Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr20 Machi kur. 1-2
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
  • Vichwa vidogo
  • MACHI 2-8
  • MACHI 16-22
  • MACHI 23-29
  • MACHI 30–APRILI 5
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
mwbr20 Machi kur. 1-2

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

MACHI 2-8

BORESHA HUDUMA YAKO

it-1 604 ¶5

Abrahamu angewezaje kutangazwa kuwa mwadilifu kabla ya kifo cha Kristo?

Pia, imani ya Abrahamu, pamoja na kazi zake, ‘ilihesabiwa [ilitangazwa au kuonekana] kwake kuwa uadilifu.’ (Ro 4:20-22) Bila shaka, hilo halimaanishi kwamba yeye na wanaume wengine waaminifu walioishi kabla ya nyakati za Ukristo walikuwa wakamilifu au hawakuwa na dhambi; hata hivyo, kwa sababu ya kuonyesha imani katika ahadi ya Mungu kuhusu ule “uzao” na kwa sababu walijitahidi kufuata amri za Mungu, hawakuhesabiwa kuwa wasio waadilifu bila kuwa na kibali cha Mungu, kama wanadamu wengine. (Mwa 3:15; Zb 119:2, 3) Kwa upendo Yehova aliwahesabu kuwa wasio na hatia, wakilinganishwa na ulimwengu wa wanadamu uliotengwa na Mungu. (Zb 32:1, 2; Efe 2:12) Hivyo, kwa sababu ya imani yao, Mungu angeweza kushughulika na wanadamu kama hao wasio wakamilifu na kuwabariki, bila kuvunja viwango vyake vikamilifu vya haki. (Zb 36:10) Hata hivyo, wanadamu hao walitambua uhitaji wao wa kukombolewa kutoka katika dhambi na walikuwa wakisubiri wakati wa Mungu wa kuandaa ukombozi.—Zb 49:7-9; Ebr 9:26.

MACHI 16-22

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 25-26

“Esau Auza Haki Yake ya Kuzaliwa”

it-1 1242

Yakobo

Yakobo alikuwa tofauti sana na ndugu yake Esau. Esau hakuwa mtulivu, alikuwa mtu wa mbugani, mwindaji wa kuhamahama, na alipendwa sana na baba yake. Yakobo anafafanuliwa kuwa “mtu asiye na lawama [Kiebrania, tam], anayekaa katika mahema,” ambaye aliishi maisha kuchunga kondoo na alikuwa mwenye kutegemeka ilipohusu kushughulikia mambo ya nyumbani, na alipendwa sana na mama yake. (Mwa 25:27, 28) Neno hilo la Kiebrania tam linatumiwa katika sehemu nyingine kuwafafanua watu walio na kibali cha Mungu. Kwa mfano, “watu wenye kiu ya damu humchukia mtu yeyote asiye na hatia,” hata hivyo, Yehova anatuhakikishia kwamba “wakati ujao wa mtu huyo [asiye na lawama] utakuwa na amani.” (Met 29:10; Zb 37:37) Ayubu aliyekuwa mtimilifu “alikuwa asiye na lawama na mnyoofu.”—Ayu 1:1, 8, maelezo ya chini; 2:3.

it-1 835

Mzaliwa wa Kwanza

Tangu zamani mwana mzaliwa wa kwanza alikuwa na cheo cha pekee katika familia na ndiye aliyechukua ukichwa baba alipokufa. Alipata urithi maradufu wa mali za baba. (Kum 21:17) Wakati wa mlo Yosefu aliagiza kwamba Rubeni aketi mahali alipostahili kulingana na haki yake akiwa mzaliwa wa kwanza. (Mwa 43:33) Lakini si kila wakati ambapo Biblia huorodhesha majina ya wana kwa njia ambayo itampa heshima ya pekee mzaliwa wa kwanza. Mara nyingi, mwana ambaye ni maarufu au mshikamanifu ndiye huorodheshwa kwanza.—Mwa 6:10; 1Nya 1:28; linganisha Mwa 11:26, 32; 12:4; ona HAKI YA KUZALIWA; URITHI.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 245 ¶6

Uwongo

Licha ya kwamba uwongo unaodhuru unashutumiwa katika Biblia, hilo halimaanishi kwamba lazima mtu awape watu wasiohusika habari za kweli. Yesu Kristo alitoa shauri hili: “Msiwape mbwa kitu kitakatifu, wala msiwatupie nguruwe lulu zenu, wasije wakazikanyaga-kanyaga chini ya miguu yao, kisha wageuke na kuwararua ninyi.” (Mt 7:6) Hiyo ndiyo sababu nyakati nyingine Yesu hakutoa habari zote wala hakujibu maswali fulani moja kwa moja ikiwa kufanya hivyo kungetokeza madhara. (Mt 15:1-6; 21:23-27; Yoh 7:3-10) Ni wazi kwamba tunapaswa kuelewa kwa njia hiyohiyo matendo ya Abrahamu, Isaka, Rahabu, na Elisha ya kuwaongoza vibaya au kukosa kuwapa habari zote watu ambao hawakuwa watumishi wa Yehova.—Mwa 12:10-19; sura ya 20; 26:1-10; Yos 2:1-6; Yak 2:25; 2Fa 6:11-23.

MACHI 23-29

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 27-28

“Yakobo Apata Baraka Aliyostahili”

it-1 341 ¶6

Baraka

Katika jamii ya wazee wa ukoo, ilikuwa kawaida kwa baba kuwabariki wanawe muda mfupi kabla ya kufa. Hilo lilikuwa tukio muhimu na lilithaminiwa sana. Hivyo, Isaka alimbariki Yakobo akifikiri kwamba ni mzaliwa wake wa kwanza Esau. Kwa kuwa Isaka alikuwa kipofu na alikuwa amezeeka, alimwambia Yakobo kwamba atapata kibali na ufanisi mbele ya ndugu yake Esau, na akamwomba Yehova atekeleze baraka hizo. (Mwa 27:1-4, 23-29; 28:1, 6; Ebr 11:20; 12:16, 17) Baadaye, kwa hiari yake Isaka alimwita Yakobo akamwongezea na kumthibitishia baraka hiyo. (Mwa 28:1-4) Kabla ya kufa, Yakobo aliwabariki wana wawili wa kwanza wa Yosefu, kisha akawabariki watoto wake mwenyewe. (Mwa 48:9, 20; 49:1-28; Ebr 11:21) Vivyo hivyo, Musa alibariki taifa lote la Israeli kabla ya kifo chake. (Kum 33:1) Katika visa hivyo vyote matokeo yanathibitisha kwamba walitoa unabii. Katika visa fulani, wale waliokuwa wakitoa baraka hizo, waliweka mkono juu ya kichwa cha yule aliyekuwa akibarikiwa.—Mwa 48:13, 14.

MACHI 30–APRILI 5

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 29-30

“Yakobo Anaoa”

it-2 341 ¶3

Ndoa

Sherehe. Ingawa harusi haikuwa na sherehe rasmi, kwa ujumla harusi katika taifa la Israeli zilikuwa pindi zenye shangwe. Siku ya harusi, bibi-harusi alifanya maandalizi mengi kwa ajili ya harusi akiwa nyumbani. Kwanza alioga na kujipaka mafuta yenye marashi. (Linganisha Ru 3:3; Eze 23:40) Kwa kutegemea hali yake ya kiuchumi, alivalia mavazi ya kifuani na joho jeupe ambalo lilipambwa kwa mishono mingi yenye kupendeza. Nyakati nyingine, bibi-harusi alisaidiwa na wanawake wengine alipokuwa akivaa mavazi hayo. (Yer 2:32; Ufu 19:7, 8; Zb 45:13, 14) Ikiwa alikuwa na uwezo, alijipamba kwa vito na mapambo mengine (Isa 49:18; 61:10; Ufu 21:2), kisha akajifunika kwa vazi jepesi, aina ya shela, ambalo lilimfunika kutoka kichwani hadi kwenye miguu. (Isa 3:19, 23) Hilo linatusaidia kuelewa kwa nini ilikuwa rahisi sana kwa Labani kumdanganya Yakobo hivi kwamba Yakobo hakujua kwamba Labani alikuwa akimpa Lea badala ya Raheli. (Mwa 29:23, 25) Rebeka alijifunika kichwa kwa shela alipokuwa karibu kukutana na Isaka. (Mwa 24:65) Kwa kufanya hivyo, bibi-harusi alikuwa akitoa ishara ya kujitiisha, au kutambua mamlaka ya bwana-harusi.—1Ko 11:5, 10.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 50

Kufanywa Kuwa Mwana

Raheli na Lea waliona watoto wa Yakobo ambao walizaliwa na vijakazi wao kuwa watoto wao wenyewe, ‘waliozaliwa kwenye magoti yao.’ (Mwa 30:3-8, 12, 13, 24) Watoto hao walipata urithi pamoja na wale waliozaliwa na wake halali wa Yakobo. Walikuwa watoto wa Yakobo kwa njia ya asili, na kwa kuwa vijakazi hao walikuwa mali ya wake zake, Raheli na Lea walikuwa na haki ya kuwaona watoto hao kuwa mali yao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki