Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 23
  • Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jibu la Biblia
  • Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2020
  • Ufalme Wa Mungu
    Amkeni!—2013
  • Ishi Milele Juu ya Dunia-paradiso
    Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?
  • Baada ya Har-Magedoni, Dunia-Paradiso
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 23
Mandhari ya Paradiso

Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?

Jibu la Biblia

Ufalme wa Mungu utaondoa serikali zote za wanadamu na kuitawala dunia yote. (Danieli 2:44) Baada ya kutimiza hilo, Ufalme wa Mungu . . .

  • Utawaondoa waovu, ambao wanatudhuru kwa sababu ya ubinafsi wao. “Nao waovu, watakatiliwa mbali kutoka duniani.”—Methali 2:22.

  • Utakomesha vita vyote. “[Mungu] anakomesha vita mpaka kwenye mwisho wa dunia.”—Zaburi 46:9.

  • Utaondoa umaskini na kuleta amani duniani. “Kila mtu ataishi kwa amani chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, na hakuna mtu atakayewaogopesha.”—Mika 4:4, Good News Translation.

  • Utaigeuza dunia kuwa paradiso. “Majangwa yasiyokuwa na maji yatafurahi; mashamba yasiyozaa yatashangilia na kuchanua maua.”—Isaya 35:1, Contemporary English Version.

  • Utaandaa kazi nzuri na yenye kufurahisha kwa kila mtu. “Watu [wa Mungu] waliochaguliwa wataitumia kazi ya mikono yao wenyewe kikamilifu. Hawatafanya kazi ya bure.”—Isaya 65:21-23.

  • Utaondoa magonjwa. “Hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”—Isaya 33:24.

  • Utatuondolea uzee. “Nyama yake na iwe laini kuliko wakati wa ujana; na arudi kwenye siku za nguvu za ujana wake.”—Ayubu 33:25.

  • Utawafufua wafu. “Wote waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho wataisikia sauti yake [Yesu] na kutoka.”—Yohana 5:28, 29.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki