Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w17 Januari uku. 32
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Faida na Hasara za Moto
    Amkeni!—2002
  • Moto! Je, Utatumia Kizima-Moto Kipi?
    Amkeni!—2001
  • Uthibitisho Mkubwa Zaidi wa Upendo wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Jaribu la Imani
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
w17 Januari uku. 32
IIsaka akiwa amebeba kuni na Abrahamu akibeba chombo kilicho na makaa ya moto

Je, Wajua?

Moto ulisafirishwaje katika nyakati za kale?

SIMULIZI la Biblia katika Mwanzo 22:6 linasema kwamba Abrahamu alipokuwa akijitayarisha kwenda kutoa dhabihu katika eneo la mbali, “alichukua kuni za toleo la kuteketezwa akamtwika Isaka mwana wake, naye akachukua mikononi mwake moto na kisu cha kuchinjia, na wote wawili wakasonga mbele pamoja.”

Maandiko hayataji njia iliyotumiwa kuwasha moto nyakati za kale. Kuhusu simulizi lililotajwa mwanzoni, mchunguzi mmoja anaamini kwamba “haingekuwa rahisi kubeba [mwali wa moto] katika safari hiyo ndefu” ya Abrahamu na Isaka. Kwa hiyo, huenda kile kilichozungumziwa ni kifaa kilichohitajika ili kuwasha moto.

Hata hivyo, wengine husema kwamba haikuwa rahisi kuwasha moto nyakati za kale. Ilipowezekana, watu waliona kwamba ilikuwa rahisi kuomba kaa lenye moto kutoka kwa majirani badala ya kuwasha moto. Wasomi kadhaa wanaamini kwamba kile ambacho Abrahamu alibeba kilikuwa chombo fulani, labda chungu kilichoning’inizwa kwa mnyororo, chenye makaa ya moto yaliyohifadhiwa kutoka kwenye moto uliowashwa usiku uliotangulia. (Isa. 30:14) Wakati wa safari ndefu, makaa yenye moto yaliyosafirishwa kwa njia hiyo yangeweza kutumiwa pamoja na kuni ndogo kuwasha moto kwa urahisi wakati wowote.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki