Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 8/11 uku. 21
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Unamna-Namna wa Viumbe Katika Amazoni
  • Mfadhaiko Kazini
  • Je, Kufikiria Kuhusu Michezo Huchochea Jeuri?
  • Je, Nicheze Michezo ya Kompyuta au ya Vidio?
    Amkeni!—1996
  • Je, Nicheze Michezo ya Kompyuta?
    Amkeni!—2008
  • Je, Kuna Hatari kwa Wachezaji?
    Amkeni!—2002
  • Nicheze Michezo ya Kompyuta?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 8/11 uku. 21

Kuutazama Ulimwengu

Uchunguzi uliofanywa nchini Kanada na Marekani wa bidhaa 5,296 zinazosemekana kuwa hazidhuru mazingira ulionyesha kwamba asilimia 95 ya bidhaa hizo “zinatoa madai ya uwongo kwamba hazidhuru mazingira.”—TIME, MAREKANI.

Walinda usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bangkok “walishuku sana” mizigo ya mwanamke mmoja walipoipitisha kwenye mashini ya kukagua mizigo. Maofisa hao walipofungua mfuko mmoja ili kuukagua, walipata mtoto wa simbamarara akiwa hai lakini alikuwa amedungwa sindano ya kulala.—HAZINA YA WANYAMA WA PORI ULIMWENGUNI, THAILAND.

Unamna-Namna wa Viumbe Katika Amazoni

Bonde la Mto Amazoni ni moja kati ya maeneo yenye unamna-namna mwingi zaidi wa viumbe ulimwenguni. Katika muda wa miaka kumi iliyopita, zaidi ya spishi 1,200 za mimea na wanyama, yaani, samaki, amfibia, reptilia, ndege, na mamalia, waligunduliwa huko na kuorodheshwa, inasema ripoti ya Hazina ya Wanyama wa Pori Ulimwenguni (WWF). Hilo linamaanisha kwamba kwa wastani, spishi mpya hugunduliwa katika eneo hilo la Amazoni kila baada ya siku tatu. “Idadi ya spishi mpya zinazogunduliwa inashangaza na hiyo haitii ndani vikundi vingi vya wadudu wanaogunduliwa,” anasema Sarah Hutchison, msimamizi wa WWF huko Brazili.

Mfadhaiko Kazini

Asilimia 20 ya Wafini wanasema kwamba kazi yao inaathiriwa kwa sababu wana tatizo la kukaza fikira na kusahau. Kulingana na ripoti moja ya Taasisi ya Afya ya Wafanyakazi ya Ufini, matatizo kama hayo yanazidi kuwaathiri wale walio na umri wa chini ya miaka 35, umri ambao ubongo unapaswa kuwa makini zaidi. Kati ya mambo ambayo yanasababisha hali hiyo ni kupokea habari nyingi kupita kiasi na kubadilika-badilika kwa mifumo ya kompyuta. “Wengi wanahisi kwamba wanapata habari nyingi sana hivi kwamba hawawezi kuchanganua ni habari gani muhimu kwa kazi yao,” anasema Profesa Kiti Müller. Gazeti Helsinki Times linasema: “Ikiwa mfadhaiko unaendelea kwa muda mrefu, ubongo huuzoea na huenda tusipate dalili zozote zinazoonyesha kwamba tuna mkazo kupita kiasi hadi tunapokuwa wagonjwa.”

Je, Kufikiria Kuhusu Michezo Huchochea Jeuri?

Mtu huendelea kuwa na hasira kwa muda gani baada ya kucheza mchezo wa video wenye jeuri? Watafiti fulani walipanga kwamba wanafunzi wa kiume na wa kike wacheze michezo ya video iliyokuwa na jeuri na isiyokuwa na jeuri kwa muda wa dakika 20. Baadaye, nusu ya watu katika kila kikundi waliambiwa wafikirie kuhusu mchezo waliocheza. Ripoti hiyo inasema kwamba “siku iliyofuata, wachezaji walishindana vikali na mtu wa kuwaziwa, na mshindi angemwadhibu mwenye kushindwa kwa kumpulizia kelele nyingi kwenye sikio kupitia vifaa vya kusikilizia vinavyowekwa masikioni.” Wanafunzi wa kiume waliofikiria kuhusu mchezo huo wenye jeuri walitenda kwa jeuri zaidi. Waanzilishi wa utafiti huo wanasema hivi, kama ilivyoripotiwa katika jarida Social Psychological and Personality Science: “Kwa kawaida, watu wanaocheza michezo yenye jeuri huicheza kwa zaidi ya dak[ika] 20 na huenda wana zoea la kufikiria kuhusu michezo hiyo.” Hakuna mabadiliko yoyote yaliyoonekana katika wanafunzi wa kike, kwa kuwa wao huchukia michezo ya video yenye jeuri.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki