HOSEA YALIYOMO 1 Mke wa Hosea na watoto anaozaa (1-9) Yezreeli (4), Lo-ruhama (6), na Lo-ami (9) Tumaini la kurudishwa na kuwa na umoja (10, 11) 2 Waisraeli wasio waaminifu waadhibiwa (1-13) Wamrudia Yehova akiwa kama mume wao (14-23) “Utaniita mume Wangu” (16) 3 Hosea amkomboa mke wake mzinzi (1-3) Waisraeli watamrudia Yehova (4, 5) 4 Kesi ya Yehova dhidi ya Waisraeli (1-8) Watu hawamjui Mungu nchini (1) Waisraeli waabudu sanamu na kufanya ukahaba (9-19) Wapotoshwa na roho ya ukahaba (12) 5 Waefraimu na watu wa Yuda wahukumiwa (1-15) 6 Wasihiwa wamrudie Yehova (1-3) Upendo mshikamanifu usiodumu wa Waisraeli (4-6) Upendo mshikamanifu ni bora kuliko dhabihu (6) Mwenendo wa aibu wa Waisraeli (7-11) 7 Uovu wa Waefraimu (1-16) Hawataepuka wavu wa Mungu (12) 8 Matokeo ya kuabudu sanamu (1-14) Kupanda upepo, kuvuna kimbunga (7) Waisraeli wamemsahau Muumba wao (14) 9 Mungu awakataa Waefraimu kwa sababu ya dhambi zao (1-17) Wajiweka wakfu kwa mungu anayechukiza (10) 10 Waisraeli ni mzabibu ulioharibika, wataangamizwa (1-15) Kupanda na kuvuna (12, 13) 11 Mungu ampenda Israeli tangu utotoni (1-12) “Nikamwita mwanangu atoke Misri” (1) 12 Waefraimu wanapaswa kumrudia Yehova (1-14) Yakobo alishindana na Mungu (3) Yakobo alimlilia Mungu ili ambariki (4) 13 Waefraimu waabudu sanamu na kumsahau Yehova (1-16) “Ewe Kifo, yako wapi maumivu yako makali?” (14) 14 Wasihiwa wamrudie Yehova (1-3) Kutoa sifa ya midomo (2) Waisraeli waponywa, hawatakosa uaminifu tena (4-9)