Kujikumbusha Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maulizo ya kujikumbusha yanayofuata yatatumiwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi katika juma tokea tarehe 26 mwezi wa 4, 2010. Kwa dakika 20, mwangalizi wa shule ataongoza kujikumbusha kunakotegemea habari zilizozungumziwa tokea tarehe 1 mwezi wa 3 mpaka tarehe 26 mwezi wa 4, 2010.
1. Naomi alimaanisha nini aliposema “Yehova ndiye amenifedhehesha na Mweza-Yote ndiye amenisababishia msiba”? (Ruthu 1:21) [w05 3/1 uku. 27 fu. 2]
2. Ni sifa gani zilizomfanya Ruthu ajulikane kuwa “mwanamke bora”? (Ruthu 3:11) [w05 3/1 uku. 28 fu. 6]
3. Namna gani maneno ya Elkana “Je, mimi si bora kwako kuliko wana kumi” yalimtia nguvu muke wake? (1 Sam. 1:8) [w90 3/15 uku. 27 fu. 5-6]
4. Ni nini kilichofanya ombi la Waisraeli la kupata mfalme liwe lisilofaa? (1 Sam. 8:5) [w05 9/15 uku. 20 fu. 17; it-2-F uku. 827 fu. 1]
5. Namna gani Samweli aliyekuwa ‘amezeeka na mwenye imvi,’ alijionyesha kuwa mfano mzuri katika kusali kwa ajili ya wengine, na hilo linaonyesha nini? (1 Sam. 12:2, 23) [w07 6/1 uku. 29 fu. 14-15]
6. Kwa nini Sauli aliwaonyesha Wakeni wema kwa njia ya pekee? (1 Sam. 15:6) [w05 3/15 uku. 22 fu. 10]
7. Kwa nini Sauli alimwuliza Daudi, “Wewe mvulana, wewe ni mwana wa nani?” (1 Sam. 17:58) [w07 8/1 uku. 31 fu. 3, 5]
8. Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Daudi alivyoshugulikia tatizo nzito huko Gathi? (1 Sam. 21:12, 13) [w05 3/15 uku. 24 fu. 4]
9. Namna gani Yonathani alionyesha upendo na unyenyekevu alipoona kuwa jambo la lazima kumwunga mkono na kumtia moyo rafiki yake Daudi? (1 Sam. 23:17) [lv uku. 28 fu. 10, maelezo ya chini.]
10. Tunajifunza nini kutokana na kukutana kwa Sauli na mchawi katika En-dori? (1 Sam. 28:8-19) [w05 3/15 uku. 24 fu. 7]