Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
Austria Yasimama Imara 66
Je! imani yako ya Kikristo inaweza kustahimili yale manyimo makali ya kambi za mateso za Nazi? Mashahidi wa Yehova katika Austria walisimama imara usoni pa mnyanyaso wa ukatili kama huo mikononi mwa waonezi wao. Soma ujue jinsi walivyovumilia.
Barbados Yavuna Mbegu za Ufalme 148
Miongoni mwa vile visiwa vyenye kulowa jua vya Karibea, Barbados hutoa ushuhuda si wa kupanda mbegu za Ufalme tu bali pia wa kuvuna tunda la kiroho. Jifunze jinsi mbegu za ujumbe wa Ufalme zilivyoenea pia kwenye visiwa jirani.
Ekwedori Yakubali Ukweli 198
Likitagaa ikweta, Ekwedori ni bara la idadi ya watu wanaotofautiana sana kama vile wakulima wenye mavazi kidogo sana na wanabenki wenye suti za kufanyia biashara. Kwa miaka 53 iliyopita, baadhi ya Waekwedori hawa, wanaokusalimu kwa mkono na kutabasamu kwa haraka, wamekuwa na hamu nyingi ya kukubali ukweli wa Biblia. Vumbua sababu ni nini.