WIMBO NA. 1
Sifa za Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Mungu, Mwenye Uwezo,
Muumba wetu, mwenye enzi kuu.
Uumbaji wakusifu wewe;
Unaonyesha nguvu zako.
2. Hukumu zako zote za haki.
Uadilifu, unatufundisha.
Neno lako tunapolisoma,
Hekima yako, twaiona.
3. Upendo wako, ni sifa kuu.
Zawadi zako, hazina kifani.
Jina lako, nazo sifa zako,
Twazitangaza kwa furaha.
(Ona pia Zab. 36:9; 145:6-13; Mhu. 3:14; Yak. 1:17.)