Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g16 Na. 5 uku. 7
  • Kuimulika Amerika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuimulika Amerika
  • Amkeni!—2016
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kusoma Barua Pepe Mara Chache Hupunguza Mkazo
  • Kulinda Viumbe wa Baharini
  • Jeuri Nchini Brazili
  • Jinsi ya Kudhibiti Mfadhaiko
    Amkeni!—2010
  • Jinsi ya Kukabiliana na Mkazo
    Amkeni!—2020
  • Mkazo Mzuri, Mkazo Mbaya
    Amkeni!—1998
  • Ninaweza Kukabiliana Jinsi Gani na Mikazo Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2016
g16 Na. 5 uku. 7
Samaki wakiwa baharini

KUUTAZAMA ULIMWENGU

Kuimulika Amerika

Habari kutoka nchi za Magharibi zinaonyesha kwamba hekima ya Biblia ina faida sikuzote.

Kusoma Barua Pepe Mara Chache Hupunguza Mkazo

Mtu anayesoma barua pepe mara tatu kwa siku anaonekana mtulivu; anayesoma kila mara huwa na mkazo

Utafiti uliofanywa Vancouver, nchini Kanada, ulionyesha kwamba kusoma barua pepe mara tatu kwa siku, badala ya kila mara unapotumiwa kunaweza kupunguza mkazo. Kostadin Kushlev, aliyeongoza utafiti huo alisema hivi: “Watu hushindwa kujizuia kusoma barua pepe, ilhali kufanya hivyo kungepunguza mkazo.”

JAMBO LA KUFIKIRIA: Tunaishi “nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo,” hivyo, ni muhimu kutafuta njia za kupunguza mkazo!—2 Timotheo 3:1.

Kulinda Viumbe wa Baharini

Shirika la Kuhifadhi Wanyama-Pori lilipokea ripoti iliyosema hivi: “Idadi ya konokono, kamba na samaki imeripotiwa kuongezeka katika maeneo ambayo uvuvi umepigwa marufuku nchini Belize na visiwa vya Karibea. Inaongezea hivi: “Huenda idadi ya viumbe hao ikaongezeka kwa kasi katika maeneo yasiyovuliwa, yaani, kati ya mwaka mmoja hadi sita, hata hivyo, ili kurudia hali yake ya awali . . . huenda ikachukua miaka mingi.” Janet Gibson, meneja wa shirika hilo alisema hivi kuhusu nchi ya Belize: “Ni wazi kwamba kupiga marufuku uvuvi katika maeneo fulani kumechangia kuongeza kwa samaki na viumbe wengine wa baharini.”

JAMBO LA KUFIKIRIA: Je, uwezo wa asili wa kurudia hali ya awali hauthibitishi kwamba kuna Muumba mwenye hekima?—Zaburi 104:24, 25.

Jeuri Nchini Brazili

Vyombo vya habari vya Agência Brasil vinaripoti kwamba visa vya jeuri vimeongezeka sana nchini humo. Mwaka wa 2012, watu zaidi ya 56,000 waliuawa, hiyo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa na Wizara ya Afya katika kipindi cha mwaka mmoja. Luís Sapori mtaalamu wa mambo ya usalama wa Umma alisema kwamba ongezeko hilo linaonyesha kwamba maadili yameharibika. Watu wanapokosa kutii sheria za nchi, “wao hutumia nguvu ili kupata kile wanachotaka.”

JE, WAJUA? Biblia ilitabiri kuhusu wakati ambao upendo wa wengi “utapoa” na uasi sheria utaongezeka.—Mathayo 24:3, 12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki