Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g17 Na. 6 uku. 3
  • Je, Ulimwengu Umepoteza Mwelekeo Au La?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ulimwengu Umepoteza Mwelekeo Au La?
  • Amkeni!—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Wanasayansi Wasogeza Mbele Mshale wa Saa ya Mwisho wa Dunia—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2012
  • Watu Wanapendezwa Sana na Mwisho wa Dunia
    Amkeni!—2012
  • Je, Tisho la Nyuklia Limekwisha?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2017
g17 Na. 6 uku. 3
Saa ya Maangamizi

HABARI KUU | JE, ULIMWENGU UMEPOTEZA MWELEKEO?

Je, Ulimwengu Umepoteza Mwelekeo Au La?

MWANZONI mwa mwaka wa 2017 wanasayansi walitoa tangazo lenye kuogopesha. Mwezi Januari, kikundi cha wanasayansi kilitangaza kwamba ulimwengu umekaribia kupatwa na janga kubwa zaidi kuwahi kutokea. Wakitumia Saa ya mfano ya Maangamizi inayoonyesha jinsi wanadamu ulimwenguni pote wanavyokaribia kuangamia, wanasayansi walisogeza mbele mshale wa dakika wa saa hiyo kwa sekunde 30. Saa hiyo inaonyesha kwamba sasa hivi bado dakika mbili na nusu tu kabla ya saa sita usiku, kumaanisha kwamba ulimwengu umekaribia sana kuangamia kuliko wakati mwingine wowote kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita!

Mwaka wa 2018, wanasayansi wanapanga kufanya uchunguzi tena ili kuona tumekaribia kwa kadiri gani mwisho wa ulimwengu. Je, Saa ya Maangamizi bado itaonyesha kwamba tumekaribia janga kubwa ambalo halijawahi kutokea? Una maoni gani? Je, ulimwengu umepoteza mwelekeo? Huenda swali hilo likaonekana kuwa gumu kwa sababu hata wataalamu wenyewe hawakubaliani kuhusu jambo hilo. Si kila mtu anayeamini kwamba kuna siku isiyoepukika ya maangamizi.

Kwa kweli, mamilioni ya watu wanaamini kwamba kutakuwa na maisha mazuri wakati ujao. Wanasema kwamba wana uthibitisho unaoonyesha kuwa wanadamu na dunia yetu itadumu milele na kwamba maisha yetu yataboreka. Je, uthibitisho huo unaaminika? Je, ulimwengu umepoteza mwelekeo au la?

“Saa ya Maangamizi ni mchoro wa saa unaotambuliwa ulimwenguni pote ambao unaonyesha jinsi tunavyokaribia kuharibu kabisa mfumo wa maisha duniani kupitia vifaa hatari vya kisasa tulivyobuni sisi wenyewe. Silaha za nyuklia zinachukua nafasi ya kwanza, lakini vitu vingine hatari vinatia ndani vifaa vya kisasa vinavyoharibu hali ya hewa, teknolojia za kibiolojia, na teknolojia za intaneti ambazo zinaweza kuisababishia dunia na wanadamu madhara ya kudumu, iwe ni kwa kukusudia, au kimakosa.”—Bulletin of the Atomic Scientists.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki