Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 5/8 uku. 31
  • Mimi Sivuti Sigara!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mimi Sivuti Sigara!
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • “Mimi Sijafa”
    Amkeni!—2011
  • Kitabu Cha Biblia Namba 27—Maombolezo
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Maoni ya Kikristo Juu ya Kuvuta Sigareti
    Amkeni!—1990
  • Fadhili Huondoa Uchungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 5/8 uku. 31

Mimi Sivuti Sigara!

KICHWA hicho kilipewa wanafunzi wengi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya kuandika yaliyodhaminiwa na Shirika la Kitiba la Jimbo la Missouri (MSMA) huko Marekani. Karibu wanafunzi 675 kutoka katika shule 42 walishiriki katika mashindano hayo. Msichana mwenye umri wa miaka 12 anayeitwa Breanna ndiye aliyeshinda tuzo, na shairi lake lilichapishwa kwenye jarida Missouri Medicine la shirika la MSMA. Pia, Breanna alipata nafasi ya kusoma shairi lake mbele ya wahudhuriaji wa kusanyiko hilo la kila mwaka la MSMA. Kabla ya kufanya hivyo, Breanna aliwaambia wasikilizaji wake hivi:

“Mimi ni Shahidi wa Yehova, na mambo yote ya shairi langu yalitoka kwenye gazeti Amkeni! Ama kweli, wazo fulani la sehemu niipendayo sana ya shairi langu ilitoka kwenye jalada la gazeti hilo. Kuna picha ya fuvu la kichwa na sigara ikining’inia mdomoni mwake na inasema: ‘Kifo Chauzwa.’ Kwa miaka mingi gazeti Amkeni! limechapisha makala nyingi zinazohusu hatari ya kuvuta sigara.”

Mashahidi wa Yehova hawavuti sigara. Wanaamini kwamba kutumia kimakusudi vitu vinavyouchafua mwili ni kupuuza zawadi ya uhai na kutomheshimu Muumba. (Matendo 17:24, 25) Hivyo, wao hufuata shauri hili la Maandiko: “Acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.”—2 Wakorintho 7:1.

Kama Mashahidi wengine vijana, Breanna hujitahidi kuishi kulingana na viwango vya Biblia. Kwa kweli vijana hao wote huufurahisha moyo wa Muumba wao.—Methali 27:11.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Breanna (sasa akiwa na umri wa miaka 14) akishikilia shairi lake

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki