Wimbo Na. 34
Kuishi Kulingana na Jina Letu
Makala Iliyochapishwa
1. Yah Mweza Yote, wa tangu milele,
Mungu wa haki, ’pendo na nguvu,
Chanzo cha kweli na hekima yote,
Mutawala Mwenye Enzi kuu.
Tunafurahi kukutumikia,
Kweli ya Ufalme twatangaza!
(KORASI)
Ni pendeleo kuwa Mashahidi.
Ee, Na tuishi kwa jina letu!
2. Tufanyapo kazi bega kwa bega,
Upendo unatuunganisha,
Kufunza kweli na kukutukuza;
Hutupa sisi furaha tele.
Twaitwa kwa jina lako Yehova;
Twapendelewa kukupa sifa!
(KORASI)
Ni pendeleo kuwa Mashahidi.
Ee, Na tuishi kwa jina letu!
(Ona pia Kum. 32:4; Zab. 43:3; Dan. 2:20, 21.)