Ufu 12:10, 12

Taabu ya sasa yamaanisha ni wakati wa kuunga mkono Ufalme. Ufu 11:15-18

C. Haumo ‘katika mioyo,’ hausitawishwi kupitia jitihada za wanadamu

Ufalme uko mbinguni, si duniani. 2Ti 4:18; 1Ko 15:50; Zb 11:4

Haumo ‘katika mioyo’; Yesu alikuwa akizungumza na Mafarisayo. Lu 17:20, 21

Si sehemu yoyote ya ulimwengu huu. Yoh 18:36; Lu 4:5-8; Da 2:44

Utachukua mahali pa serikali na viwango vya ulimwengu. Da 2:44

35. Ufufuo

A. Tumaini kwa wafu

Wote walio makaburini watafufuliwa. Yoh 5:28, 29

Ufufuo wa Yesu ni uhakikisho kamili. 1Ko 15:20-22; Mdo 17:31

Watenda-dhambi juu ya roho hawatafufuliwa. Mt 12:31, 32

Wale wanaoonyesha imani wamehakikishiwa hilo. Yoh 11:25

B. Ufufuo kwenye uzima ama mbinguni au duniani

Wote hufa katika Adamu; hupokea uzima katika Yesu. 1Ko 15:20-22; Ro 5:19

Watakaofufuliwa watakuwa na maumbile tofauti. 1Ko 15:40, 42, 44

Wale walio pamoja na Yesu watakuwa kama yeye. 1Ko 15:49; Flp 3:20, 21

Wale wasiotawala watakuwa duniani. Ufu 20:4b, 5, 13; 21:3, 4

36. Ukumbusho, Misa

A. Ukumbusho wa Mlo wa Jioni wa Bwana

Hufanywa mara moja kwa mwaka katika siku ya Pasaka. Lu 22:1, 17-20; Kut 12:14

Ni kuadhimisha kifo cha kidhabihu cha Kristo. 1Ko 11:26; Mt 26:28

Wenye tumaini la mbinguni hushiriki kula. Lu 22:29, 30; 12:32, 37

Jinsi mtu anavyojua ana tumaini hilo. Ro 8:15-17

B. Misa si ya Kimaandiko

Msamaha wa dhambi hutaka damu imwagwe. Ebr 9:22

Kristo ndiye Mpatanishi mmoja tu wa agano jipya. 1Ti 2:5, 6; Yoh 14:6

Kristo yuko mbinguni; hashushwi chini na kasisi. Mdo 3:20, 21

Hakuna uhitaji wa kutoa tena dhabihu ya Kristo. Ebr 9:24-26; 10:11-14

37. Uovu, Taabu za Ulimwengu

A. Anayesababisha taabu za ulimwengu

Utawala mwovu ni kisababishi cha nyakati mbaya leo. Met 29:2; 28:28

Mtawala wa ulimwengu ni adui ya Mungu. 2Ko 4:4; 1Yo 5:19; Yoh 12:31

Ole zinaletwa na Ibilisi, wakati ni mfupi. Ufu 12:9, 12

Ibilisi kufungwa, amani tukufu kufuata. Ufu 20:1-3; 21:3, 4

B. Sababu ya uovu kuruhusiwa

Ibilisi alitilia shaka ushikamanifu wa viumbe kwa Mungu. Ayu 1:11, 12

Waaminifu wamepewa nafasi ya kuthibitisha ushikamanifu. Ro 9:17; Met 27:11

Ibilisi amethibitishwa kuwa mwongo, suala litasuluhishwa. Yoh 12:31

Waaminifu watapewa thawabu ya uzima wa milele. Ro 2:6, 7; Ufu 21:3-5

C. Wakati wa mwisho uliorefushwa ni uandalizi wenye rehema

Kama katika siku za Noa, huchukua muda kutoa onyo. Mt 24:14, 37-39

Mungu hakawii, bali ni mwenye rehema. 2Pe 3:9; Isa 30:18

Biblia hutusaidia tusinaswe ghafula. Lu 21:36; 1Th 5:4

Tafuta uandalizi wa Mungu sasa ili kupata ulinzi. Isa 2:2-4; Sef 2:3

D. Suluhisho la taabu za ulimwengu si kutoka kwa wanadamu

Wanadamu wanahofu sana, wanafadhaika. Lu 21:10, 11; 2Ti 3:1-5

Ufalme wa Mungu utafaulu, si wanadamu. Da 2:44; Mt 6:10

Ili kuishi, fanya amani na Mfalme sasa. Zb 2:9, 11, 12

38. Upinzani, Mateso

A. Sababu Wakristo wapingwa

Yesu alichukiwa, alitabiri upinzani. Yoh 15:18-20; Mt 10:22

Kushikamana na kanuni za haki huhukumu ulimwengu. 1Pe 4:1, 4, 12, 13

Shetani, mungu wa mfumo huu, hupinga Ufalme. 2Ko 4:4; 1Pe 5:8

Mkristo haogopi, Mungu hutegemeza. Ro 8:38, 39; Yak 4:8

B. Mke hapaswi kumruhusu mume amtenge na Mungu

Ilionywa kimbele; huenda wengine wakampa habari zisizo za kweli. Mt 10:34-38; Mdo 28:22

Lazima mke amtegemee Mungu na Kristo. Yoh 6:68; 17:3

Kwa uaminifu huenda akaokoa mume pia. 1Ko 7:16; 1Pe 3:1-6

Mume ni kichwa, lakini hapaswi kuamuru juu ya ibada. 1Ko 11:3; Mdo 5:29

C. Mume hapaswi kumruhusu mke amzuie asimtumikie Mungu

Lazima ampende mke na familia, atake wapate uzima. 1Ko 7:16

Ana daraka la kuamua, kutoa riziki. 1Ko 11:3; 1Ti 5:8

Mungu humpenda mwanamume anayetetea kweli. Yak 1:12; 5:10, 11

Kukosa msimamo ili kuwe amani hufanya mtu akose kibali cha Mungu. Ebr 10:38

Aongoze familia kwenye furaha katika ulimwengu mpya. Ufu 21:3, 4

39. Utatu

A. Mungu, Baba, ni Mtu mmoja, mkuu zaidi katika ulimwengu mzima

Mungu si watu watatu. Kum 6:4; Mal 2:10; Mk 10:18; Ro 3:29, 30

Mwana aliumbwa; Mungu alikuwa peke yake kabla ya hapo. Ufu 3:14; Kol 1:15; Isa 44:6

Mungu ni mtawala wa ulimwengu mzima nyakati zote. Flp 2:5, 6; Da 4:35

Mungu atainuliwa juu ya wote. Flp 2:10, 11

B. Mwana ni mdogo kwa Baba kabla na baada ya kuja duniani

Mwana alikuwa mtiifu mbinguni, alitumwa na Baba. Yoh 8:42; 12:49

Alikuwa mtiifu duniani, Baba ni mkuu zaidi. Yoh 14:28; 5:19; Ebr 5:8

Amepandishwa cheo mbinguni, bado anajitiisha. Flp 2:9; 1Ko 15:28; Mt 20:23

Yehova ni kichwa na Mungu wa Kristo. 1Ko 11:3; Yoh 20:17; Ufu 1:6

C. Umoja wa Mungu na Kristo

Sikuzote wana upatano kamili. Yoh 8:28, 29; 14:10

Umoja, kama ule wa mume na mke. Yoh 10:30; Mt 19:4-6

Waamini wote lazima wawe na umoja uleule. Yoh 17:20-22; 1Ko 1:10

Ibada moja ya Yehova kupitia Kristo milele. Yoh 4:23, 24

D. Roho takatifu ya Mungu ni nguvu zake za utendaji

Ni nguvu, si mtu. Mt 3:16; Yoh 20:22; Mdo 2:4, 17, 33

Hiyo si mtu aliye mbinguni pamoja na Mungu na Kristo. Mdo 7:55, 56; Ufu 7:10

Hiyo huelekezwa na Mungu ili kutimiza makusudi yake. Zb 104:30; 1Ko 12:4-11

Wanaotumikia Mungu huipokea, huongozwa nayo. 1Ko 2:12, 13; Ga 5:16

40. Uumbaji

A. Wakubaliana na sayansi iliyothibitishwa; hukanusha mageuzi

Sayansi hukubaliana na utaratibu wa uumbaji. Mwa 1:11, 12, 21, 24, 25

Sheria ya Mungu ya viumbe kuzaa kulingana na “aina” yake ni ya kweli. Mwa 1:11, 12; Yak 3:12

B. Siku za uumbaji si siku za saa 24

“Siku” yaweza kumaanisha tu kipindi cha wakati. Mwa 2:4

Siku moja kwa Mungu yaweza kuwa muda mrefu. Zb 90:4; 2Pe 3:8

41. Uzima

A. Uzima wa milele umehakikishiwa wanadamu watiifu

Mungu, ambaye hawezi kusema uwongo, ameahidi uzima. Tit 1:2; Yoh 10:27, 28

Uzima wa milele umehakikishiwa wale wanaoonyesha imani. Yoh 11:25, 26

Kifo kitaharibiwa. 1Ko 15:26; Ufu 21:4; 20:14; Isa 25:8

B. Uzima wa mbinguni ni kwa wale tu walio ndani ya mwili wa Kristo

Mungu huchagua washiriki kama inavyompendeza. Mt 20:23; 1Ko 12:18

Ni 144,000 tu wanaochukuliwa kutoka duniani. Ufu 14:1, 4; 7:2-4; 5:9, 10

Hata Yohana Mbatizaji hatakuwa katika Ufalme wa mbinguni. Mt 11:11

C. Uzima duniani umeahidiwa hesabu isiyo na kikomo, “kondoo wengine”

Hesabu iliyo na kikomo pamoja na Yesu mbinguni. Ufu 14:1, 4; 7:2-4

“Kondoo wengine” si ndugu za Kristo. Yoh 10:16; Mt 25:32, 40

Wengi sasa wanakusanyika kwa ajili ya wokovu duniani. Ufu 7:9, 15-17

Wengine watafufuliwa kwa ajili ya uzima duniani. Ufu 20:12; 21:4

42. Wokovu

A. Wokovu hutoka kwa Mungu kupitia dhabihu ya fidia ya Yesu

Uzima ni zawadi ya Mungu kupitia Mwana wake. 1Yo 4:9, 14; Ro 6:23

Wokovu unawezekana tu kupitia dhabihu ya Yesu. Mdo 4:12

Matendo hayawezekani wakati wa “toba ya wakati wa kufa.” Yak 2:14, 26

Lazima kujitahidi ili kuufikia. Lu 13:23, 24; 1Ti 4:10

B. “Mtu akiisha kuokolewa, ameokolewa sikuzote” si wazo la Kimaandiko

Washiriki wa roho takatifu wanaweza kuanguka. Ebr 6:4, 6; 1Ko 9:27

Waisraeli wengi waliharibiwa ingawa waliokolewa kutoka Misri. Yuda 5

Wokovu si jambo la kutokea dakika moja. Flp 2:12; 3:12-14; Mt 10:22

Wale wanaokengeuka wanakuwa wabaya zaidi kuliko hapo mwanzoni. 2Pe 2:20, 21

C. “Kuokolewa kwa watu wote ulimwenguni” si wazo la Kimaandiko

Toba haiwezekani kwa wengine. Ebr 6:4-6

Mungu hapendezwi na kifo cha mwovu. Eze 33:11; 18:32

Lakini upendo hauwezi kuendekeza ukosefu wa uadilifu. Ebr 1:9

Waovu wataharibiwa. Ebr 10:26-29; Ufu 20:7-15

43. Yehova, Mungu

A. Jina la Mungu

“Mungu” si jina la kibinafsi; Bwana wetu ana jina la kibinafsi. 1Ko 8:5, 6

Tunasali jina lake litakaswe. Mt 6:9, 10

Jina la Mungu ni Yehova. Zb 83:18; Kut 6:2, 3; 3:15; Isa 42:8

Jina katika Biblia ya Union Version ya Kiswahili. Kut. 6:3; Zb 83:18; Isa 12:2; 26:4, n.k.

Yesu alijulisha jina hilo. Yoh 17:6, 26; 5:43; 12:12, 13, 28

B. Kuwako kwa Mungu

Haiwezekani kumwona Mungu na kuishi. Kut 33:20; Yoh 1:18; 1Yo 4:12

Si lazima kumwona Mungu ili kuamini. Ebr 11:1; Ro 8:24, 25; 10:17

Mungu anajulikana kwa kazi zake zinazoonekana. Ro 1:20; Zb 19:1, 2

Utimizo wa unabii unathibitisha kuwako kwa Mungu. Isa 46:8-11

C. Sifa za Mungu

Mungu ni upendo. 1Yo 4:8, 16; Kut 34:6; 2Ko 13:11; Mik 7:18

Ana hekima kuu. Ayu 12:13; Ro 11:33; 1Ko 2:7

Anatenda kwa haki. Kum 32:4; Zb 37:28

Ni mweza-yote, ana nguvu zote. Ayu 37:23; Ufu 7:12; 4:11

D. Si wote wanaomtumikia Mungu yule mmoja

Njia ambayo huonekana njema si yenye kufaa sikuzote. Met 16:25; Mt 7:21

Barabara mbili, ni moja tu inayoongoza kwenye uzima. Mt 7:13, 14; Kum 30:19

Miungu mingi lakini kuna Mungu mmoja tu wa kweli. 1Ko 8:5, 6; Zb 82:1

Kumjua Mungu wa kweli ni lazima ili kupata uzima. Yoh 17:3; 1Yo 5:20

44. Yesu

A. Yesu ni Mwana wa Mungu na Mfalme aliyewekwa rasmi

Mzaliwa wa kwanza wa Mungu, alitumiwa kuumba vitu vingine vyote. Ufu 3:14; Kol 1:15-17

Alifanywa kuwa mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, mdogo kidogo kuliko malaika. Ga 4:4; Ebr 2:9

Alizaliwa kwa roho ya Mungu, akikusudiwa kuwa mbinguni. Mt 3:16, 17

Alipandishwa kwenye cheo cha juu zaidi kuliko wakati wa maisha yake kabla ya kuwa mwanadamu. Flp 2:9, 10

B. Imani katika Yesu Kristo ni ya lazima ili kupata wokovu

Kristo ndiye Uzao ulioahidiwa wa Abrahamu. Mwa 22:18; Ga 3:16

Yesu tu ndiye Kuhani Mkuu, na fidia. 1Yo 2:1, 2; Ebr 7:25, 26; Mt 20:28

Uzima unapatikana kwa kumjua Mungu na Kristo, kutii. Yoh 17:3; Mdo 4:12

C. Mengi zaidi ya imani katika Yesu yanahitajiwa

Imani ni lazima iambatane na matendo. Yak 2:17-26; 1:22-25

Lazima kuzitii amri, kufanya kazi aliyofanya. Yoh 14:12, 15; 1Yo 2:3

Si wote wanaotumia jina la Bwana watakaoingia katika Ufalme. Mt 7:21-23

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki