Kujikumbusha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Kujikumbusha, vitabu vikiwa vyenye kufungwa, habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi katika majuma toka Septemba 4 mpaka Desemba 18, 2000. Tumia karatasi nyingine uandike majibu ya maulizo mengi iwezekanavyo katika wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa kujikumbusha kwa kuandika, Biblia tu ndiyo inaweza kutumiwa kwa kujibu ulizo lolote. Mitajo inayofuata ulizo imetiwa kwa ajili ya utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu zaweza kuwa hazionyeshwi juu ya mitajo yote ya Mnara wa Mlinzi.]
Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:
1. Daudi alimzuia Abishai asimwue Shimei kwa kuwa Daudi alikuwa na hatia kuhusiana na mashtaka ambayo Shimei alifanya dhidi yake. (2 Sam. 16:5-13) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w99-SW 5/1 uku. 32 fu. 3.]
2. Dhamiri iliyo safi, iliyozoezwa vizuri huongoza kwenye uhusiano wa kibinafsi pamoja na Mungu, na pia ni ya maana sana kwa ajili ya wokovu wetu. (Ebr. 10:22; 1 Pet. 1:15, 16) [w98-SW 9/1 uku. 4 fu. 4]
3. Habari katika 1 Wafalme ina thamani ya kihistoria tu kwa Mkristo kwa kuwa wafalme 2 tu juu ya wale 14 waliotawala katika Israeli na Yuda baada ya kifo cha Solomoni ndio walifanikiwa kufanya yaliyo haki machoni pa Yehova. [si-SW uku. 64 fu. 1]
4. Utawala wa Miaka Elfu wa Yesu unaweza kulinganishwa na utawala wa miaka 40 wa Solomoni wenye amani na ufanisi. (1 Fal. 4:24, 25, 29) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w90-SW 6/1 uku. 6 fu. 5.]
5. Mazishi yenye heshima ya Abiya ulikuwa uhakikisho wa wazi kwamba yeye alikuwa mwabudu mwaminifu mmoja pekee wa Yehova katika nyumba ya Yeroboamu. (1 Fal. 14:10, 13) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w95-SW 4/1 uku. 12 fu. 11.]
6. Kupata ubatizo wa Kikristo kunaonyesha kwamba mtu amekuwa mtumishi mkomavu wa Mungu. [w98-SW 10/1 uku. 28 fu. 2]
7. Yehova alimpa Eliya nguvu inayopita ya wanadamu, naye alimfanya asiweze kupatwa na woga. (1 Fal. 18:17, 18, 21, 40, 46) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w98-SW 1/1 uku. 31 fu. 2.]
8. Hekalu la Solomoni lilikuwa jengo la kutokeza si kwa sababu ya utukufu wake na uzuri wake wa nje tu bali pia kwa sababu hilo lilikuwa kivuli cha hekalu la kiroho la Yehova lililo lenye utukufu zaidi. [si-SW uku. 69 fu. 26]
9. Upofu ambao Elisha aliomba upige jeshi la maaskari Wasiria ulikuwa bila shaka upofu wa kiakili kwa kuwa wangeweza kumwona Elisha lakini hawangeweza kutambua yeye alikuwa nani. (2 Fal. 6:18, 19) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona si-SW uku. 71 fu. 10.]
10. Kuvaa “ushuhuda,” kunakotajwa kwenye 2 Wafalme 11:12, ilikuwa alama ya kimfano ya kuonyesha kwamba maelezo ya mfalme kuhusu Sheria ya Mungu hayangeweza kubadilishwa, na kwamba ilifaa kuyatii. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w91-SW 2/1 uku. 31 fu. 6.]
Jibu maulizo yafuatayo:
11. Kwa kupatana na 1 Yohana 2:15-17, ni nini wazazi wenye kumwogopa Mungu wanapaswa kuhimiza watoto wao waepuke wakati wanapowaongoza katika kuchagua kazi ya kimwili yenye kufaa? [w98-SW 7/15 uku. 5 fu. 2]
12. Ni nini linalomaanishwa na andiko la 2 Samweli 18:8, ambalo linasema: “Mwitu ukakula watu [wengi] kuliko upanga.”? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w87-SW 3/15 uku. 31 fu. 2.]
13. Ni nani leo wanaoweza kulinganishwa na watu wa jamaa ya Goliathi, Warefaimu, na ni nini wanalojitahidi kufanya? (2 Sam. 21:15-22) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w89-SW 1/1 uku. 20 fu. 8.]
14. Ni kanuni gani ya kibiblia yenye mafaa tunayojifunza kutokana na 2 Samweli 6:6, 7? [si-SW uku. 63 fu. 30]
15. Ni kanuni gani ya maana tunayoweza kujifunza kutokana na tukio linalohusu mwanamume aliyeuawa kwa sababu ya kutoheshimu Sabato? (Hes. 15:35) [w98-SW 9/1 uku. 20 fu. 2]
16. Ni kwa kufanya nini tunaweza kumwiga malkia wa Sheba, ambaye alisafiri mwendo mrefu ili kusikiliza “hekima ya Solomono”? (1 Fal. 10:1-9) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w99-SW 7/1 uku. 31 maf. 1-2.]
17. Kulingana na 1 Wafalme 17:3, 4, 7-9, 17-24, ni katika njia gani tatu Eliya alionyesha imani katika Yehova? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w92-SW 4/1 uku. 19 fu. 5.]
18. Kwa nini kukataa kwa Nabothi kutoa shamba lake la mizabibu kwa Ahabu hakukuwa wonyesho wa kichwa kigumu kwa upande wake? (1 Fal. 21:2, 3) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w97-SW 8/1 uku. 13 fu. 18.]
19. Maneno ya 2 Wafalme 6:16 yametumikaje ili kuwatia moyo watumishi wa Yehova leo? [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w98-SW 6/15 uku. 18 fu. 5.]
20. Ni katika njia gani Wakristo wa kweli leo wanapaswa kujilinda dhidi ya usimoni? [w98-SW 11/15 uku. 28 fu. 5]
Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:
21. __________________________ hakupaswi kumfanya Mkristo wa kweli ashiriki katika desturi zisizompendeza __________________________ . (Mez. 29:25; Mt. 10:28) [w98-SW 7/15 uku. 20 fu. 5]
22. Katika kutoa ushahidi mbele ya Mfalme Agripa, Paulo alitumia __________________________ , akikazia mambo ambayo juu ya hayo yeye na Agripa __________________________ . (Mdo. 26:2, 3, 26, 27) [w98-SW 9/1 uku. 31 fu. 3]
23. Kwa kuwa Mungu __________________________ , huenda wengine wakafikiri kwamba yeye si mtu, lakini vipindi vingi na vyenye uangalifu vya __________________________ vitasaidia mtu ‘kumwona Yeye asiyeonekana.’ (Ebr. 11:27) [w98-SW 9/15 uku. 21 maf. 3-4]
24. Kama inavyoonekana katika kisa cha jenerali Msiria __________________________ , nyakati nyingine mtu hupata faida kubwa kutokana na __________________________ kudogo tu. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w99-SW 2/1 uku. 3 fu. 6–uku. 4 fu. 1.]
25. Kama vile moyo wa Yehonadabu ulivyokuwa pamoja na Mfalme Yehu, __________________________ leo unatambua kwa moyo wote na kushirikiana na Yehu Mkubwa Zaidi, __________________________ , anayewakilishwa duniani na __________________________ . (2 Fal. 10:15, 16) [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w98-SW 1/1 uku. 13 maf. 5-6.]
Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:
26. Ni (Shetani; Yehova; Yoabu) ndiye alimchochea Daudi ‘kuhesabu Israeli na Yuda.’ (2 Sam. 24:1) [4, Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w92-SW 7/15 uku. 5 fu. 2.]
27. Kwa kupatana na 1 Wafalme 8:1 na Mhubiri 1:1, Solomoni alikutanisha watu ili (kujenga hekalu; kufuatilia maadui wa Israeli; kumwabudu Yehova). [7, Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona si-SW uku. 112 fu. 3.]
28. Ile miaka 20 ambayo katika hiyo Solomoni alijenga hekalu na nyumba yake katika Yerusalemu inaweza kulinganishwa na kipindi cha marekebisho ya kimafundisho na ya kitengenezo kilichoanza katika (1919; 1923; 1931) na kilichomalizika katika (1938; 1942; 1950). (1 Fal. 9:10) [8, Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w92-SW 3/1 uku. 20 kisanduku.]
29. Neno “mbingu” kama linavyotumiwa kwenye 2 Wafalme 2:11 linaelekeza kwa (makao ya kiroho ya Mungu; ulimwengu halisi; angahewa ya dunia, ambako ndege huruka na pepo huvuma.) [13, Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w97-SW 9/15 uku. 15 kisanduku.]
30. (Herode Mkuu; Kaisari Augusto; Tiberio Kaisari) ndiye aliyeamuru kufanya hesabu ya idadi ya watu hivi kwamba tokeo likawa kuzaliwa kwa Yesu katika Bethlehemu badala ya Nazareti. [16, w98-SW 12/15 uku. 7 kisanduku]
Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nazo:
Zab. 15:4; 2 Sam. 12:28; 2 Sam. 15:18-22; 2 Fal. 3:11; Kol. 3:13
31. Ukichwa katika mpango wa kitheokrasi wa Yehova unapaswa kuheshimiwa. [4, si-SW uku. 63 fu. 30]
32. Uaminifu-mshikamanifu kwa tengenezo la Yehova na wawakilishi walo lazima udumishwe. [4, si-SW uku. 63 fu. 30]
33. Uthamini kuelekea rehema ya Yehova unaweza kuchochea mtu awe mwenye kujizuiza na mwenye kufunika makosa. [11, w98-SW 11/1 uku. 6 fu. 3]
34. Ni pendeleo kuonyesha ukaribishaji-wageni na kuhudumia kwa unyenyekevu watumishi waaminifu wa Yehova walio katika utumishi wa pekee. [13, Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w97-SW 11/1 uku. 31 fu. 1.]
35. Mtu mwenye kumwogopa Mungu hufanya yote awezayo ili kutimiza ahadi yake ya kulipa deni zake, hata ikiwa hali zisizotazamiwa zinafanya iwe vigumu zaidi kuliko ilivyotazamiwa. [15, w98-SW 11/15 uku. 27 fu. 1]