Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr20 Mei kur. 1-2
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
  • Vichwa vidogo
  • MEI 4-10
  • MEI 11-17
  • MEI 25-31
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
mwbr20 Mei kur. 1-2

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

MEI 4-10

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 36-37

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 678

Edomu

(E·do·mu) [Nyekundu] Waedomu (Wa·e·do·mu).

Edomu lilikuwa jina la pili ambalo Esau, pacha ya Yakobo alipewa. (Mwa 36:1) Alipewa jina hilo kwa sababu ya kuuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa kubadilishana na mchuzi mwekundu. (Mwa 25:30-34) Kwa sadfa, Esau alikuwa mwekundu sana alipozaliwa (Mwa 25:25), na ardhi ambayo yeye na wazao wake walimiliki baadaye ilikuwa na rangi hiyo pia.

it-1 561-562

Utunzaji

Mchungaji aliposema kwamba angewachunga au kuwalinda kondoo, alikuwa akionyesha kwamba anakubali kisheria kuwa mtunzaji wa wanyama hao. Alikuwa akimhakikishia mmiliki kwamba wangelishwa na kwamba hawataibiwa, la sivyo angelipa fidia. Hata hivyo, sheria ilimwondolea mtunzaji huyo lawama wakati ambapo hali zinazopita uwezo wa kibinadamu zilitokea, kama vile kondoo waliposhambuliwa na wanyama wa mwituni. Ili aondolewe wajibu huo, alipaswa kumletea mmiliki wa wanyama hao ushahidi, kama vile, mzoga ulioraruliwa na wanyama wa mwituni. Baada ya kuchunguza ushahidi huo, mmiliki wa wanyama hao alipaswa kumtangaza mtunzaji huyo kuwa hana hatia.

Kanuni hiyo ilitumiwa kwa ujumla kwa mali yoyote ambayo mtu alikabidhiwa, hata katika mahusiano ya familia. Kwa mfano, mtoto wa kwanza wa kiume alionwa kuwa mtunzaji wa kisheria wa ndugu na dada zake wadogo. Hilo linatusaidia kuelewa kwa nini Rubeni akiwa mwana wa kwanza wa Yakobo alijaribu kuokoa uhai wa Yosefu wakati ambapo ndugu zake walitaka kumuua, kama andiko la Mwanzo 37:18-30 linavyoonyesha. Alisema: “‘Tusimuue.’ . . . ‘Msimwage damu. . . . msimdhuru.’ Rubeni alikusudia kumwokoa kutoka mikononi mwao ili amrudishe kwa baba yake.” Baadaye, Rubeni alipogundua kwamba Yosefu hakuwepo, alikuwa na wasiwasi mwingi sana hivi kwamba “akayararua mavazi yake” na kusema hivi kwa mshangao: “Mtoto amepotea! Sasa mimi—nitafanya nini?” Alijua kwamba angewajibika kwa sababu ya kumpoteza Yosefu. Ili kukwepa lawama, kwa ujanja ndugu hao walileta ushahidi wa uwongo ulioonyesha kwamba Yosefu alikuwa ameuawa na mnyama wa mwituni. Walifanya hivyo kwa kuchovya joho la Yosefu lenye mistari ndani ya damu ya mbuzi. Kisha wakampelekea Yakobo, baba yao, ambaye pia alikuwa mwamuzi wa ukoo wao, ushahidi huo, naye Yakobo akamwondolea Rubeni hatia kwa sababu, kwa msingi wa joho la Yosefu lililojaa damu ambalo liliwasilishwa na ndugu zake kama ushahidi, Yakobo alifikia mkataa kwamba Yosefu alikuwa ameuawa.—Mwa 37:31-33.

MEI 11-17

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 38-39

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 555

Onani

(O·na·ni) [linatokana na “nguvu za kujitokeza, nguvu zenye msukumo”].

Mwana wa pili wa Yuda kupitia binti ya Shua Mkanaani. (Mwa 38:2-4; 1Nya 2:3) Baada ya Eri, aliyekuwa ndugu yake mkubwa kufa bila kupata mtoto, Onani aliambiwa afunge ndoa ya ndugu-mkwe na Tamari, mjane wa Eri. Ikiwa angezaa mwana, mwana huyo asingekuwa mwanzilishi wa familia ya Onani, na urithi wa mwana mzaliwa wa kwanza ungekuwa wa mwana huyo akiwa mrithi wa Eri; ilhali ikiwa mrithi asingezaliwa, Onani ndiye angepata urithi huo. Onani alipolala na Tamari, “alimwaga shahawa zake ardhini” badala ya kumpa Tamari. Kwa kufanya hivyo, Onani hakuwa akipiga punyeto, kwa kuwa simulizi hilo linasema “alipolala na mke wa ndugu yake” alimwaga shahawa zake. Inaonekana kwamba Onani alizuia kimakusudi kumwaga shahawa ndani ya njia ya uzazi ya Tamari. Licha ya kwamba Onani hakuwa na mtoto, Yehova alimuua kwa kukosa kumtii baba yake, kwa sababu ya tamaa yake, na kwa kutenda dhambi dhidi ya mpango wa ndoa wa Mungu, na si kwa sababu ya kupiga punyeto.—Mwa 38:6-10; 46:12; Hes 26:19.

MEI 25-31

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 42-43

“Yosefu Aonyesha Sifa ya Kujizuia”

it-2 108 ¶4

Yosefu

Kwa sababu ya mambo yaliyotukia, ndugu wa kambo wa Yosefu walianza kuhisi kwamba Mungu anawaadhibu kwa kumuuza Yosefu utumwani miaka mingi iliyopita. Wakiwa mbele ya ndugu yao, ambaye bado hawakumtambua, walianza kuzungumzia jinsi walivyokuwa na hatia. Yosefu aliposikia maneno yao yaliyoonyesha toba, alilemewa na hisia hivi kwamba akalazimika kuondoka mbele yao ili alie. Aliporudi, aliagiza kwamba Simeoni afungwe hadi wakati ambapo watarudi wakiwa na ndugu yao mdogo.—Mwa 42:21-24.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 795

Rubeni

Sifa fulani nzuri za Rubeni zilionekana alipowasihi ndugu zake tisa wasimuue Yosefu badala yake wamtupe ndani ya shimo ambalo halikuwa na maji. Rubeni alikusudia kurudi kwa siri ili kumwokoa Yosefu kutoka kwenye shimo hilo. (Mwa 37:18-30) Miaka 20 hivi baadaye ndugu hao walipolaumiana kwamba walikuwa wakishtakiwa kuwa wapelelezi nchini Misri kwa sababu walikuwa wamemtesa Yosefu, Rubeni aliwakumbusha wenzake kwamba yeye hakuhusika katika njama yao ya kumuua Yosefu. (Mwa 42:9-14, 21, 22) Pia, Yakobo alipokataa kumruhusu Benjamini aambatane na ndugu zake kurudi Misri mara ya pili, ni Rubeni aliyewatoa watoto wake wawili kuwa dhamana, akisema: “Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha [Benjamini] kwako.” —Mwa 42:37.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki