Kujikumbusha shule ya huduma ya kitheokrasi
Kujikumbusha, vitabu vikiwa vyenye kufungwa, habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi katika majuma toka Mei 3 hadi Agosti 23, 1999. Tumia karatasi nyingine uandike majibu ya maulizo mengi iwezekanavyo katika wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa kujikumbusha kwa kuandika, Biblia tu ndiyo inayoweza kutumiwa kwa kujibu ulizo lolote. Mitajo inayofuata ulizo imetiwa kwa ajili ya utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu zaweza kuwa hazionyeshwi juu ya mitajo yote ya Mnara wa Mlinzi.]
Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:
1. Si lazima wazazi wavunje kanuni za Biblia ili kushughulikia watoto wao kwa njia yenye kufaa. [fy-SW uku. 108 fu. 14]
2. Kichwa cha Biblia nzima ni kule kutetewa kwa Yehova kupitia Ufalme utakaotawaliwa na ile “mbegu” iliyoahidiwa. (Mwa. 3:15) [si-SW uku. 17 fu. 30]
3. Kuna ushuhuda mchache wa kiakiolojia na mwingineo wa nje unaothibitisha usahihi wa matukio yaliyoandikwa katika kitabu cha Kutoka. [si-SW uku. 20 fu. 4]
4. Wale wanaoishi katika ufukara (umaskini) mkubwa hawako katika hali ya kutoa mchango wa kifedha ili kuendeleza faida za Ufalme. [w97-SW 9/15 uku. 5 fu. 7]
5. Kuwalipa wazazi na babu na nyanya haki yao ni sehemu ya ibada yetu kwa Yehova. (1 Tim. 5:4) [w97-SW 9/1 uku. 4 maf. 1-2]
6. Kushika sabato kulikuwa kwanza ishara kati ya Yehova na mataifa yote. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona rs-SW uku. 269 fu. 2.]
7. Mtoto anapofikia umri wa kutosha kuanza kufanya maamuzi yake mwenyewe, yeye huwa na kiasi kilichoongezeka cha daraka kwa matendo yake, zaidi kuhusiana na sheria ya Mungu. (Rom. 14:12) [fy-SW uku. 135 fu. 17]
8. Musa aliandika kitabu cha Walawi mnamo mwaka wa 1513 K.W.K. [si-SW uku. 25 maf. 3-4]
9. Maneno ya Yesu yanayoandikwa kwenye Luka 21:20, 21 yalitimizwa mnamo 66 W.K., majeshi ya Kiroma chini ya amri ya Jemadari Tito yalipoondoka kutoka Yerusalemu. [w97-SW 4/1 uku. 5 maf. 4-5]
10. Fundisho la Epikurasi lilikuwa hatari kwa Wakristo kwa kuwa lilikuwa na msingi juu ya mtazamo wake usio na imani, unaoelezwa kwenye 1 Wakorintho 15:32. [w97-SW 11/1 uku. 24 fu. 4]
Jibu maulizo yafuatayo:
11. Ni somo gani tunalojifunza kutokana na katazo la kutokula mafuta ya nyama, linalosemwa kwenye Walawi 3:17? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w84-F 15/5 uku. 27 fu. 3.]
12. Kwa nini Yehova ameruhusu Shetani Ibilisi aweko? (Kut. 9:15) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w92-SW 3/15 uku. 10 fu. 14.]
13. Wakati mshiriki wa familia anapopatwa na ugonjwa mkali, ni hatua gani zinazopasa kuchukuliwa na familia ili kuweka mambo ya kutangulizwa? (Mez. 15:22) [fy-SW uku. 122 fu. 14]
14. Taifa la Israeli lilikuwa “ufalme wa makuhani” katika maana gani? (Kut. 19:6) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 7/1 uku. 16 fu. 8.]
15. Kuna tofauti gani kati ya jicho “sahili” na jicho “bovu”? (Mt. 6:22, 23) [w97-SW 10/1 uku. 26 fu. 5]
16. Inaweza kusemwaje kwamba Daudi alitembea “kwa uaminifu-maadili wa moyo na unyoofu” huku akiwa alifanya makosa? (1 Fal. 9:4) [w97-SW 5/1 uku. 5 fu. 2]
17. Ni mapendeleo gani ya siku ya kisasa yanayoonyeshwa kimbele na jambo la kwamba Waisraeli walifanya “yote kama BWANA alivyoagiza” kuhusiana na ujenzi wa tabenakulo? (Kut. 39:32) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 12/15 uku. 12 fu. 9.]
18. Ni nini kinachoonyeshwa na jambo la kwamba Yehova alijifunua kuwa “Mimi nitathibitika kuwa kile ambacho mimi nitathibitika kuwa”? (Kut. 3:14) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 10 fu. 6.]
19. Ni somo gani linalofundishwa na tukio lenye kuhusisha Nadabu na Abihu, linalorekodiwa kwenye Walawi 10:1, 2? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w84-F 15/5 uku. 27 fu. 4.]
20. Chini ya Sheria ya Musa, kwa nini kuzaliwa kwa mtoto kulimfanya mama awe “si safi”? (Law. 12:2, 5) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w84-F 15/5 uku. 27 fu. 6.]
Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:
21. Ingawa hakuna ponyo la kimuujiza kwa upweke, mzazi anayelea watoto peke yake aweza kuuvumilia kwa nguvu kutoka kwa _________________________, nguvu inayopatika kupitia _________________________ zenye kudumu. (1 Tim. 5:5) [fy-SW uku. 112 fu. 21]
22. Jambo lenye kuhuzunisha katika maisha ya mtu laweza kuwa tokeo la _________________________ au kwa sababu ya hali yetu wenyewe _________________________. [w97-SW 5/15 uku. 22 fu. 7]
23. Kitabu cha Kutoka hufunua Yehova kuwa _________________________ na _________________________ wa makusudi yake mazuri sana. [si-SW uku. 24 fu. 26]
24. Kimsingi, ni jinsi tutendavyo _________________________, si jinsi tutendavyo _________________________, ndivyo hufunua vile tulivyo kindani kwelikweli. [w97-SW 10/15 uku. 29 fu. 4]
25. Ikiwa misherehekeo ya mavuno ina vidokezo _________________________ au _________________________, Wakristo wa kweli waweza kuepuka kutompendeza Yehova kwa kukataa _________________________ kokote katika ibada hiyo iliyochafuliwa. [w97-SW 9/15 uku. 9 fu. 6]
Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:
26. Ile “miaka mia nne” ya kuteswa kwa mbegu ya Abrahamu ilianza wakati Ishmaeli alipomfanyia mzaha Isaka katika (1943 K.W.K.; 1919 K.W.K.; 1913 K.W.K.) na ikaisha kwa kukombolewa kutoka Misri katika (1543 K.W.K.; 1519 K.W.K.; 1513 K.W.K.). (Mwa. 15:13) [si-SW uku. 17 fu. 31]
27. Iwe familia yakabiliana kwa mafanikio na ugonjwa mbaya sana au sivyo yategemea kwa kadiri kubwa (usalama wa kifedha; mtazamo; kanuni ya bima) wa washiriki wa familia. (Mez. 17:22) [fy-SW uku. 120 fu. 10]
28. Mtu anayesema moyoni mwake “Hakuna Mungu” huitwa “mpumbavu” kwa kuwa yeye ni (mwenye kupungukiwa kiadili; asiye na elimu; mwenye kukosa uwezo wa kufikiri). (Zab. 14:1) [w97-SW 10/1 uku. 6 fu. 8]
29. Adamu na Hawa walipoasi, jambo la maana zaidi walilopoteza lilikuwa (ukamilifu; uhusiano na Mungu; makao ya bustani), uliokuwa ufunguo wao wa kupata furaha. [w97-SW 10/15 uku 6 fu. 2]
30. Kitabu cha (Mwanzo; Kutoka; Mambo ya Walawi) chataja takwa la utakatifu mara nyingi zaidi kuliko kitabu kinginecho chote cha Biblia. [si-SW uku. 26 fu. 9]
Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nazo:
Kut. 5:2; 21:29; Mez. 1:8; Gal. 5:20; Yak. 1:14, 15
31. Mtu yeyote anayedai kuwa Mkristo ambaye, kwa kurudia-rudia na bila kutubu, hushindwa na hasira za ghafula zenye jeuri, kutia ndani kutenda vibaya washiriki wa familia, aweza kutengwa na ushirika kutoka katika kutaniko. [fy-SW uku. 150 fu. 23]
32. Jinsi tutendavyo huanza na jinsi tunavyofikiri. [fy-SW uku. 148 fu. 18]
33. Yehova Mungu hushusha wale wote wanaokataa kwa kiburi kukubali Uungu wake. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w92-SW 12/15 uku. 13 fu. 18.]
34. Ingawa Biblia humgawia baba daraka kuu la kuwafunza watoto, mama ana fungu la maana la kutimiza pia. [fy-SW uku. 133 fu. 12]
35. Sheria haikuruhusu ulegevu uwe dai la kuomba rehema mtu alipouawa. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 11 fu. 5.]