Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr20 Aprili kur. 1-2
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
  • Vichwa vidogo
  • APRILI 13-19
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
mwbr20 Aprili kur. 1-2

Marejeo ya Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo

APRILI 13-19

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 31

“Yakobo na Labani Wafanya Agano la Amani”

it-1 883 ¶1

Galeedi

Yakobo na Labani walifanya agano baada ya kupatana kuhusu mambo waliyokuwa wakizozania. Kwa hiyo, Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe na kuwaagiza “ndugu” zake watengeneze rundo la mawe, ambalo huenda yalitengenezwa katika muundo wa meza na wakala mlo wa agano. Labani alipaita mahali hapo kwa jina la Kiaramu (Kisiria) “Yegar-sahadutha,” lakini Yakobo akapaita “Galeedi,” katika lugha ya Kiebrania. Majina yote mawili yalikuwa na maana ileile. Labani alisema: “Rundo hili la mawe [Kiebrania, gal] ni ushahidi [Kiebrania, ʽedh] kati yangu mimi na wewe leo.” (Mwa 31:44-48) Rundo hilo la mawe (na nguzo ya jiwe) likawa ushahidi kwa wapita-njia wote. Pia katika mstari wa 49 uliitwa, “Mnara wa Mlinzi [Kiebrania, mits·pahʹ],” kwa sababu ulikuwa ushahidi kwamba Yakobo na Labani walikubaliana kudumisha amani kati yao na katika familia zao. (Mwa 31:50-53) Baadaye mawe yalitumiwa kwa njia hiyohiyo kutoa ushahidi kimyakimya.—Yos 4:4-7; 24:25-27.

it-2 1172

Mnara wa Mlinzi

Yakobo alitengeneza rundo la mawe na kuliita “Galeedi” (linalomaanisha “Rundo la Ushahidi”) na “Mnara wa Mlinzi.” Kisha Labani akasema: “Yehova na awe mlinzi kati yangu mimi na wewe tunapokuwa hatuonani.” (Mwa 31:45-49) Rundo hilo la mawe lilingetoa ushahidi kwamba Yehova alikuwa akiangalia kuona ikiwa Yakobo na Labani walikuwa wakitimiza agano lao la amani.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 1087-1088

Terafimu

Utafiti wa wachimbuaji wa vitu vya kale kule Mesapotamia na maeneo yanayozunguka yanaonyesha kwamba kumiliki terafimu kuliashiria ni nani ambaye angepokea urithi wa familia. Kulingana na bamba fulani lenye maandishi lililopatikana kule Nuzi, katika hali fulani ikiwa mwana-mkwe angemiliki miungu ya familia angeweza kwenda mahakamani na kudai mali ya baba-mkwe aliyekufa. (Ancient Near Eastern Texts, edited by J. Pritchard, 1974, pp. 219, 220, and ftn 51) Labda Raheli alikuwa na wazo hilo akilini na hivyo akaona kwamba alikuwa na haki ya kuchukua terafimu kwa sababu ya matendo ya udanganyifu ambayo baba yake alimtendea Yakobo. (Linganisha Mwa 31:14-16.) Umuhimu wa terafimu kuhusiana na haki za urithi unaonyesha kwa nini Labani alihangaika sana kuzipata hivi kwamba aliambatana na ndugu zake alipokuwa akimfuata Yakobo umbali wa safari ya siku saba. (Mwa 31:19-30) Bila shaka, Yakobo hakujua jambo ambalo Raheli alikuwa amefanya (Mwa 31:32), na hakuna jambo lolote linaloonyesha kwamba alikusudia kutumia terafimu hizo kuwanyang’anya wana wa Labani urithi. Yakobo hakujihusisha kamwe na sanamu. Bila shaka, terafimu hizo zilikuwa zimeharibiwa kufikia wakati ambapo Yakobo alifukia miungu ya kigeni chini ya ule mti mkubwa uliokuwa karibu na Shekemu, au ziliharibiwa wakati huo.—Mwa 35:1-4.

APRILI 20-26

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 32-33

“Je, Unapigana Mweleka Kupata Baraka?”

it-2 190

Kilema, Ulemavu

Ulemavu wa Yakobo. Yakobo alipokuwa na umri wa miaka 97 hivi, alipigana mweleka usiku wote na malaika aliyekuwa amejivika mwili wa mwanadamu. Alifanikiwa kumzuia malaika huyo asiondoke hadi alipombariki. Wakati wa pambano hilo, malaika aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo, na kukitegua. Kwa sababu hiyo, Yakobo akaanza kuchechemea. (Mwa 32:24-32; Ho  12:2-4) Hilo lingemkumbusha Yakobo kwamba ingawa malaika huyo alisema Yakobo ‘alipambana na Mungu [malaika wa Mungu] na wanadamu na hatimaye akashinda,’ ukweli ni kwamba hakumshinda malaika mwenye nguvu wa Mungu. Yakobo alipewa nafasi ya kupambana na malaika huyo kwa sababu hilo lilipatana na kusudi la Mungu, naye aliruhusu hilo ili kuthibitisha kwamba Yakobo alitamani sana kupata baraka kutoka kwa Mungu.

it-1 1228

Israeli

1. Jina ambalo Mungu alimpa Yakobo alipokuwa na umri wa miaka 97 hivi. Yakobo alipigana na malaika usiku ambao alikuwa njiani kwenda kukutana na ndugu yake Esau, baada ya kuvuka kijito cha Yaboki. Kwa sababu alistahimili katika pambano hilo, jina lake lilibadilishwa kuwa Israeli kama ishara ya baraka za Mungu. Ili kukumbuka matukio hayo, Yakobo alipaita mahali hapo Penieli au Penueli. (Mwa 32:22-31; ona YAKOBO Na. 1.) Baadaye, alipokuwa Betheli Mungu alithibitisha kwamba jina lake lilikuwa limebadilishwa, na kuanzia wakati huo hadi Yakobo alipokufa aliitwa Israeli. (Mwa 35:10, 15; 50:2; 1Nya 1:34) Ingawa hivyo, jina hilo linapotajwa zaidi ya mara 2,500 katika Biblia mara nyingi zaidi linatumiwa kuwarejelea wazao wa Yakobo wakiwa kama taifa.—Kut 5:1, 2.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 980

Mungu, Mungu wa Israeli

Baada ya kupambana na malaika wa Yehova huko Penieli, Yakobo alipewa jina Israeli. Baada ya kukutana na Esau ndugu yake na kufanya amani, Yakobo aliishi katika eneo la Sukothi na kisha akahamia Shekemu. Akiwa huko alinunua kisehemu fulani cha shamba kutoka kwa wana wa Hamori na kupiga hema lake hapo. (Mwa 32:24-30; 33:1-4, 17-19) “Akajenga madhabahu huko na kuiita Mungu, Mungu wa Israeli,” au “Mungu Aliye Mungu wa Israeli.” (Mwa 33:20) Kwa kutaja jina lake jipya Israeli na kulihusianisha na jina la madhabahu hiyo, Yakobo alionyesha kwamba anakubali na kuthamini jina hilo na kumshukuru Mungu kwa kumrudisha salama katika Nchi ya Ahadi. Maneno hayo yanapatikana mara moja tu katika Maandiko.

APRILI 27–MEI 3

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 600 ¶4

Debora

1. Mlezi wa Rebeka. Rebeka alipoondoka nyumbani kwa Betheuli baba yake, na kuhamia Palestina ili kuolewa na Isaka, Debora aliambatana naye. (Mwa 24:59) Baada ya kutumikia nyumbani kwa Isaka kwa miaka mingi, huenda Debora alihamia nyumbani kwa Yakobo Rebeka alipokufa. Inaonekana kwamba miaka 125 baada ya Rebeka kuolewa na Isaka, Debora alikufa na kuzikwa chini ya mti mkubwa huko Betheli. Jina la mti huo (Alon-bakuthi, linalomaanisha “Mti Mkubwa wa Maombolezo”) linaonyesha jinsi alivyopendwa sana na Yakobo na familia yake.—Mwa 35:8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki