WIMBO NA. 79
Wafundishe Kusimama Imara
Makala Iliyochapishwa
1. Ni shangwe kufunza kondoo
Mapenzi ya Yehova.
Wawe na nguvu za kiroho.
Imara wasimame.
(KORASI)
Ee Yehova, twakuomba
Twakusihi uwatunze
Katika jina la Yesu: Twakuomba
Waweze kuwa imara.
2. Walipopata majaribu
Uliwaimarisha.
Nasi tukawategemeza
Ili wasonge mbele.
(KORASI)
Ee Yehova, twakuomba
Twakusihi uwatunze
Katika jina la Yesu: Twakuomba
Waweze kuwa imara.
3. Twasali wawe na imani
Kwako Yehova Mungu.
Watii na kuvumilia.
Pigano walishinde.
(KORASI)
Ee Yehova, twakuomba
Twakusihi uwatunze
Katika jina la Yesu: Twakuomba
Waweze kuwa imara.
(Ona pia Luka 6:48; Mdo. 5:42; Flp. 4:1.)