Kujikumbusha shule ya huduma ya kitheokrasi
Kujikumbusha, vitabu vikiwa vyenye kufungwa, habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi katika majuma toka Septemba 6 hadi Desemba 20, 1999. Tumia karatasi nyingine uandike majibu ya maulizo mengi iwezekanavyo katika wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa kujikumbusha kwa kuandika, Biblia tu ndiyo inaweza kutumiwa kwa kujibu ulizo lolote. Mitajo inayofuata ulizo imetiwa kwa ajili ya utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu zaweza kuwa hazionyeshwi juu ya mitajo yote ya Mnara wa Mlinzi.]
Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:
1. Yehova ameruhusu utawala wa kibinadamu wenye kujitegemea wenyewe ili kuthibitisha kwamba njia yake ya kutawala sikuzote ni sawa na ya haki. (Kum. 32:4; Yobu 34:10-12; Yer. 10:23) [w97-SW 2/15 uku. 5 fu. 3]
2. Biblia inaonyesha kwamba Mungu anakataza kulalamika kwa namna zote. [w97-SW 12/1 uku. 30 maf. 3-4]
3. Wazazi hudumisha uhusiano pamoja na watoto wao waliooa katika mahali panapofaa kwa kutambua kanuni za kimungu za ukichwa na utaratibu mzuri. (Mwa. 2:24; 1 Kor. 11:3; 14:33, 40) [fy-SW uku. 164 fu. 6]
4. Marko 6:31-34 laonyesha kwamba Yesu alisukumwa na huruma kuelekea umati kwa sababu tu ya ugonjwa na umaskini wao. [w97-SW 12/15 uku. 29 fu. 1]
5. Ikiwa Mkristo aliye mmoja wa kondoo wengine hawezi kuhudhuria Ukumbusho wa kifo cha Yesu, yeye angepaswa kuuadhimisha mwezi mmoja baadaye kulingana na kanuni inayosemwa kwenye Hesabu 9:10, 11. (Yn. 10:16) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w93-SW 2/1 uku. 31 fu. 9.]
6. Ijapokuwa babu au nyanya Wakristo hawachukui daraka la baba na mama ili kukazia kikiki kweli katika watoto wao, babu au nyanya wanaweza kuchangia katika ukuzi wa kiroho wa mtoto. (Kum. 6:7; 2 Tim. 1:5; 3:14, 15) [fy-SW uku. 168 fu. 15]
7. Mezali 6:30 laonyesha kwamba kuiba kunaweza kusamehewa au kutetewa chini ya hali fulani. [g97-SW 11/8 uku. 19 fu. 2]
8. Mnamo 1530, William Tyndale alikuwa wa kwanza kutumia jina la Mungu, Yehova, katika tafsiri ya Kiingereza ya Maandiko ya Kiebrania. [w97-SW 9/15 uku. 28 fu. 3]
9. Leo, jiji la makimbilio la ufananisho ni uandalizi wa Mungu wa kutulinda tusipatwe na kifo ambacho kingetokana na kuvunja amri yake juu ya utakaso wa damu. (Hes. 35:11) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 17 fu. 8.]
10. Jina Kumbukumbu la Torati, linalomaanisha “Sheria ya Pili,” lafaa kwa sababu kitabu hiki cha Biblia ni mrudilio tu wa Sheria. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona si-SW uku. 36 fu. 4.]
Jibu maulizo yafuatayo:
11. Ni nini linalofananishwa na ile mikate miwili iliyotiwa chachu, ambayo ilitolewa na kuhani mkuu wakati wa Sikukuu ya Pentekoste? (Law. 23:15-17) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w98-SW 3/1 uku. 13 fu. 21.]
12. Yubile ya Kikristo ilianza wakati gani, na hiyo ilileta uhuru wa aina gani wakati huo? (Law. 25:10) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 5/15 uku. 24 fu. 14.]
13. Kulingana na maandishi ya kitabu cha Hesabu, kuokoka kunategemea mambo gani matatu? [si-SW uku. 30 fu. 1]
14. Ni katika njia gani Musa alikuwa mfano mzuri katika kuonyesha kwamba hakuwa na roho ya wivu? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 9/15 uku. 18 fu. 11.]
15. Kisa cha Kora, Dathani na Abiramu kinaonyeshaje kwamba kuona hakumfanyi sikuzote mtu aamini? [w97-SW 3/15 uku. 4 fu. 2]
16. Ni pande gani mbili za kuwaheshimu wazazi wazee-wazee zinazoonyeshwa kwenye Mathayo15:3-6 na 1 Timotheo 5:4? [fy-SW kur. 173-5 maf. 2-5]
17. Ni somo gani la maana linakaziwa kwenye Hesabu 26:64, 65? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona g95-SW 8/8 kur. 10-11 maf. 5-8.]
18. Mfano wa Finehasi unatusaidiaje kufahamu kile ambacho wakfu kwa Yehova humaanisha? (Hes. 25:11) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 16 maf. 12-13.]
19. Mtu aliye katika jiji la makimbilio la ufananisho anawezaje ‘kwenda nje ya mupaka’ wa jiji hilo? (Hes. 35:26) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 20 fu. 20.]
20. Ni katika njia gani Codex Sinaiticus ilikuwa baraka kwa utafsiri wa Biblia? [w97-SW 10/15 uku. 11 fu. 2]
Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:
21. Yehova aliruhusu uovu uwepo ili kuthibitisha mara moja kwa wakati wote kweli ya msingi kwamba yeye peke yake ndiye __________________________ na kwamba __________________________ sheria zake ni kwa lazima kwa ajili ya amani na furaha yenye kuendelea ya viumbe vyake vyote. (Zab. 1:1-3; Mez. 3:5, 6; Mhu. 8:9) [w97-SW 2/15 uku. 5 fu. 4]
22. Kitabu cha Walawi ni chenye kutokeza katika kukazia __________________________ wa damu, kikionyesha kwamba matumizi pekee yanayoruhusiwa ya damu ni kwa __________________________. [si-SW uku. 29 fu. 33]
23. Kwa kupatana na Zaburi 144:15b, furaha ya kweli ni hali ya moyoni, inayotegemea __________________________ ya kweli na __________________________ mzuri pamoja na Yehova. [w97-SW 3/15 uku. 23 fu. 7]
24. Biblia iliyotokana na tafsiri ya Biblia ya Kiebrania katika Kigiriki cha kawaida, iliyomalizika yapata mwaka wa 150 K.W.K., ilikuja kujulikana kuwa __________________________; tafsiri ya Jerome ya Biblia katika Kilatini ilikuja kujulikana kuwa __________________________, ikiwa ilimalizika yapata mwaka wa 400 W.K. [w97-SW 8/15 uku. 9 fu. 1; uku. 10 fu. 4]
25. Kwa kurejezea habari kuhusu Balaamu na Kora kama inavyoandikwa katika kitabu cha Hesabu, Yuda alionya Wakristo ili wajilinde wasinaswe na mitego ya __________________________ na __________________________. [si-SW uku. 35 fu. 35]
Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:
26. Mara moja kwa mwaka, kwenye (Sikukuu ya Vibanda; Siku ya Kufunika; Sikukuu ya Kupitwa), taifa lote la Israeli, kutia ndani wakazi-wageni waliomwabudu Yehova, lilipaswa (kuacha kazi zote; kulipa sehemu za kumi; kutoa matoleo ya matunda ya kwanza) na kufunga. (Law. 16:29-31) [Usomaji wa Biblia wa kila siku; ona w96-SW 7/1 uku. 10 fu. 12.]
27. Moja ya miradi ya Halmashauri ya Tafsiri ya Biblia ya Ulimwengu Mpya ulikuwa kutokeza tafsiri ambayo ingekuwa (ya neno kwa neno kwa kadiri iwezekanavyo; usimulizi katika maneno mengine wa lugha za awali; yenye kupatana na uelewevu mahususi wa kimafundisho) ili kuwapa wasomaji nafasi ya kukaribia zaidi onjo la lugha ya awali na ule utaratibu wa mawazo unaohusianishwa na lugha hizo. [w97-SW 10/15 uku. 11 fu. 5]
28. Kulingana na Waebrania 13:19, sala zenye kuendelea za waamini wenzetu zaweza kubadili (yale ambayo Mungu huruhusu; wakati wa kutenda wa Mungu; jinsi Mungu anavyoongoza mambo). [w97-SW 4/15 uku. 6 fu. 1]
29. ‘Kamba ya rangi ya samawi juu ya kishada cha kila pindo’ la Waisraeli iliombwa kuwa (urembo mtakatifu; alama ya kuwa wenye kiasi; kikumbusha chenye kuonekana cha kuwa wenye kuwekwa kando kutoka ulimwengu wakiwa watu wa Yehova). (Hes. 15:38, 39) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w84-F 1/15 uku. 20 fu. 16.]
30. Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kilichukua kipindi cha wakati cha (miezi miwili; mwaka mmoja; miaka miwili), na uandikaji wake ulimalizika mapema katika (1513; 1473; 1467) K.W.K. [si-SW uku. 36 fu. 6]
Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nazo:
Hes. 16:41, 49; Mt. 19:9; Luka 2:36-38; Kol. 2:8; 3:14
31. Maisha ya kujinyima raha hayaongozi kwenye utakatifu wa pekee wala kwenye nuru ya kweli. [g97-SW 10/8 uku. 21 fu. 3]
32. Uasherati ndio msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka kukiwa na uwezekano wa kuoa au kuolewa tena. [fy-SW kur. 158-9 fu. 15]
33. Kuwa mwenye shughuli katika utendaji mbalimbali wa kitheokrasi, hata katika miaka ya uzee, kunaweza kusaidia mtu akabiliane na kifo cha mwenzi wa ndoa. [fy-SW kur. 170-1 fu. 21]
34. Kuchambua njia ya Yehova ya kutekeleza haki kupitia watumishi wake waliowekwa rasmi kunaweza kuwa na matokeo yenye kuleta msiba. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w96-SW 6/15 uku. 21 fu. 13.]
35. Upendo usio na ubinafsi unawaunganisha mume na mke pamoja na kuwafanya watake kunufaishana zaidi na kunufaisha watoto wao. [fy-SW uku. 187 fu. 11]