Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/14 uku. 6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2014
Huduma Yetu ya Ufalme—2014
km 12/14 uku. 6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Desemba 29, 2014.

  1. Tunapaswa kuwa na maoni gani kuhusu amri iliyo katika Kumbukumbu la Torati 14:1 inayokataza kujikatakata mwili wakati wa kumuombolezea mtu aliyekufa? [Nov. 3, w04 9/15 uku. 27 fu. 4]

  2. Kwa nini wafalme wa Israeli walipaswa kuwa na nakala yao wenyewe ya Sheria ya Mungu na ‘kuisoma siku zote za maisha yao’? (Kum. 17:18-20) [Nov. 3, w02 6/15 uku. 12 fu. 4]

  3. Kwa nini Biblia inasema kwamba “usilime kwa ng’ombe-dume na punda pamoja,” na amri hiyo ya kutofunga nira isivyo sawa inawahusuje Wakristo? (Kum. 22:10) [Nov. 10, w03 10/15 uku. 32]

  4. Kwa nini kutwaa “kuwa rehani jiwe la kusagia la mkononi au jiwe lake la juu la kusagia” kulikatazwa? (Kum. 24:6) [Nov. 17, w04 9/15 uku. 26 fu. 3]

  5. Waisraeli walipaswa kutii wakiwa na mtazamo gani, na ni nini kinapaswa kutuchochea kumtumikia Yehova? (Kum. 28:47) [Nov. 24, w10 9/15 uku. 8 fu. 4]

  6. Andiko la Kumbukumbu la Torati 30:19, 20 lina matakwa gani matatu ya msingi ya kupata uzima? [Nov. 24, w10 2/15 uku. 28 fu. 17]

  7. Je, tunapaswa kutamka kwa sauti ya chini maneno yote kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo tunaposoma? Eleza. (Yos. 1:8) [Des. 8, w13 4/15 uku. 7 fu. 4]

  8. “Mkuu wa jeshi la Yehova” anayetajwa kwenye Yoshua 5:14, 15 ni nani, na jambo hilo linatutia moyo jinsi gani? [Des. 8, w04 12/1 uku. 9 fu. 2]

  9. Ni nini kilichomwongoza Akani afanye dhambi, na tunajifunza nini kutokana na mfano wake mbaya? (Yos. 7:20, 21) [Des. 15, w10 4/15 uku. 20-21 fu. 2,  5]

  10. Kielelezo cha Kalebu kinatutiaje moyo leo? (Yos. 14:10-13) [Des. 29, w04 12/1 uku. 12 fu. 2]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki