Indonesia
SIMULIZI hili lenye kusisimua linahusu Wakristo jasiri ambao walisimama imara wakati wa misukosuko ya kisiasa, migogoro ya kidini, na marufuku iliyodumu kwa miaka 25. Soma kuhusu ndugu aliyekuwa katika orodha ya watu ambao wangeuawa na Wakomunisti na kuhusu Mkristo mkomavu ambaye awali alikuwa kiongozi wa kundi la uhalifu. Soma historia inayosisimua ya wasichana wawili viziwi waliokuwa marafiki na baadaye wakagundua kwamba walitoka katika familia moja. Pia, soma jinsi watu wa Yehova wanavyofaulu kuhubiri eneo lenye Waislamu wengi duniani.