Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr20 Februari kur. 1-4
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
  • Vichwa vidogo
  • FEBRUARI 3-9
  • FEBRUARI 10-16
  • FEBRUARI 24–MACHI 1
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
mwbr20 Februari kur. 1-4

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

FEBRUARI 3-9

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 12-14

“Agano Linalokuhusu”

it-1 522 ¶4

Agano

Agano Pamoja na Abrahamu. Inaelekea agano pamoja na Abrahamu lilianza kufanya kazi wakati Abramu (Abrahamu) alipovuka Efrati akiwa njiani kwenda Kanaani. Agano la Sheria lilifanywa miaka 430 baadaye. (Gal 3:17) Yehova alikuwa amezungumza na Abrahamu alipokuwa akiishi Mesopotamia, katika Uru la Wakaldayo, akamwambia asafiri kwenda kwenye nchi ambayo Mungu angemwonyesha. (Mdo 7:2, 3; Mwa 11:31; 12:1-3) Kutoka 12:40, 41 (LXX) kinatuambia kwamba kwenye mwisho wa miaka 430 ya kukaa Misri na katika nchi ya Kanaani, “siku hiyohiyo” Israeli, ambao walikuwa wamekuwa katika utumwa Misri, wakatoka. Siku waliyokombolewa kutoka Misri ilikuwa Nisani 14, 1513 K.W.K., tarehe ya Pasaka. (Kut 12:2, 6, 7) Inaelekea jambo hilo ni kama linaonyesha kwamba Abrahamu alivuka Mto Efrati kuelekea Kanaani mnamo Nisani 14, 1943 K.W.K., na kwa wazi ni wakati huo ambapo agano pamoja na Abrahamu lilianza kufanya kazi. Mungu alimtokea Abrahamu tena baada ya yeye kuwa amesafiri na kuingia Kanaani hadi Shekemu na kuifafanua zaidi ahadi hiyo, akisema, “Nitaupa uzao wako nchi hii,” hivyo akaonyesha uhusiano wa agano hili pamoja na ile ahadi katika Edeni, na kufunua kwamba ule “uzao” ungepitia njia ya kibinadamu, yaani, ungepitia nasaba ya kibinadamu. (Mwa 12:4-7) Yehova alifafanua mengi zaidi baadaye, kama ambavyo imeandikwa kwenye Mwanzo 13:14-17; 15:18; 17:2-8, 19; 22:15-18.

w89 7/1 3 ¶4

Kwa Nini Inakupasa Ujue Ukweli Juu ya Abrahamu

Hiyo ni ahadi ya kushangaza sana, na Abrahamu aliisikia ikitamkwa katika angalau pindi nyingine mbili. (Mwanzo 18:18; 22:18) Ili kuitimiza, Mungu hata atawafufua kutoka kwa wafu wawakilishi wa jamaa ambazo zimekufa zikamalizika kabisa. Maisha yatakuwa baraka kweli kweli kwa wafufuliwa hao, kwa kuwa wengi wao watarudi kwenye hali ya kidunia inayofanana na Paradiso ambayo mwanadamu alipoteza hapo awali. Baada ya hapo, watafunzwa jinsi ya kupata baraka ya uhai wa milele.—Mwanzo 2:8, 9, 15-17; 3:17-23.

it-2 213 ¶3

Sheria

Kulingana na uthibitisho wa kihistoria, wasomi fulani wanaamini kwamba wakati wa kuuza ardhi, mnunuzi angeonyeshwa ardhi kutoka umbali fulani, na kuonyeshwa mipaka yake. Ikiwa mnunuzi angesema “nimeona,” ingemaanisha amekubali kisheria. Yehova alipomwahidi Abrahamu kwamba atampa nchi ya Kanaani, Abrahamu aliambiwa kwanza aangalie pande zote nne. Abrahamu hakusema, “nimeona,” huenda kwa sababu Mungu alimwambia kwamba angeupa uzao wa Abrahamu Nchi ya Ahadi baadaye. (Mwa 13:14, 15) Ikiwa maoni yaliyotolewa hapo juu ni sahihi, basi Musa, akiwa mwakilishi wa kisheria wa taifa la Israeli, aliambiwa ‘aone’ nchi, jambo ambalo lingemaanisha kwamba nchi hiyo sasa ilikuwa mali ya Israeli kisheria, na wangeimiliki chini ya uongozi wa Yoshua. (Kum 3:27, 28; 34:4; ona pia maneno ambayo Shetani alimwambia Yesu katika Mt 4:8.) Tendo lingine ambalo inaonekana lilikuwa na maana hiyohiyo ya kisheria ni: kutembea katika nchi na kuivuka au kuingia ndani yake ili kuimiliki. (Mwa 13:17; 28:13) Kwenye hati fulani za kale, idadi ya miti katika shamba ilitajwa kwenye hati ya ununuzi.—Linganisha na Mwa 23:17, 18.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-2 683 ¶1

Kuhani

Melkizedeki mfalme wa Salemu alikuwa kuhani (ko·henʹ) asiye wa kawaida. Biblia haitaji ukoo wake, kuzaliwa kwake, wala kifo chake. Ukuhani wake haukutegemea urithi, na hakuwa na mtangulizi wala mrithi. Melkizedeki alikuwa na cheo cha kuhani na mfalme. Ukuhani wake ulikuwa mkuu kuliko ukuhani wa Lawi, kwa sababu Lawi, alimlipa Melkizedeki sehemu ya kumi, kwa kuwa bado alikuwa ndani ya Abrahamu wakati ambapo Abrahamu alimpa Melkizedeki sehemu ya kumi kisha Melkizedeki akambariki. (Mwa 14:18-20; Ebr 7:4-10) Katika hayo yote, Melkizedeki alimwakilisha kinabii Yesu Kristo, “kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki.”—Ebr 7:17.

FEBRUARI 10-16

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 15-17

“Kwa Nini Yehova Alibadilisha Majina ya Abramu na Sarai?”

it-1 817

Kosa, Kutafuta Makosa

Kwa upande mwingine, mara nyingi njia na matendo ya mwanadamu ni yenye makosa. Tumerithi dhambi na makosa kutoka kwa Adamu. (Ro 5:12; Zb 51:5) Lakini Yehova, ambaye hana kosa, “anajua vema umbo letu, akikumbuka kwamba sisi ni mavumbi,” na ni mwenye rehema. (Zb 103:13, 14) Alimwona Noa mwaminifu “kuwa mtu asiye na kosa miongoni mwa watu wa siku zake.” (Mwa 6:9) Alimwamuru hivi Abrahamu, “Tembea mbele zangu na ujithibitishe mwenyewe kuwa bila kosa.” (Mwa 17:1) Ingawa wanaume hao wawili hawakuwa wakamilifu na walikufa, Yehova aliwaona kuwa wasio na kosa, kwa kuwa yeye “huona ndani ya moyo.” (1Sa 16:7; linganisha na 2Fa 20:3; 2Nya 16:9.) Aliwaagiza hivi Waisraeli: “Mnapaswa kudhihirisha kwamba hamna lawama mbele za Yehova Mungu wenu.” (Kum 18:13; 2Sa 22:24) Alimtoa Mwana wake ambaye hakuwa na hatia (Ebr 7:26) awe dhabihu ya ukombozi, na kwa msingi huo anaweza kuwaita wale wanaoonyesha imani na utii kuwa “waadilifu,” au wasio na kosa, na wakati uleule kudumisha msimamo wake wa kuwa Mwamuzi mwadilifu asiye na kosa.—Ro 3:25, 26; tazama UTIMILIFU; UKAMILIFU.

it-1 31 ¶1

Abrahamu

Muda ukapita. Sasa walikuwa wameishi Kanaani kwa karibu miaka kumi, ingawa hivyo Sara aliendelea kuwa tasa. Baadaye alipendekeza kwamba kijakazi wake Mmisri aliyeitwa Hagari azae mtoto kwa ajili yake. Abrahamu akakubali. Basi mwaka wa 1932 K.W.K., Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 86, Ishmaeli akazaliwa. (Mwa 16:3, 15, 16) Muda ukazidi kupita. Mwaka wa 1919 K.W.K., Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 99, ili kuthibitisha au kutia muhuri uhusiano wa kipekee wenye agano kati yake na Abrahamu, Yehova aliagiza wanaume wote katika nyumba ya Abrahamu watahiriwe. Wakati huohuo Yehova akabadilisha jina lake kutoka Abramu na kuwa Abrahamu, “kwa sababu nitakufanya kuwa baba wa mataifa mengi.” (Mwa 17:5, 9-27; Ro 4:11) Muda mfupi baadaye, malaika watatu waliojivika miili ya kibinadamu, ambao Abrahamu aliwakaribisha kwa ukarimu katika jina la Yehova, waliahidi kwamba Sara mwenyewe angepata mimba na kumzaa mwana, ndiyo, ndani ya mwaka uliofuata!—Mwa 18:1-15.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 460-461

Kronolojia

Yehova alimwambia Abramu (Abrahamu): “Ujue kwa hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si yao na kwamba watu wa nchi hiyo watawafanya kuwa watumwa na kuwatesa kwa miaka 400.” (Mwa 15:13; tazama pia Mdo 7:6, 7.) Jambo hilo lilisemwa kabla Isaka, “uzao” ulioahidiwa, hajazaliwa. Mwaka wa 1932 K.W.K. kijakazi Mmisri, Hagari, alimzalia Abramu mwana aliyeitwa Ishmael, naye Isaka akazaliwa mwaka wa 1918 K.W.K. (Mwa 16:16; 21:5) Tukihesabu miaka 400 kurudi nyuma tangu Waisraeli walipotoka Misri, kipindi cha ‘kuteseka’ (Mwa 15:14), tunafika mwaka wa 1913 K.W.K., wakati ambapo Isaka alikuwa na umri wa miaka mitano hivi. Inaonekana kwamba Isaka alikuwa ameacha kunyonya na tayari alikuwa “mkaaji mgeni” katika nchi ya kigeni, hivyo alijionea mwanzo wa kuteseka kulikotabiriwa kutokana na jinsi Ishmaeli alivyokuwa “akimdhihaki,” wakati huo Ishmaeli akiwa na umri wa miaka 19. (Mwa 21:8, 9) Ingawa nyakati hizi huenda tukaona kitendo cha Ishmaeli cha kumdhihaka Isaka kuwa kisicho na madhara yoyote, nyakati hizo hali ilikuwa tofauti. Hilo linaonekana kupitia jinsi Sara alivyotenda na jinsi Mungu alivyokubaliana naye aliposisitiza kwamba Hagari na mwanaye Ishmaeli wafukuzwe. (Mwa 21:10-13) Jambo hilo liliandikwa kwa undani katika Biblia ili kuonyesha mwanzo wa kipindi kilichotabiriwa cha miaka 400 ya kuteseka ambacho kingekwisha baada ya Waisraeli kutoka Misri.—Gal 4:29.

it-1 778 ¶4

Kutoka Misri

“Katika kizazi cha nne.” Tunapaswa kukumbuka Yehova alimwambia Abrahamu kwamba katika kizazi chake cha nne wazao wake wangerudi Kanaani. (Mwa 15:16) Kwa miaka yote 430 tangu agano pamoja na Abrahamu lilipoanza kufanya kazi hadi Waisraeli walipotoka Misri, kulikuwa na zaidi ya vizazi vinne, hata tukizingatia kwamba wakati huo watu waliishi kwa muda mrefu zaidi, kama rekodi zinavyoonyesha. Lakini Waisraeli waliishi Misri kwa miaka 215 tu. Vizazi vyao vinne tangu walipoingia Misri vinaweza kuhesabiwa kwa njia hii, tukitumia mfano wa kabila moja la Israeli, kabila la Lawi: (1) Lawi, (2) Kohathi, (3) Amramu, na (4) Musa.—Kut 6:16, 18, 20.

Kutafuta Hazina za Kiroho

w88 5/15 23 ¶5-6

Je! Ye Yote Ameona Mungu?

Sasa inawezekana kuelewa ni kwa nini Abrahamu alielekeza maneno kwa mnenaji wa Mungu wa kimalaika aliyejivika mwili kama kwamba alikuwa akiongea na Yehova Mungu mwenyewe. Kwa kuwa malaika huyu alinena yale yale kabisa ambayo Mungu alitaka amwambie Abrahamu, na alikuwa hapo akimwakilisha Yeye binafsi, maandishi ya Kibiblia yangeweza kusema kwamba “Yehova mwenyewe alitokea kwake.”—Mwanzo 18:1, NW.

Kumbuka kwamba mnenaji wa Mungu wa kimalaika angeweza kupitisha ujumbe Wake mbalimbali sawasawa kabisa na vile simu au redio inavyoweza kupitisha maneno yetu kwa mtu mwingine. Kwa sababu hiyo, inaweza kueleweka ni jinsi gani Abrahamu, Musa, Manoa, na wengine wangeweza kunena pamoja na malaika aliyejivika mwili kama kwamba walikuwa wanaongea na Mungu. Ingawa hao watu mmoja mmoja waliweza malaika hawa na utukufu wa Yehova ulioonekana kupitia kwao, wao hawakuweza kuona Mungu. Basi, hiyo haipinganishi kwa vyo vyote ile taarifa ya mtume Yohana:”Hakuna mwanadamu ameona Mungu wakati wo wote.” (Yohana 1:18, NW) Kile ambacho wanaume hawa waliona kilikuwa wawakilishi wa kimalaika wala si Mungu mwenyewe.

FEBRUARI 24–MACHI 1

Kutafuta Hazina za Kiroho

w89 7/1 20 ¶9

Abrahamu—Kielelezo kwa Wote Wanaotafuta Urafiki wa Mungu

9 Abramu aliitikia kwa kitendo kingine cha imani. Kama vile usimulizi unavyosema: “Huko akamjengea madhabahu Bwana [Yehova, NW].” (Mwanzo 12:7) Inaelekea kwamba kwa kufanya hivi alitoa pia dhabihu ya mnyama, kwa maana neno la Kiebrania la “madhabahu” linamaanisha “mahali pa dhabihu.” Baadaye, Abramu alirudia vitendo hivi vya imani katika sehemu nyingine za bara hilo. Kwa kuongezea hilo, yeye ‘aliitia jina la Yehova.’ (Mwanzo 12:8; 13:18; 21:33, NW) Kifungu cha Kiebrania kinachosema ‘kuitia jina’ kinamaanisha pia ‘kujulisha wazi (kuhubiri) jina hilo.’ Watu wa nyumba ya Abramu na pia Wakanaani ni lazima wawe walimsikia akilijulisha wazi jina la Mungu wake, Yehova, kwa ujasiri. (Mwanzo 14:22-24) Vilevile, wote wanaotafuta urafiki wa Mungu leo ni lazima waliitie jina lake kwa imani. Hii ingehusisha ndani kushiriki kuhubiri peupe, ‘sikuzote wakimtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, tunda la midomo linalofanyiza tangazo la peupe kwa jina lake.’—Waebrania 13:15; Warumi 10:10, NW.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki