Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 6/14 uku. 3
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2014
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • China
  • Ulimwenguni
  • Kanada
  • Ireland
  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Matibabu Mbalimbali na Masuala Yanayohusika
    Amkeni!—2004
  • Arusi za Kikristo Ambazo Zinaleta Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ni Nini Hutendeka Katika Harusi za Mashahidi wa Yehova?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2014
g 6/14 uku. 3

KUUTAZAMA ULIMWENGU

China

Wenzi wa Ndoa waliotalikiana

Kiwango cha talaka jijini Beijing kilifikia asilimia 41 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2013 kwa kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka wa 2012. Wataalamu wanasema kwamba huenda hali hiyo imesababishwa na wenzi wa ndoa wanaotaka kuepuka kiwango kipya cha kodi cha asilimia 20 kutokana na mauzo ya nyumba. Katika hali fulani watu waliotalikiana wanaweza kupunguziwa kodi hiyo wanapouza nyumba mara ya pili.

Ulimwenguni

Wadudu wanaoliwa wakiwa katika sahani

Shirika la Umoja wa Mataifa linawashauri watu kula wadudu ili kupambana na utapiamlo. Kulingana na ripoti moja ya hivi karibuni, wadudu wana lishe nao hula vitu ambavyo wanadamu hawali, hivyo wadudu wanaoliwa ni chakula “kinachoweza kuliwa badala ya nyama.” Hata hivyo ripoti hiyo ilisema kwamba “katika maeneo fulani watu hawapendi kula wadudu.”

Kanada

viini-tete vya wanadamu vilivyogandishwa

Kliniki za mambo ya uzazi zinakabili vizuizi vya kisheria na kimaadili kuhusiana na viini-tete vya wanadamu vilivyogandishwa ambavyo “wamiliki” wake hawapatikani tena. Iliripotiwa kwamba kliniki fulani inamiliki viini-tete 1,000 vya wateja ambao “haijulikani waliko.”

Ireland

Huduma ya ndoa ya wasioamini kuwapo kwa mungu

Wakatoliki nchini Ireland walichagua kati ya kufunga ndoa ya kidini au ya kiserikali hadi mwaka 2013, wakati ndoa zinazofungwa na kikundi cha haki za binadamu zilipoanzishwa. Kulingana na shirika la habari la Reuters, “uhitaji wa watu wengi wa kufunga ndoa isiyo ya kiserikali au ya kidini umesababisha msongamano” katika kikundi hicho cha kufungisha ndoa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki