Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 9/13 kur. 6-9
  • Ukweli Kuhusu Halloween

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukweli Kuhusu Halloween
  • Amkeni!—2013
  • Habari Zinazolingana
  • Chanzo cha Halloween Ni Nini?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Ukweli Kuhusu Sherehe Zinazopendwa
    Amkeni!—2001
  • Je, Sherehe Zinazopendwa Zinaweza Kudhuru?
    Amkeni!—2001
  • “Hatutaki Kusherehekea ‘Halloween!’”
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2013
g 9/13 kur. 6-9

HABARI KUU

Ukweli Kuhusu Halloween

Je, Halloween, au Mkesha wa Sikukuu ya Watakatifu Wote husherehekewa unakoishi? Nchini Marekani na Kanada, Halloween ni maarufu sana na husherehekewa Oktoba 31, kila mwaka. Hata hivyo, desturi kama zile zinazofanywa wakati wa Halloween zimeenea katika sehemu nyingine nyingi ulimwenguni pote. Katika sehemu fulani, kuna sikukuu ambazo ingawa zimepewa majina tofauti, zina kusudi lilelile kama Halloween: kuwasiliana na viumbe wa roho iwe ni kupitia roho za wafu, wachawi, na hata ibilisi na malaika wake waovu.—Ona sanduku “Sikukuu Zinazofanana na Halloween Ulimwenguni Pote.”

HUENDA wewe binafsi usiamini kwamba kuna viumbe wa roho wenye nguvu zisizo za kawaida. Huenda ukawa na maoni ya kwamba kushiriki katika sherehe ya Halloween na sherehe nyingine zinazofanana na hiyo ni njia ya kujifurahisha tu na ya kuwafundisha watoto wako kuwa wabunifu. Hata hivyo, watu wengi wanaona sikukuu hizo kuwa zenye madhara kwa sababu zifuatazo:

  1. Kitabu Encyclopedia of American Folklore (Ensaiklopedia ya Desturi za Wamarekani) kinasema: “Halloween inahusisha hasa kuwasiliana na viumbe wa roho, ambao wengi wao hutisha au kuogopesha.” (Ona sanduku “Historia ya Halloween.”) Vivyo hivyo, Halloween na sikukuu nyingine nyingi zina asili ya kipagani na huhusisha sana kuabudu mababu waliokufa. Hata leo, watu ulimwenguni pote hutumia siku hizo kuwasiliana na roho zinazosemekana kuwa za wafu.

  2. Ingawa Halloween huonwa kuwa sikukuu ya Wamarekani, kila mwaka idadi ya watu wanaoisherehekea katika nchi mbalimbali inazidi kuongezeka. Hata hivyo, watu wengi ambao wameanza kuisherehekea hivi karibuni hawajui kwamba ishara, mapambo, na desturi za Halloween, ambazo nyingi zinahusianishwa na viumbe wa roho wenye nguvu zisizo za kawaida na uchawi, zilitoka kwa wapagani.—Ona sanduku “Chanzo Chake Ni Nini?”

  3. Maelfu ya wafuasi wa dini ya kiuchawi inayoitwa Wiccan, ambao hufuata desturi za Waselti wa kale bado huita Halloween kwa jina lake la kale, yaani, Samhain, nao husema kwamba huo ndio usiku mtakatifu zaidi katika mwaka. Likimnukuu mtu anayedai kuwa mchawi, gazeti USA Today lilisema hivi: “Wakristo ‘hawatambui kwamba wanasherehekea sikukuu yetu pamoja nasi. . . . Tunafurahia jambo hilo.’”

  4. Sikukuu kama vile Halloween zinapingana na mafundisho ya Biblia. Biblia inaonya hivi: “Pasiwe mtu yeyote miongoni mwenu . . . apigaye ramli, wala mwaguzi, wala mpiga bao, wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu.”—Kumbukumbu la Torati 18:10, 11, Biblia Habari Njema; ona pia Mambo ya Walawi 19:31; Wagalatia 5:19-21.

[Picha katika ukurasa wa 9]

Familia zinaweza kuwa na wakati mzuri hata bila kujihusisha katika sikukuu zisizompendeza Mungu

Kwa sababu ya mambo yaliyozungumziwa katika makala hii, ni jambo la hekima kujua chanzo kisichofaa cha Halloween na sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo. Kujua mambo kwa undani kutakusaidia kujiunga na wengine wengi ambao hawasherehekei sikukuu hizo.

“Wakristo ‘hawatambui kwamba wanasherehekea sikukuu yetu pamoja nasi. . . . Tunafurahia jambo hilo.’”—Gazeti USA Today, likimnukuu mtu anayedai kuwa mchawi

SIKUKUU ZINAZOFANANA NA HALLOWEEN ULIMWENGUNI POTE

Kwa ujumla, Halloween huonwa kuwa sikukuu ya Wamarekani. Lakini sasa sikukuu hiyo inapendwa sana katika sehemu nyingi ulimwenguni. Isitoshe, kuna sikukuu nyingine zinazofanana na Halloween katika maana ya kwamba zinasherehekea kuwapo kwa viumbe wa roho na utendaji wao. Zifuatazo ni baadhi ya sikukuu maarufu zinazofanana na Halloween ambazo zinapatikana ulimwenguni pote.

  • Amerika Kaskazini - Siku ya Wafu

  • Amerika Kusini - Kawsasqanchis

  • Afrika - Dansi ya Egungun Aliyevalia Kinyago

  • Ulaya - Siku ya Wafu na sherehe nyingine tofauti-tofauti za Halloween

  • Asia - Sherehe ya Bon

CHANZO CHAKE NI NINI?

Vyanzo vya Baadhi ya Desturi na Ishara za Halloween

MAJINI YANAYONYONYA DAMU, WATU-MBWEHA, WACHAWI, MAITI ZINAZOTEMBEA: Tangu zamani viumbe hao wamehusianishwa na roho waovu.

PEREMENDE: Waselti wa kale walijaribu kuwatuliza roho waovu kwa kuwapa peremende. Baadaye, kanisa liliwatia watu moyo waende nyumba kwa nyumba Mkesha wa Siku ya Watakatifu Wote ili kuwaombea waliokufa na kupewa chakula kama malipo. Mwishowe hiyo ikaja kuwa desturi ya Halloween, watu walienda nyumba kwa nyumba wakiomba peremende na kuwatisha watu wasiowapa peremende.

MAVAZI: Waselti walivaa vinyago ili roho waovu wadhani kwamba wao ni roho na hivyo wasiwadhuru. Kanisa liliingiza desturi za kipagani katika sherehe za Siku ya Wafu na Siku ya Watakatifu Wote. Baadaye, waadhimishaji walienda nyumba kwa nyumba wakiwa wamevalia kama watakatifu, malaika, na mashetani.

MABOGA: Aina fulani ya boga linaloitwa tanipu lilichongwa na kutiwa mshumaa ili kufukuza roho waovu. Watu fulani walisema kwamba mshumaa huo uliwakilisha nafsi zilizokuwa zimezuiliwa toharani. Baadaye, watu walianza kutumia maboga ya kawaida.

HISTORIA YA HALLOWEEN

KARNE YA 5 K.W.K.

Waselti wanaadhimisha sherehe ya Samhain mwishoni mwa Oktoba, mwezi ambao waliamini kwamba mizuka na roho waovu walizurura duniani kuliko wakati mwingine wowote.

KARNE YA 1 W.K.

Waroma wanawashinda Waselti na wanaanza kufuata desturi za Samhain zinazohusiana na roho waovu.

KARNE YA 7 W.K.

Inasemekana kwamba Papa Boniface wa Nne anaanzisha sherehe ya kila mwaka ya Siku ya Watakatifu Wote ili kuwakumbuka wafia-imani.a

KARNE YA 11 W.K.

Novemba 2 inawekwa kuwa Siku ya Wafu yaani siku ya kuwakumbuka wafu.

KARNE YA 18 W.K.

Jina la sikukuu hiyo Halloween (Usiku Mtakatifu) linaanza kuonekana katika machapisho.

KARNE YA 19 W.K.

Maelfu ya watu wa Ireland wanaohamia Marekani wanakuja na desturi zao za Halloween, na baada ya muda, desturi hizo zinachanganywa na zile za wahamiaji wengine kutoka Uingereza, Ujerumani, Afrika, na sehemu nyingine za ulimwengu.

KARNE YA 20 W.K.

Halloween inakuwa sikukuu maarufu kotekote nchini Marekani.

KARNE YA 21 W.K.

Halloween inakuwa biashara kubwa inayowaletea wafanyabiashara mabilioni ya pesa ulimwenguni pote.

a Neno la Kiingereza hallow ni neno la kale linalomaanisha “mtakatifu.” Siku ya Watakatifu Wote ni sikukuu ya kuwakumbuka watakatifu waliokufa. Katika Kiingereza Mkesha wa Siku ya Watakatifu Wote uliitwa All Hallow Even, baadaye ulifupishwa kuwa Halloween.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki