WIMBO NA. 82
“Acheni Nuru Yenu Iangaze”
Makala Iliyochapishwa
1. Yesu aamuru,
Twangaze nuru.
Bila ubaguzi,
Wote waone.
Neno lake Mungu,
Liwape nuru.
Tufundishapo Neno,
Twangaze nuru.
2. Tunapotangaza
Habari njema.
Neno lake Mungu,
Latuongoza.
Linawapatia,
Wote nafasi.
Wachague wenyewe,
Toka moyoni.
3. Tufanyapo mema,
Nuru yang’aa.
Fundisho la Bwana,
Tunalipamba.
Tunampendeza,
Yehova Mungu.
Tuangaze daima,
Nuru ya kweli.
(Ona pia Zab. 119:130; Mt. 5:14, 15, 45; Kol. 4:6.)