Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Juni 30, 2014.
Kwa nini kanuni iliyorekodiwa kwenye Kutoka 23:2 ni muhimu sana tunapochagua vitumbuizo na tafrija? [Mei 5, w11 7/15 uku. 10-11 fu. 3-7]
Sheria iliyosema kwamba makuhani walipaswa kuoga kabla ya kutoa dhabihu kwa Yehova ilikuwa ni muhimu kiasi gani, na inatoaje kikumbusho chenye nguvu kwa watumishi wa Mungu leo? (Kut. 30:18-21) [Mei 19, w96 7/1 uku. 9 fu. 9]
Kwa nini Haruni hakuadhibiwa alipotengeneza ndama wa dhahabu? (Kut. 32:1-8, 25-35) [Mei 19, w04 3/15 uku. 27 fu. 4]
Sheria ya Mungu kukataza Waisraeli kuoa watu walioabudu miungu wengine inahusianaje na maoni ya Mkristo kuhusu uchumba na ndoa? (Kut. 34:12-16) [Mei 26, w89-E 11/1 uku. 20-21 fu. 11-13]
Kwa nini kisa cha Bezaleli na Oholiabu ni kitia moyo kwetu leo? (Kut. 35:30-35) [Mei 26, w10 9/15 uku. 10 fu. 13]
Bamba la “Ishara takatifu ya wakfu” ambalo liliwekwa juu ya kilemba kilichovaliwa na kuhani mkuu wa Israeli, lilikuwa ni kikumbusho cha nini, na alama hiyo inatufundisha nini kuhusu kujiweka wakfu? (Kut. 39:30) [Juni 2, w01 2/1 uku. 14 fu. 2-3]
Wakristo wote wana daraka lipi kuhusu kuripoti dhambi nzito za Mkristo mwenzao? (Law. 5:1) [Juni 9, w97 8/15 uku. 27]
Dhabihu za ushirika zilikuwa na sehemu gani muhimu katika wakati wa Waisraeli, na mpango huo unafananisha nini leo? (Law. 7:31-33) [Juni 16, w12 1/15 uku. 19 fu. 11-12]
Dhambi ya Nadabu na Abihu wana wa Haruni, huenda ilihusisha nini, na tunajifunza nini kutokana na simulizi hilo? (Law. 10:1, 2, 9) [Juni 23, w04 5/15 uku. 22 fu. 6-8]
Kwa nini kuzaa kulimfanya mwanamke awe “asiye safi”? (Law. 12:2, 5) [Juni 23, w04 5/15 uku. 23 fu. 2]