Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr22 Mei kur. 1-4
  • Marejeo ya Daftari la “Mkutano wa Huduma na Maisha”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la “Mkutano wa Huduma na Maisha”
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2022
  • Vichwa vidogo
  • MEI 2-8
  • MEI 16-22
  • MEI 30–JUNI 5
  • JUNI 6-12
  • JUNI 13-19
  • JUNI 20-26
  • JUNI 27–JULAI 3
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2022
mwbr22 Mei kur. 1-4

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

MEI 2-8

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 1 SAMWELI 27-29

“Mbinu ya Vita ya Daudi”

it-1 41

Akishi

Mara mbili wakati ambapo Daudi alikuwa akimkimbia Sauli, alikimbilia kwenye eneo la Mfalme Akishi. Pindi ya kwanza, aliposhukiwa kuwa adui, Daudi alijifanya kuwa mwenda wazima, na hivyo Akishi akamwacha akiamini kwamba ni mpumbavu asiyeweza kumdhuru yeyote. (1Sa 21:10-15; Zb 34:Maelezo ya utangulizi; 56:Maelezo ya utangulizi) Pindi ya pili, Daudi aliandamana na mashujaa 600 wa vita pamoja na familia zao, kwa hiyo, Akishi akawaagiza waishi Siklagi. Katika muda wa mwaka mmoja na miezi minne ambao waliishi huko, Akishi aliamini kwamba Daudi na wanaume wake walikuwa wakishambulia miji ya Yudea, lakini kwa kweli Daudi alikuwa akiwashambulia Wageshuri, Wagirzi, na Waamaleki. (1Sa 27:1-12) Daudi alifaulu kumpumbaza Akishi sana hivi kwamba Wafilisti walipokuwa wakipanga kumshambulia Mfalme Sauli, Akishi alimweka Daudi kuwa mlinzi wake wa kibinafsi. Ni baada tu ya watawala wa Wafilisti kulalamika, ndipo Daudi na wanaume wake walipoagizwa warudi Siklagi. (1Sa 28:2; 29:1-11) Daudi alipokuwa mfalme na kupigana dhidi ya Gathi, inaonekana kwamba Akishi hakuuawa. Aliendelea kuishi hadi wakati wa utawala wa Sulemani.​—1Fa 2:39-41; ona GATHI.

it-2 245 ¶6

Uwongo

Ingawa Biblia inashutumu kusema uwongo uliokusudiwa kuwadhuru wengine, hilo halimaanishi kwamba mtu anawajibika kufunua habari za kweli kwa watu ambao hawana haki ya kupokea habari hizo. Yesu Kristo alisema hivi: “Msiwape mbwa kitu kitakatifu, wala msiwatupie nguruwe lulu zenu, wasije wakazikanyaga-kanyaga chini ya miguu yao, kisha wageuke na kuwararua ninyi.” (Mt 7:6) Hiyo ndiyo sababu pindi fulani Yesu alikataa kutoa habari zote au majibu ya moja kwa moja kwa maswali ambayo yangemletea madhara bila sababu. (Mt 15:1-6; 21:23-27; Yoh 7:3-10) Ni wazi kwamba tunapaswa kuwa na maoni hayohayo kumhusu Abrahamu, Isaka, Rahabu, na Elisha walipowaelekeza vibaya au kuepuka kuwapa habari zote watu ambao hawakuwa waabudu wa Yehova.​—Mwa 12:10-19; sura ya 20; 26:1-10; Yos 2:1-6; Yak 2:25; 2Fa 6:11-23.

MEI 16-22

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 1-3

Hazina za Kiroho

it-1 369 ¶2

Ndugu

Neno “ndugu” hutumiwa pia kurejelea watu walioungana ili kutimiza jambo fulani na walio na malengo na makusudi yaleyale. Kwa mfano, Mfalme Hiramu wa Tiro alimwita Mfalme Sulemani ndugu yake, si kwa sababu walikuwa na cheo na mamlaka yaleyale bali pia kwa sababu walikuwa na mapendezi yaleyale ya kuandaa mbao na vitu vingine kwa ajili ya hekalu. (1Fa 9:13; 5:1-12) Daudi aliandika hivi: “Tazama! Jinsi ilivyo vema na jinsi inavyopendeza ndugu kukaa pamoja kwa umoja!” Daudi alimaanisha kwamba si uhusiano wa damu peke yake unaotokeza amani na umoja miongoni mwa ndugu wa kimwili. (Zb 133:1) Kwa kweli, Daudi alimwita Yonathani ndugu yake, si kwa sababu walizaliwa na wazazi walewale, bali kwa sababu walipenda na kuvutiwa na mambo yaleyale. (2Sa 1:26) Marafiki walio na utu na mwelekeo unaofanana, hata kuhusu mambo mabaya, wanaitwa kwa kufaa kuwa ndugu.​—Met 18:9.

MEI 30–JUNI 5

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 7-8

Hazina za Kiroho

it-2 206 ¶2

Siku za Mwisho

Unabii wa Balaamu. Kabla ya Waisraeli kuingia Nchi ya Ahadi, nabii Balaamu alimwambia Mfalme Balaki wa Moabu hivi: “Njoo nikwambie mambo ambayo watu hawa [Waisraeli] watawatendea watu wako [siku za mwisho, Union Version]. . . . Nyota itatoka kwa Yakobo, na fimbo ya ufalme itainuka katika Israeli. Naye hakika atapasua paji la uso la Moabu na fuvu la kichwa la wana wote wa vurugu.” (Hes 24:14-17) Katika utimizo wa kwanza wa unabii huo, “nyota” hiyo ilithibitika kuwa Mfalme Daudi, aliyewatiisha Wamoabu. (2Sa 8:2) Hivyo, ni wazi kwamba katika utimizo wa unabii huo, “siku za mwisho” zilianza wakati ambapo Daudi aliwekwa kuwa mfalme. Kwa kuwa Daudi alitangulia kumwakilisha Yesu akiwa Mfalme wa Kimasihi, unabii huo ungemhusu Yesu pia wakati ambapo angewatiisha maadui wake.​—Isa 9:7; Zb 2:8, 9.

JUNI 6-12

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 9-10

Hazina za Kiroho

it-1 266

Ndevu

Miongoni mwa watu wengi walioishi katika maeneo ya Mashariki, kutia ndani Waisraeli, ndevu zilionwa kuwa uthibitisho wa heshima ya kiume. Sheria ya Mungu iliwakataza Waisraeli wasinyoe “masharafa,” nywele zilizo katikati ya sikio na jicho, na ncha za ndevu zao. (Law 19:27; 21:5) Ni wazi kwamba sheria hiyo ilitolewa kwa sababu ilikuwa desturi ya dini fulani za kipagani kufanya hivyo.

JUNI 13-19

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 11-12

Hazina za Kiroho

it-1 590 ¶1

Daudi

Hata hivyo, Yehova alikuwa akitazama, naye akafichua jambo hilo lote lenye kuchukiza. Ikiwa Yehova angeruhusu kesi hiyo kumhusu Daudi na Bath-sheba ishughulikiwe na waamuzi wa kibinadamu chini ya Sheria ya Musa, wakosaji wote wawili wangeuawa, na bila shaka, mtoto ambaye hakuwa amezaliwa aliyetokezwa na uzinzi wao angekufa pamoja na mama yake. (Kum 5:18; 22:22) Hata hivyo, Yehova alishughulikia kesi hiyo mwenyewe na kumwonyesha Daudi rehema kwa sababu ya agano la Ufalme (2Sa 7:11-16), bila shaka pia kwa sababu Daudi mwenyewe alikuwa ameonyesha rehema (1Sa 24:4-7; linganisha Yak 2:13), na kwa sababu Mungu aliona watenda-dhambi hao wameonyesha toba. (Zb 51:1-4) Lakini haimaanishi kwamba hawakupata adhabu. Kupitia nabii Nathani, Yehova alitangaza hivi: “Tazama, ninakuletea msiba kutoka katika nyumba yako mwenyewe.”​—2Sa 12:1-12.

JUNI 20-26

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 13-14

“Ubinafsi wa Amnoni Ulitokeza Msiba”

it-1 32

Absalomu

Uuaji wa Amnoni. Urembo wa Tamari, dada ya Absalomu, ulimfanya Amnoni aliyekuwa ndugu-nusu yake, amtamani. Amnoni alijifanya kuwa mgonjwa na akaomba Tamari atumwe nyumbani kwake ili ampikie, na baada ya hapo akambaka. Upendo wa kimahaba ambao Amnoni alikuwa nao kumwelekea Tamari ulibadilika kuwa chuki mbaya sana hivi kwamba akaagiza Tamari atupwe nje barabarani. Tamari alirarua joho lake lenye mistari lililomtambulisha kuwa binti ya mfalme ambaye ni bikira na kutia majivu kichwani mwake, kisha akakutana na Absalomu. Upesi Absalomu akachunguza hali hiyo na kumshuku Amnoni, kuonyesha kwamba tayari alitambua ndugu-nusu yake alikuwa na tamaa hiyo kumwelekea. Hata hivyo, Absalomu alimwagiza dada yake asimshtaki, naye akampeleka akaishi nyumbani kwake.​—2Sa 13:1-20.

it-1 33 ¶1

Absalomu

Miaka miwili ikapita. Wakati wa kukata manyoya ya kondoo ukafika, ambayo ni pindi ya kusherehekea. Absalomu akaandaa karamu kule Baal-hasori kilomita 22 hivi Kaskazini-Mashariki ya Yerusalemu, naye akawaalika wana wote wa mfalme na Daudi mwenyewe. Baba yake aliposema kwamba hataweza kuhudhuria, Absalomu alimsihi sana amruhusu Amnoni, mwana wake wa kwanza, ahudhurie kwa niaba yake. (Met 10:18) Wakati wa karamu, Amnoni ‘alipokuwa amechangamka kwa sababu ya divai,’ Absalomu aliwaagiza watumishi wake wamuue. Wana wale wengine walikimbia kurudi Yerusalemu, naye Absalomu akakimbilia uhamishoni kwa babu yake wa Siria katika ufalme wa Geshuri uliokuwa Mashariki ya Bahari ya Galilaya. (2Sa 13:23-38) “Upanga” uliokuwa umetabiriwa na nabii Nathani sasa ulikuwa umeingia “nyumbani” mwa Daudi na ungeendelea kuwa hapo maisha yake yote.​—2Sa 12:10.

JUNI 27–JULAI 3

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 15-17

“Absalomu Aliasi kwa Sababu ya Kiburi”

it-1 860

Mtu Aliyekimbia Mbele ya Gari

Ilikuwa desturi ya maeneo ya Mashariki kuwa na watu waliokimbia mbele ya magari ya wafalme ili kutayarisha na kutangaza kwamba mfalme alikuwa njiani na ambao walimsaidia kwa ujumla. (1Sa 8:11) Absalomu na Adoniya, wakiiga utukufu huo wa kifalme na wakijaribu kuongezea heshima na kujaribu kuonyesha kwamba uasi wao ulikubaliwa, waliwaweka watu 50 waliokimbia mbele ya magari yao wenyewe.​—2Sa 15:1; 1Fa 1:5; ona WAKIMBIAJI.

it-1 1083-1084

Hebroni

Miaka kadhaa baadaye, Absalomu mwana wa Daudi alirudi Hebroni na kujaribu kumnyang’anya baba yake ufalme, lakini hakufanikiwa. (2Sa 15:7-10) Huenda Absalomu alichagua kuanzia shughuli zake kunyakua utawala huko Hebroni kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria wa jiji hilo. Jiji la Hebroni lilikuwa mji mkuu wa awali wa Yuda, na pia ndilo jiji ambalo Absalomu alilelewa. Baadaye, Mfalme Rehoboamu, mjukuu wa Daudi, alijenga upya jiji la Hebroni. (2Nya 11:5-10) Baada ya Wababiloni kuangamiza Yuda na wahamishwa Wayahudi kurudi, baadhi ya Wayahudi hao waliorudi waliishi huko Hebroni (Kiriath-arba).​—Ne 11:25.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki