WIMBO NA. 42
Sala ya Mtumishi wa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Baba Yetu, Mwenye Enzi Kuu,
Jina lako litakaswe milele;
Mapenzi yako yatimizwe.
Tunakuomba, Ufalme uje.
Utakapoagiza,
Baraka tuzione.
2. Twashukuru kwa baraka zako,
Unatupa zawadi nyingi njema.
Chanzo cha uhai na nuru,
Watupa hekima, ufahamu.
Twashukuru daima,
Twakusifu Yehova.
3. Ulimwengu una dhiki nyingi.
Tufariji tunakutegemea.
Tunakutupia mizigo.
Tupe nguvu za kusonga mbele.
Tufanye upendayo,
Tutimize nadhiri.
(Ona pia Zab. 36:9; 50:14; Yoh 16:33; Yak. 1:5.)