Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w13 7/15 uku. 26
  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Habari Zinazolingana
  • Washiriki Wapya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Washiriki Wapya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Mkutano wa Kihistoria
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
w13 7/15 uku. 26
[Picha katika ukurasa wa 26]

Mshiriki Mpya wa Baraza Linaloongoza

Jumatano asubuhi, Septemba 5, 2012, familia ya Betheli ya Marekani na ya Kanada zilitangaziwa kwamba mshiriki mpya ameongezwa katika Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova. Mark Sanderson alianza kutumikia akiwa mshiriki wa Baraza Linaloongoza kuanzia Septemba 1, 2012.

Ndugu Sanderson alilelewa na wazazi wake Wakristo huko San Diego, California, Marekani, naye alibatizwa Februari 9, 1975. Alianza kutumikia akiwa painia huko Saskatchewan, Kanada, Septemba 1, 1983. Alihitimu darasa la saba la Shule ya Mazoezi ya Kihuduma (sasa inaitwa Shule ya Biblia ya Ndugu Waseja) Desemba 1990, huko Marekani. Ndugu Sanderson aliwekwa rasmi Aprili 1991 ili kutumikia akiwa painia wa pekee katika kisiwa cha Newfoundland, Kanada. Baada ya kutumikia akiwa mwangalizi badala wa mzunguko, Februari 1997, alialikwa kutumikia akiwa mshiriki wa familia ya Betheli ya Kanada. Mnamo Novemba 2000, alipewa mgawo wa kuhamia ofisi ya tawi ya Marekani, alikotumika katika idara ya Huduma za Habari za Hospitali na baadaye katika Idara ya Utumishi.

Katika Septemba 2008, Ndugu Sanderson alihudhuria Shule ya Washiriki wa Halmashauri ya Tawi na baadaye akawekwa rasmi kuwa mshiriki wa Halmashauri ya Tawi ya Filipino. Septemba 2010, alialikwa kurudi tena Marekani alikotumikia akiwa msaidizi katika Halmashauri ya Utumishi ya Baraza Linaloongoza.

Washiriki wa Sasa wa Baraza Linaloongoza

[Picha]

Waliosimama nyuma, kushoto kwenda kulia: D. H. Splane, A. Morris wa Tatu, D. M. Sanderson, G. W. Jackson, M. S. Lett. Walioketi mbele, kushoto kwenda kulia: S. F. Herd, G. Lösch, G. H. Pierce. Washiriki wote wa Baraza Linaloongoza ni Wakristo watiwa-mafuta

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki