WIMBO NA. 139
Wazia Wakati Vitu Vyote Vitakuwa Vipya
Makala Iliyochapishwa
	- 1. Hebu waza, mimi nawe; - Sote katika dunia mpya. - Fikiria Paradiso, - Amani na uhuru tele, - Na uovu wote kwisha. - Utawala wake Yehova, - Utaitawala dunia yote. - Kwa moyo wote sote - tutamwimbia: - (KORASI) - “Yehova Mungu twakushukuru. - Umefanya vyote viwe vipya. - Tunachochewa na ukarimu wako; - Wastahili heshima na utukufu.” 
- 2. Hebu waza, mimi nawe; - Tukiwa katika Paradiso. - Tuonayo, kusikia - Hayatatutia uoga. - Yote kweli, katabiri; - Hema lake kalitandaza, - Afufue walio kaburini; - Tumwimbie Yehova - sifa pamoja: - (KORASI) - “Yehova Mungu twakushukuru. - Umefanya vyote viwe vipya. - Tunachochewa na ukarimu wako; - Wastahili heshima na utukufu.” 
(Ona pia Zab. 37:10, 11; Isa. 65:17; Yoh. 5:28; 2 Pet. 3:13.)